Jinsi unaweza kukabiliana na changamoto za kazi baada ya kuhitimu

TTCC_TECNO

Member
Oct 23, 2023
22
10
Safari baada ya chuo kwa wahitimu inaweza kuwa na furaha na changamoto kwa pamoja. Unapojitosa katika ulimwengu wa kitaaluma, moja ya changamoto kubwa mtaani kwa wahitimu ni kazi hapa kuna vidokezo muhimu vya kukusaidia kufanya mabadiliko na kujenga mustakabali wa mafanikio.

Maisha baada ya chuo ni jambo la kufikiria kwa umakini, hivyo mojawapo ya njia muhimu za kusaidia ni kuhakikisha unajifunza jinsi ya kutengeneza Wasifu wa Kazi (CV) kitaalamu kwa kutumia templeti za mtandaoni na kutazama mafunzo kupitia video kwenye website mbalimbali kama vile https://www.resume-now.com/, Free CV Maker: Build Your Professional CV Online, https://www.indeed.com/ hizi zinaweza kutoa msaada mkubwa, njia nyingine muhimu ni (NETWORKING), hii inaweza kufanyika pia kwa kutumia website mbalimbali kwa kujisajili, kupakia CV yako na kuunganishwa na wataalamu.

Hapa kuna tovuti kadhaa zitakazokusaidia na website zilizoowekwa kuongoza moja kwa moja: Mabumbe Zoom Tanzania - ZoomTanzania Jobs, BrighterMonday Find The Right Job with BrighterMonday, Myjobo.com Tanzania Jobs List Modern – My Job, NaukriHub Tanzania https://www.naukri.com/jobs-in/, Mabumbe Jobs, Kwenye website hizi za kazi, unaweza kujiandikisha, kutengeneza wasifu wako, kupakia CV yako, kutafuta kazi, na kutuma maombi.

Hata hivyo, tovuti kama LinkedIn LinkedIn Tanzania: Log In or Sign Up ni mtandao wa kimataifa, unakusaidia si tu kwa maombi ya kazi bali pia kuunganishwa na wataalamu mbalimbali. Kwa ajili ya mafunzo ya haraka katika taasisi za serikali, ni vyema kutumia website ya TAESA TaESA | Job Portal.

Unapoelekea katika awamu baada ya chuo, kumbuka kwamba kila uzoefu unachangia katika maendeleo yako binafsi na kitaalamu. Kwa mtazamo wa kujituma na ahadi ya kuboresha kila mara, utakuwa na vifaa vyema vya kufanikiwa katika ulimwengu wenye changamoto zaidi baada ya kuhitimu.
 
Wamesema kazi hazipo na zikitokea tu wanadai wenye connection ndio wanazipata. Sasa tujifunze kuanika CV Ili iwaje.
 
Wamesema kazi hazipo na zikitokea tu wanadai wenye connection ndio wanazipata. Sasa tujifunze kuanika CV Ili iwaje.
asante sana tutajitaidi pia kutoa darasa juu ya swala la kujiajili na namna ya kupata vyanzo vya kuanza biashara karibu
 
Back
Top Bottom