Jinsi ya kuchaji maji

Jinsi ya kuchaji maji

Elimu inazidi kuwa ghali, na wanadamu wazidi kuwa malimbukeni. Ahsante mshana jr kwa elimu hii adhimu na ya bure!
 
Wapendwa wakati tukisubiria jukwaa letu lianzishwe (jukwaa la mambo ya kiroho ama jukwaa la mambo ya giza) tuendelee mdogo mdogo huku HM.

Kwanza lazima ifahamike wazi kwamba maji ndio yanachukua asilimia 75 ya mwili wa mwanadamu na asilimia hiyo hiyo kwenye dunia katika ujumla wake.
Ni katika hayo maji kuna aina zake tofauti
1. maji baridi na maji chumvi
2. maji mfu na maji hai

Maji baridi ni yale ya kwenye mito mabwawa na baadhi ya maziwa wakati yale majimoto (majichumvi) ni yale ya baharini

Maji mfu ni yale maji ya viwandani yaliyochanganywa na kemikali mbalimbali, haya maji tunayoita special, maji ya chupa

Maji hai ni maji asili ambayo hayajapitia mkondo wa kuyasafisha kwa kutumia kemikali zozote. Maji baridi na maji chumvi pia ni maji hai

Kwenye mambo haya ya kiroho wengine huita ya gizani, maji yana matumizi yake pia. Hasa kwenye kutakasa, kunuia, kubariki, kubatiza nakadhalika. Na ili upate maji husika yenye nguvu ya kutenda katika hayo inabidi ufanye yafuatayo;
1. weka maji baridi kwenye bakuli
2. weka kiasi kidogo cha chumvi
3. weka kipande cha jiwe angavu/jiwe kioo(quartz stone) kwenye bakuli husika
4. weka bakuli lako kwenye kiambaza ambapo mwanga wa mwezi mpevu utafika moja kwa moja na kwa urahisi..
5. Alfajiri toa bakuli lako weka maji kwenye chupa safi tayari kwa matumizi husika...!!!

Maji haya hayahusiani na ulozi wala ushirikina yoyote anaweza kuyatumia kama kinga na tiba ya nguvu hasi na roho hasi



Sent using Jamii Forums mobile app
uko vzuri Sana Mshana
 
Back
Top Bottom