Jinsi Vimbunga/Dhoruba (Hurricanes/Storm) vinavyopewa Majina

Wataalamu wa Hali ya Hewa katika eneo ambalo linaathiriwa na vimbunga, kwa mfano nchi zote ambazo ziko karibu na bahari ya hindi, hukutana kabla ya msimu wa vimbunga ili kutoa mjina ya vimbunga hivyo, na kila nchi inawasilisha majina na hatimaye wanakuwana majina ya imbunga(list) kwa msimu huo. List ya majina huanzia A hadi Z. Kimbunga cha kwanza kitapewa lile jina linaloanzia na A, na cha tatu jina linaloanzia na C, n.k. kutoka katika list iliyoandaliwa

Majina ni ya mchanganyiko, ya kike na kiume na sio kweli kuwa majina huwa ya kike. Katika bahari ya Hindi, msimu wa vimbunga ni kuanzia Nov hadi April. List ya majina lazima iasilishwe WMO na hayatawi kufanana na majina ya bahari nyingine.

Mara nyingi vimbunga vyenye majina ya kike vimekuwana nguvu sana kuliko vile vyenye majina ya kiume
 
Baadhi ya vimbunga vikubwa vinavyotokea duniani hutajwa kwa majinam mfano Kimbunga cha Katrina,Mathew...nk

Tusaidiane ni vigezo gani hutumika kuvipa majina vimbunga hivi

Karibuni
 
Mi ninavyofahamu vimbunga vyote huwa vina majina ya kike-rita,katrina,sasha sababu yangu binafsi isiyokuwa na utaalamu wowote ni kuwa mwanamke ndo chanzo cha majanga yote duniani!
 
Mi ninavyofahamu vimbunga vyote huwa vina majina ya kike-rita,katrina,sasha sababu yangu binafsi isiyokuwa na utaalamu wowote ni kuwa mwanamke ndo chanzo cha majanga yote duniani!

THAT'S THE POINT MAN.

Ndio Maana mie huwa nawagonga nawabanjua then nawatema nasepa mbele..
Sitaki kukaa nao muda mrefu wasije kunipa majanga buree...

[HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng
 
Huricane ni aina ya pepo ambayo huvuma kwa speed ya km ,60 kwa saa na hutokea katika mgandamizo mkubwa wa bahari ya pacific..ndo maana nikasema hutokana na aina ya upepo
 
Huwa kila msimu wa kimbunga unapoanza na ndipo majina yanaanza kwa mpangilio wa alphabet. Inaanza na A kwa kimbunga namba moja kuendelea mpaka Z kwa cha mwisho. Lakini msimu sababu ni miezi kadhaa huwa alphabet hazifiki mwisho.
Huricane center huko America watatoa jina walipendalo kutokana na mtiririko huo.
 
pia Mimi ujiuliza mbona vimbinga hivi havjawahi kuitwa majina ya ule upande mwengine kama mudy hadja husna aicha n.k
 
Baada ya hiki Mathew kinachofuata kitakuwa na herufi N mwanzo.
 
wadau nimekaa na kutafakari sijapata jibu ni kwanini haya majanga ya kimbunga na mafuriko yanayotokea zaidi marekani tangu miaka ya 1950 hadi hivi leo yanapewa majina ya kike kama KATRINA,ALICE,NK kwa sasa kilichotokea wekend hii wamekiita IRENE. mwenye ufahamu atujuze ni kwanini?

Wnamaa kubwa sana | HAKINA HURUMA
 
Umewahi kusikia vimbunga vikiwa na majina ya kushangaza, mfano cha sasa kinachoitwa Matthew ambayo kimekumba maeneo ya Haiti, Jamaica, Jamhuri ya Dominika, Bahamas na baadhi ya majimbo ya Marekani.
Mwezi uliopita kulikuwa na kimbunga kingine kilichojulikana kama Hermine ambacho kilisababisha uharibifu mkubwa jimbo la Florida.
Lakini kinachokumbukwa sana ni kile kwa jina Katrina ambacho kiliathiri sana majimbo ya Louisiana, Mississippi na Alabama nchini Marekani.
Je, vimbunga hivi hupewa vipi majina?
Vimbunga vinavyopewa majina
Vimbunga katika maeneo ya bahari ya Atlantiki, maeneo ya Caribbean na Ghuba ya Mexico hupewa majina ya Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambalo lina makao yake makuu nchini Uswizi.
Zamani, ni majina ya kike pekee yaliyotumiwa lakini kuanzia 1979, majina ya kiume yalianza kutumiwa. Huwa kuna makundi sita ya majina ambayo hutumiwa kwa mzunguko.

Hii ina maana kwamba majina yaliyotumiwa kwenye vimbunga mwaka hu hayatatumiwa tena hadi 2022.

Majina kwenye orodha hii yanaweza kubadilishwa na WMO.

Orodha hii ilianza kutumiwa mwaka 1979. Kabla ya hapo, jina la kimbunga Fern lilibadilishwa mwaka 1966 na badala yake kukatumiwa Frieda. Hakuna sababu iliyotolewa.

_91541721_storm_names.jpg
Image copyrightWORLD METEOROLOGICAL ORGANISATION
Majina yanavyoacha kutumiwa
Baadhi ya majina huacha kutumiwa, sana kunapotokea uharibifu mkubwa au hasara kubwa hivi kwamba kutumia tena jina hilo kutafufua kumbukumbu zenye uchungu.

Mfano ni kimbunga Katrina kilichoua watu 2,000 mwaka 2005 na kusababisha uharibifu mkubwa Marekani. Kimbunga hicho kiliwaacha watu milioni moja bila makao. Mji wa New Orleans, Louisiana uliathirika sana.

Kando na Katrina, kuna majina mengine ambayo yameacha kutumiwa. Mitch, kutokana na kimbunga cha mwaka 1998 kilichoua watu 11,000 Honduras na Nicaragua, halitumiwi tena. Kimbunga hicho ndicho kibaya zaidi kukumba maeneo ya Magharibi mwa dunia katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

_91010091_getty_mitch.jpg
Image copyrightGETTY IMAGES
Kimbunga Sandy cha mwaka 2012 na Kimbunga Irene 2011 pia vilisababisha uharibifu mkubwa. Majina hayo hayatumiwi tena.

Kimbunga hatari zaidi kuwahi kukumba Marekani kilitokea 1780, ambapo kiliua watu 22,000 maeneo yaMartinique, Barbados na St Eustatius.

Wakati huo majina hayakuwa yameanza kutumiwa kurejelea vimbunga.

Majina yaliyoacha kutumiwa tangu 1954.
_91541722_retired.jpg
Image copyrightNATIONAL HURRICANE CENTER
Majina maeneo mengine duniani
Katika maeneo mengine duniani, huwa kuna utaratibu tofauti wa kuvipa majina vimbunga.

Lakini majina yote hupitia kwa WMO.
Chanzo BBC

Kwa mfano, maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Pasifiki na Bahari ya China Kusini, kuna jedwali la majina ambalo kila taifa linaloathirika huchangia.

Baada ya kimbunga kutokea, kimbunga kinachofuata hupewa jina linalofuata.

Kwa mfano, kimbunga cha kwanza huitwa Damrey (kimbunga cha kwanza Cambondia) na kitakachofuata kinafaa kuitwa Kaikui (jina la kwanza China).

Kimbunga cha sasa maeneo hayo ni Chaba (jina la nafasi ya nne Thailand).

Kilichotokea majuzi kiliitwa Megi na ambacho kiliathiri maeneo ya China na Taiwan. Jina hilo ni la nafasi ya nne chini ya majina ya Korea Kusini.

_91010728_pacific.jpg

Majina ya vimbunga na tufani yalianza kutumiwa Uingereza na Ireland, kwa majaribio.

Kuna jina kwa kila alfabeti, isipokuwa Q, U, X, Y na Z, ambao ndio utaratibu unaotumiwa kuvipa majina vimbunga Atlantiki Kaskazini.
Chanzo BBC
 
Back
Top Bottom