Majina ya vimbunga

kishamawe

JF-Expert Member
Jun 20, 2020
267
360
Kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza haya majina ya vimbunga. Mfano hicho kimbunga huko Nchini Zambia kinaitwa FREDDY miaka ya Nyuma kulitokea vimbunga Nchini Marekani wajuvi wanapenda kupaita U.S.A vimbunga vilikuwa na majina Catalina na mengine nimesahau.

Hoja yangu ni kwa nini vimbunga hivi hupewa majina kama ya binadamu vile na je kwa nini majanga mengine huwa hayapewi majina mfano matetemeko ya ardhi, mvua , ukame n.k japo huwa nasikia kipimo cha Tetemeko lenye ukubwa wa kipimo cha litcher kiasi fulani, wale wajuzi wasomi nipeni kupata uelewa wa hayo majina ya vimbunga yanapatikana vipi, ila wale wasio na uelewa watakuja na majibu ya mara usiwe unaandika kama unakimbizwa n.k nawasilisha kwenu
 
Niongeze! Sijasikia kimbunga kinaitwa juma, mudi, maimuna yaani kwa majina ya kisilamu
 
Majina ya vimbunga. yanapewa kwa Alphabet, A to Z. Kinachotokea hizo alphabets zinahuishwa kama vile A for Alfred, B for Bernard, C for Catherine, D for David na kadahlika. Kwa kuwa vimbunga iwe typhoons, cyclones au hurricanes kulingana na bahari inapotokea huwa vingine vinaishia kwenye levels tofauti kulingana na madhara ndio maana huishia majina ya kati. Kama hilo Freddy maana yake ni kimbunga cha 6, letter F ambacho kimeweza kufika huko. Kama kuna kingine kitakuja kitaendela letter G, inaweza kuwa Gloria au Grace, kama kitaishia katikati kwa level ya chini hakitasomeka labda mbele tena huko kwenye letter M, N na kuendelea mpaka Z
 
kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza haya majina ya vimbunga. Mfano hicho kimbunga huko Nchini Zambia kinaitwa FREDDY miaka ya Nyuma kulitokea vimbunga Nchini Marekani wajuvi wanapenda kupaita U.S.A vimbunga vilikuwa na majina Catalina na mengine nimesahau. Hoja yangu ni kwa nn vimbunga hivi hupewa majina kama ya binadamu vile. na je kwa nn majanga mengine huwa hayapewi majina mfano matetemeko ya ardhi, mvua , ukame n.k japo huwa nasikia kipimo cha Tetemeko lenye ukubwa wa kipimo cha litcher kiasi fulani, wale wajuzi wasomi nipeni kupata uelewa wa hayo majina ya vimbunga yanapatikana vipi, ila wale wasio na uelewa watakuja na majibu ya mara usiwe unaandika kama unakimbizwa n.k nawasilisha kwenu
Litcher ndo mgunduzi wa hicho kipimo,kuenzi jina lake ndo wakawa wanaita hivyo.
 
Back
Top Bottom