Jinsi ya kuacha kuvuta sigara (A Guide to Quitting Smoking)

Habarini wanajukwaa mimi ni mvutaji mzuri wa bangi na sigara nataka kuacha lakini nimeshidwa.ni saidieni njia rahisi za kukata hamu ya kuvuta sigara...
 
1505013_247551232077688_1023546303_n.jpg
 
Mkuu MziziMkavu unataka kiwanda cha sigara kifungwe?

Kauli mbiu yao:thank you for smoking!
Hhahahah ikipatikana dawa ya kuacha kuvuta Sigara ninafikiri Serikali pia itapiga marufuku hizo dawa zisiuzwe kabisa maana kiwanda cha Sigara kitafungwa na Serikali itapata hasara kwa dawa hizo za kuacha kuvuta Sigara. Hakuna hata Serikali moja duniani inayopiga vita Sigara Serikali za dunia ni kupiga vita Madawa ya kulevya wakati Aduwi mkuu wa binadamu Sigara Serikali za dunia zimenyamaza kimya tu.
 
SIGARA hata utumie nini!!! Huwezi kuacha! Dawa ya kuacha SIGARA ni wewe mwenyewe ukiamua! Chezeya kiu ya Fegi wewe!
 
Jamani ktk kitu kinacho nitesa moyo wangu ni sigara.
Nimekuwa mtumiaji wa sigara kwa miaka mingi sana,Nimejaribu kuacha sii chini ya mara 20.Na nimechemka hivyo jamani nisaidieni mbinu za kuacha sigara .
 
Personal conviction kwamba huitaki na unaweza kuishi bila kuvuta ndo dawa kuu na muhimu ya kuacha kuvuta sigara!!!!
 
...wacha mambo ya kitoto,kwani ulipoamua kuanza kuvuta hayo masigara yako ulimshauru mtu?dawa ni moja tu,kama ulivyoamua kuanza kuivuta sigara,basi leo amua kuwacha kuvuta sigara.hio ndio dawa.
 
Anza na nia dhabiti na dhati ya kuamua kuacha kuvuta. Ukishaacha jitahidi kunywa maji ya kutosha kila unaposikia hamu ya kuvuta sigara. Pia kunywa maji mara kwa mara. Hii inasaidia kupunguza sumu 'nicotine' iliyomo mwilini. Pia uwe unaoga ikiwezekana si chini ya mara 3 kwa siku. Ahsante
 
Mkuu Zingatia Kuwa Huwezi Kukatiza Uvutaji Ghafla Bali Kwa Hatua.
Njia Ya Kwanza:
Kunywa Chai Rangi Mara Ukiamka Asubuhi,kisha Saa 12 Jioni Na Saa 3 Usiku
Njia Ya Pili:
Kunywa Maji Kila Unapohisi Kiu Ya Sigara.
 
Mkuu Zingatia Kuwa Huwezi Kukatiza Uvutaji Ghafla Bali Kwa Hatua.
Njia Ya Kwanza:
Kunywa Chai Rangi Mara Ukiamka Asubuhi,kisha Saa 12 Jioni Na Saa 3 Usiku
Njia Ya Pili:
Kunywa Maji Kila Unapohisi Kiu Ya Sigara.

Lkn pia jitaidi kuwa vitu vya kutafuna tafuna km big g, pipi, karanga nk pindi usikiapo ham unatumi izo vitu
 
Dawa ni KUAMUA tu...
Hakuna sigara inayomfuata mtu isipokuwa wewe ndie unaifuata....acha kuifuata...
 
Huo ni ugonjwa tusimbeze, anatatizo! Kwa kuwa umetambua na kuamini kuwa uvutaji wa sigara unaathari ktk afya yako huo ni mwanzo mzuri kwa tiba ya kuacha uvutaji. Nafaham tiba ya asili hii; Chukua sigara zidumbukize katika maziwa mgando kwa muda wa masaa mawili, then zitoe na kuzianika juani mpaka zikauke vizuri. Mara upatapo kiu ya sigara chukua kati ya zile ulizo anika juani na uvute kukata kiu yako! Ukitapika kwa sababu ya uvutaji ni dalili nzuri ya kuwa dawa hyo inakufaa. Endelea kuzivuta mpaka hamu ya sigara itakata yenyewe!
 
1469806_247052712116318_1990078125_n.jpg



Miongoni mwa mambo magumu kabisa katika ufanikishaji wake ni mtu kuachana na uvutaji wa

sigara. Watu wengi wamekuwa wakionywa kuachana na uvutaji wa sigara kwa sababu ya madhara

yake, lakini wamekuwa wakishindwa kutokana na kukolewa na kiwango cha Nikotini inayopatikana katika tumbaku.


Vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika uvutaji kwa kufuata mkumbo, lakini baadaye

wanapokuja kutambua kuwa wako katika hatari ya kuambukizwa au pengine wana ugonjwa wa

kifua kikuu, wanakuwa katika wakati mgumu wa kuachana na uvutaji huo. Wengi wao wamekufa

huku makundi kwa makundi wakitangatanga kutafuta suluhu ya kuchana na uvutaji, si tu kwa

sababu ya kuhofia ugonjwa, bali hata kukosa uwezo wa kununua bidhaa hiyo.


Hata hivyo idadi kubwa ya wanaojaribu kuacha wamejikuta wakipata majibu ya kutoweza, kutokana

na kusumbuliwa na hamu ya uvutaji, umbumbu wa mawazo pindi wanapokaa muda mrefu bila

kuvuta, kuumwa na kichwa na hata udhaifu katika kukumbuka vitu au mambo waliyofanya au

waliyopanga kuyatenda.


Pamoja na yote hayo watalaam na washauri wa masuala uvuaji wa sigara wanasema wanaopatwa

na hayo wamekosa mbinu na muongozo wa kuwasaidia waachane na uvutaji wa sigara bila kupata madhara.


Kwa ufupi somo hili limehusisha uchunguzi wa kina pamoja na kumbukumbu za kitaalamu kutoka

kwa washauri kama Anderson JE, Jorenby DE, Scott WJ, Fiore MC, Bailey WC, Cohen SJ, ambao

wote kwa pamoja kupitia vituo vyao kikiwemo cha US Department of Health and Human Services

na Public Health Service walishawahiwa kueleza mbinu salama za kuachana na uvuaji wa sigara.

Zifuatazo ni dondoo kadhaa za kufuata ili mvutaji aache sigara kwa usalama.


1* Mvutaji lazima afahamu ni muda gani ambao huwa anavuta sigara kwa wingi, je ni wakati akiwa

amelewa au akiwa na mawazo mengi ya kimaisha? Akishafahamu hilo ajiulize ni kiwango gani cha

sigara ambacho huwa unavuta kwa siku?


2*Baada ya hapo achukua kitabu chake cha kumbukumbu na aandike muda huo ambao yeye

huvuta sigara kwa wingi. Ajiulize kwa nini huwa unavuta, atathimini madhara ya uvutaji wa sigara

kwake binafsi na kwa familia yako.


3* Kaa chini upitie kwa makini kumbukumbu zako za muda na kiwango cha sigara unazovuta kwa

nyakati hizo, kisha panga utaratibu mpya. Kwa mfano kama unavuta sana wakati ukiwa kwenye

mawazo hakikisha kuwa unapoanza kufikiria juu ya jambo fulani uwe na kitu mbadala kitachukua

nafasi ya sigara. Mfano kahawa au chai? Hakikisha kila penye hamu ya uvutaji unaweka kitu kingine

mbadala cha kufanya zaidi ya kuvuta sigara.


4*Ondoa masalio ya sigara katika sehemu ambazo unaishi, fua nguo zote na vitambaa ili kuondoa

harufu ya sigara katika eneo unalokuwepo. Usikae karibu na mtu anayevuta, usikubali kuwa

mshirika wa mvutaji na usiwe mtu wa kuendekeza sana msukumo wa mwili unaotaka uvute, bali

kila unapowaza juu ya kuvuta fikiria madhara na nia yako ya kuacha.


5*Wafahamishe rafiki zako kuwa umeamua kuachana na uvutaji, ili upate watu wa kuwaonea aibu

pale utakapoanguka na kurudia uvutaji wa sigara. Panga tarehe ya kuacha na iwe kwenye

kumbukumbu.


6*Wakati ukiiendea tarehe hiyo ya kuacha hakikisha unapunguza kiwango cha uvutaji kadiri

unavyoisogea siku hiyo. Jipangie muda mrefu zaidi ya kuvuta kulingana na kiwango chako cha

uvutaji na kuendelea kuuongeza kila siku ili uzoee kukaa saa nyingi bila kuvuta.


7*Fuata ratiba mbadala uliyojiwekea kuziba pengo la uvutaji, kama umepanga kutumia kahawa kila

unapokuwa mpweke sebuleni hakikisha unajizoeza ili ikifika tarehe yako ya kuacha usiwe mtu wa

kujiuliza cha kufanya nyakati ambazo utakuwa na hamu ya sigara.


8*Lengo lako liwe ni kufanikiwa na usikate tamaa utakaposhindwa kufanikisha lengo lako kwa

wakati uliojipangia. Mara kwa mara nenda kamuone daktari mshauri ili akupe muongozo zaidi wa

kukusaidia na ikiwezekana akupe nafasi ya kuwatembelea wagonjwa waliopata ugonjwa wa kifua

kwa sababu ya kuvuta sigara.


Kwa kifupi hizo ni dondoo chache tu za kukusaidia kuachana na uvutaji wa sigara, lakini mara

nyingi kinachoweka nguvu za kufanikisha uachaji wa sigara ni utashi wa mtu ambao hutokana na

tathimin ya kina ya muhusika na mtazamo wake juu ya sababu za kuacha. Mara nyingi

wanaoshindwa ni wale ambao hawakuzitia nguvu sababu za kuacha kwao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom