Jinsi Vimbunga/Dhoruba (Hurricanes/Storm) vinavyopewa Majina

wadau nimekaa na kutafakari sijapata jibu ni kwanini haya majanga ya kimbunga na mafuriko yanayotokea zaidi marekani tangu miaka ya 1950 hadi hivi leo yanapewa majina ya kike kama KATRINA,ALICE,NK kwa sasa kilichotokea wekend hii wamekiita IRENE. mwenye ufahamu atujuze ni kwanini?
Nenda kagoogle, andika history of hurricane names utajibiwa maswali yako yote likiwemo la kwa nini majina ya wanawake yatumika sana.
 
Majina hutolewa na 'watabiri wa hali ya hewa' meteorologists. Sababu ya kutoa majina ni kuwa kwa msimu mmoja kunaweza kuwa na hurricanes au storms nyingi na hivyo itarahisisha utambuzi. Kama nipo sahihi hurricanes ni dhoruba na storms ni vimbunga. upo uwezekano wa kupanda au kushuka daraja kutoka hurricanes hadi storms. .



senti sumuni yangu

Nguruvi, kimbunga ni hurricane, storm ni mvua kubwa/nyingi yenye pepo kali na radi
 
Majina ya VimbungaVimbunga hutokea mara kwa mara katika kipindi cha joto. Wataalamu wameanza kuvipa majina kwa kurahisisha maelewano. Katika eneo la kila bahari kuna utaratibu wa pekee wa kutolea majina kwa vimbunga kufuatana na mapatano ya wanasayansi.
Atlantikiinaona takriban vimbunga kumi au zaidi kila mwaka. Hupewa majina kufuatana alfabeti. Imekuwa kawaida tangu 1979kutumia majina ya kiume na ya kike kwa kubadilishana (zamani vilipewa majina ya kike tu lakini wanawake walilalamika).
Wataalamu wanatumia orodha sita ya majina hivyo jina linaweza kurudia baada ya miaka sita.
Kimbunga ya "Katrina" kilichoharibu mji wa New Orleans katika Agosti 2005 kilikuwa kimbunga cha 11 cha mwaka 2005. Kilifuata kimbunga "Jose" na kufuatwa na "Lee" halafu "Maria". Kama kimbunga inasababisha uharibifu mkubwa sana jina lake huondolewa katika orodha maana yake jina hili halitarudia. "Katrina" imebadilishwa kuwa "Katia" katika orodha ya mwaka itakayotumika mwaka 2011 (ikitokea itakuwa kimbunga kinachofuata "Jose" ya 2011)
mi unazidi kunipoteza
 
Mwenye ufahamu naomba anijuze kwanini vimbunga vingi huitwa majina ya kike mfano hiki kimbunga kilichotokea Uingereza kuitwa kimbunga Dorisi.
 
Mkuu...

Hii system ya kutajia majina vimbunga ilianza mwanzo mwa 1900s. Vilikuwa vinapewa majina yoyote tu mpaka mid-90s pale ilipoanzishwa system ya kutajia vimbunga majina ya kike.

Lakini 1979 vimbunga vilianza kupewa majina ya kiume pia. Kwahiyo ishu ya majina isikuchanganye sana mkuu..

Vimbunga vinapewa majina tu kwa ajili ya kupunguza ma-technical terms na numbers ili kurahisisha tu mawasiliano kwa watu tusio na ujuzi na hizo mambo za hali ya hewa.
 
Back
Top Bottom