Jinsi Vimbunga/Dhoruba (Hurricanes/Storm) vinavyopewa Majina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi Vimbunga/Dhoruba (Hurricanes/Storm) vinavyopewa Majina

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Kunguru Mjanja, Aug 28, 2011.

 1. Kunguru Mjanja

  Kunguru Mjanja JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2011
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 1,667
  Likes Received: 2,499
  Trophy Points: 280
  kimbunga.jpg

  Kwanini vimbunga vinapewa majina?

  Hii ni ili kuwarahisishia wataalamu wa hali ya hewa kuweza kufuatilia vimbunga hivyo, na pia kuwapa urahisi kwa watu kufuatilia ili kujua vimbunga hivyo vinaelekea wapi waviepuke.

  Pia sehemu nyingine kunaweza kupatwa na vimbunga zaidi ya 100 ndani ya miezi 12, hivyo majina yameweza kuwarahisha wataalamu kutofautisha vimbunga hivyo.

  Watabiri wanasema majina mafupi, tofauti tofauti ya vimbunga yanarahisisha kwenye mawasiliano na kusaidia kuondoa kutokuelewana.

  Nani anafanya uamuzi wa majina?
  Kuna mikutano ya kila mara ya wanasayansi wa mambo ya hali ya hewa duniani kote ili kuamua majina mapya ya vimbunga yatakayotumika mwaka unaofuata.

  Uingereza, ofisi za watu wa hali ya hewa huwaambia wananchi kupendekeza majina.

  Nani anaamua jina la kike au kiume kutumika?
  Vimbunga vinapokezana kwa kupewa majina ya kike na ya kiume.

  Vimbunga vinapewaje majina yake?
  Katika mwaka 1950, Kituo cha vimbunga cha kitaifa cha Marekani kilianza kutumia majina maalum kwa vimbunga. Kwa sasa Shirika la hali ya hewa Duniani ndilo linalo simamia na boresha orodha ya majina.

  Vimbunga awali vilikuwa vikitambulika kwa kutumia namba za latitude-longitude.

  Baada ya hapo vimbunga vilikuwa vinapewa majina kwa kutumia herufi, na kwa mtindo wa kutamka herufi hizo ulikuwa kama wa Jeshi, kama Adam, Baker, Charlie, na majina haya yalikuwa yanatumika kila msimu wa vimbunga.

  Mwaka 1953, shirika lilianza kutumia majina ya kike na kuachana na njia hiyo ya kutumia herufi kila msimu. Mwaka 1979 majina ya kiume yalianza kutumika.
  _91541722_retired.jpg
  Pichani ni majina ya Vimbunga yaliyowahi kutumika kuanzia mwaka 1954 hadi 2015

  Majina hutofautishwa katika bahari kuu za dunia kama vile Pacific, India na Antilantic. Majina ya Vimbunga vya Bahari ya Pacific ni Tofauti na majina ya Bahari ya Hindi ili kuondoa ukinzani wa kurudia majina.

  Vimbunga katika maeneo ya bahari ya Atlantiki, maeneo ya Caribbean na Ghuba ya Mexico hupewa majina ya Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambalo lina makao yake makuu nchini Uswizi.

  Kwa sasa majina ya kike na kiume yapo kwenye orodha sita tofauti na wataalam wanatumia orodha hizo kwa zamu. Hii inamaanisha kwamba orodha ya mwaka huu itatumika tena mwaka 2023. Orodha hizi za majina zilianza kutumika kuanzia mwaka 2016.
  _91541721_storm_names.jpg
  Pichani ni orodha sita za majina ya vimbunga ambayo hutumika katika maeneo ya bahari ya Atlantiki, maeneo ya Caribbean na Ghuba ya Mexico.

  Maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Pasifiki na Bahari ya China Kusini, kuna jedwali la majina ambalo kila taifa linaloathirika huchangia.

  Baada ya kimbunga kutokea, kimbunga kinachofuata hupewa jina linalofuata.

  Kwa mfano, kimbunga cha kwanza huitwa Damrey (kimbunga cha kwanza Cambondia) na kitakachofuata kinafaa kuitwa Haikui (jina la kwanza China).
  _91010728_pacific.jpg
  Orodha ya Majina ya vimbunga katika Maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Pasifiki na Bahari ya China Kusini

  Hakuna majina yanayoanziwa na herufi Q, U, X, Y or Z kwenye orodha ya majina.

  Kama kutatokea vimbunga zaidi ya 21 kwa mwaka mmoja, kama ilivyokuwa 2005, wataalamu wa hali ya hewa wanatumia herufi za kigiriki kuongeza kuvipa majina vimbunga hivyo vilivyoongezeka.

  Majina ya vimbunga na tufani yalianza kutumiwa Uingereza na Ireland, kwa majaribio.

  Muda gani majina ya vimbunga hayatumiki tena?
  Muda pekee ambapo majina ya vimbunga yanaachwa kutotumika tena na kutokuwa kwenye orodha ya majina ni pale yanapostaafishwa.

  Majina ya vimbunga yaliyoleta madhara makubwa sana hayatumiki tena.

  Mfano, Kimbunga Katrina jina lake halitumiwi tena kutokana na kufanya uhalibifu mkubwa New Orleans mwaka 2005.

  Kimbunga Mitch, kutokana na kimbunga cha mwaka 1998 kilichoua watu 11,000 Honduras na Nicaragua, halitumiwi tena. Kimbunga hicho ndicho kibaya zaidi kukumba maeneo ya Magharibi mwa dunia katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

  Kimbunga Sandy cha mwaka 2012 na Kimbunga Irene 2011 pia vilisababisha uharibifu mkubwa. Majina hayo hayatumiwi tena.

  Kimbunga hatari zaidi kuwahi kukumba Marekani kilitokea 1780, ambapo kiliua watu 22,000 maeneo ya Martinique, Barbados na St Eustatius.

  Mifano hii yote ya vimbunga hivi, ni wakati orodha ya majina haijaanza kutumika. Japo hata wakati huu wa kutumia orodha ya majina endapo kimbunga kitafanya uharibifu jina lake halitatumika tena.
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wadau nimekaa na kutafakari sijapata jibu ni kwanini haya majanga ya kimbunga na mafuriko yanayotokea zaidi marekani tangu miaka ya 1950 hadi hivi leo yanapewa majina ya kike kama KATRINA,ALICE,NK kwa sasa kilichotokea wekend hii wamekiita IRENE. mwenye ufahamu atujuze ni kwanini?
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Haaa Hurricane Irene da hata mie nashangaaaaaa!!!! Ngoja tuone wataalamu wakikujibu..
   
 4. naumbu

  naumbu JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 3,304
  Likes Received: 3,786
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu zinakuja na kuondoka na kila kitu unaachwa mweupe just like women
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Zamani vimbunga vilikuwa na majina ya kike tu lakini baadae vikaanza kujumuisha majina ya kiume pia. Kuna hurricane Chris kwa mfano.

  Bahati mbaya inasadifu kuwa vimbunga vikali vimetokea vikiwa na majina ya kike kwa miaka hii ya karibuni.
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  kuna ivan,hiyo ndo kiboko. bt maybe u shldnt mess with women,lol
   
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Vimbunga ni alama ya hasira. Na kati ya mwanaume na mwanamke nani ana hasira kubwa/kali? Ogopa mwanamke akikasirika ndugu! ni mharibifu sana, na hana huruma na mtu. Ndiyo maana hayo mavimbunga yamepewa majina ya wanawake kuonesha kwamba sasa nature imeghafilika, haina huruma na chochote na yeyote kama vile mwanamke akikasirika, moyo wake wa asili ya upendo hugeuka kuwa shubiri.
   
 8. Tonny

  Tonny JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2011
  Joined: Sep 13, 2010
  Messages: 217
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa sababu ni man made
   
 9. enhe

  enhe JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 80
  Mfano Katrina ilikuwepo tangu zamani maana nakumbuka nikiwa mdogo"kulikuwa na wimbo.. Mvua njoo katarina usije"!!!
   
 10. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  babuyao hapo umeua kabisa, hii kali, wanasema mnaomiliki bastola ndani mkeo asijue manake siku akikasirika atakushuti kabisa hawajui kukontrol hasira zao na anatamani afanye kitu kikubwa kumaliza hasira yake hasa pale anapokuwa hajatoa machozi.
   
 11. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Yap, Untouchables, Attitudes and swingmoods! :A S 109:
   
 12. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Oops i forgot Bitching! LOL!!
   
 13. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Hurricane George ilipita miaka ya late 90s
   
 14. 124 Ali

  124 Ali JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 5,703
  Likes Received: 2,383
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  what a memory matey!
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,201
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
 16. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  eeeeh....kumbe ndio ilikuwa ina maana hiyo.....nilikuwa najiuliza sana....huyo Katarina usije....ilikuwa inakujaje kujaje.....
   
 17. M

  Masuke JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  we umeambiwa kuanzia miaka ya 1950, kipindi hicho ulikuwa mkubwa au mdogo au ulikuwa hujazaliwa kabisa?
   
 18. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa Lokissa! Maana hata hiyo nature huitwa "mother nature" siyo "father nature". Kwa hiyo nature inapoghafilika katika sura ya kimbunga lazima iitwe kwa jina la kike (femminine) kuonesha kwamba sasa mother nature kacharuka, na hana huruma na yeyote. Kumbe aitwa katrina, elninyo, irene, nk,
   
 19. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,078
  Likes Received: 7,301
  Trophy Points: 280
  Nimeukumbuka wimbo wa "No Woman, No Cry" by Bob Marley.
  Tafsiri yangu rahisi tu juu ya huu wimbo kwa kufuatisha neno kwa neno ni kua asingekuwepo mwanamke kusingekuwepo na kilio.
  Wanawake wamekua ni chanzo cha vilio vingi sana katika maisha vinavyotokana na ujambazi, umaskini, wizi, uchonganishi, vifo, n.k.
  Sasa kwakua vimbunga vingi vikubwa huja na majanga mbalimbali ikiwemo vifo, ni sawa kupewa majina ya kike.
   
 20. mtaratibuuuuuu

  mtaratibuuuuuu Member

  #20
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haki ya nani lool mmmmmh,kazi ipo wadada
   
Loading...