Jinsi unavyoibiwa ukipima shamba kwa hatua

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,657
20,940
Kwa wastani hatua ya mtu mzima ina urefu wa futi 2.5. sawa na 75cm au 0.75m. Sasa ukipimiwa upana wa hatua 70 na urefu wa hatua 70 utakuwa na eneo lenye urefu wa 70x0.75 = 52.5m. Upana pia utakuwa 52.5m.

Ukitafuta eneo ambalo ni urefu x upana =52.5x52.5= 2756.25m square. Hapo utaambiwa ni ekari moja wakati ekari moja ina mita square 4,000. Unakuwa umepunjika 4000-2756= 1244m square.

Ukinunua ekari kumi kwa hatua utapunjika 12,440 m square. Hizo ni sawa na ekari 12,440/4000= 3.

Kwa hiyo ukinunua ekari 10 kwa hatua utapunjwa 3 na kubakiwa na 7. Ukinunua 100 utapunjwa 30.
 
Sitaki kuamini kuwa umeicopy sehemu km ilivo na hujaifanyia marekebisho au km umeandika mwenyewe basi utakuwa umeandika uku upo kwenye daladala hivo ukapoteza umakini, nazani kuna marekebisho yanahitajika kwenye hizo hesabu hapo. Maoni tu
 
wapi pamekosewa?
 
kwa wastani hatua ya mtu mzima ina urefu wa futu 2.5. sawa na 75cm au 0.75m. sasa ukipimiwa upana wa hatua 70 na urefu wa hatua 70 utakuwa na eneo lenye urefu wa 70x0.75 = 52.5m. upana pia utakuwa 52.5m.
ukitafuta eneo ambalo ni urefu x upana =52.5x52.5= 2756.25m square. hapo utaambiwa ni ekari moja wakati ekari moja ina mita square 4,000. unakuwa umepunjika 4000-2756= 1244m square.

ukinunua ekari kumi kwa hatua utapunjika 12,440 m square. hizo ni sawa na ekari 12,440/4000= 3.
kwa hiyo ukinunua ekari 10 kwa hatua utapunjwa 3 na kubakiwa na 7. ukinunua 100 utapunjwa 30.

Mimi ninapolimiwa na trekta au kununua shamba huwa nachukua futi kamba ya mita 100, na nikiwa shamba wote tukiwepo nachukua kamba naipima mita 70 au 140 kulingana na ukubwa wa shamba. So tunapima kwa mita urefu na upana hakuna habari ya kuhesabu hatua na kuibiana.
 
70m * 70m = 49,000 m2 ; mita za mraba 4,047 umezipataje mkuu?
huwa unawaibia. hizo 4,900 ni yard ambazo kisahihi ni 4,840 na yard ni fupi kuliko mita. yard 1 ni sawa na mita 0.91. kipimo cha ekari duniani kote ni 4,047 au tukirahisisha tunasema 4,000. hapa inaweza kuwa 80x50, 40x100 nk. pia unapima kwa kutumia formula za hesabu za kutafuta eneo kulingana na umbo la shamba. ila mkuu umeibia sana watu.
 
Metric units ni metres na imperial units ni yard kama sijakosea, sasa hapa tuchague mfumo mmoja ili mjadala uwe mtamu na wa kueleweka.
nafikiri bongo tumezoea mita. watu wengi hasa wa kitunguu hulalamika kuwa mavuno kwa hekari siyo kama walivyoambia lakini kumbe walilima 70% ya eka na si ekari kamili. vipi miti mkuu, hupanda mingapi kwa ekari?
 
Mimi ninapolimiwa na trekta au kununua shamba huwa nachukua futi kamba ya mita 100, na nikiwa shamba wote tukiwepo nachukua kamba naipima mita 70 au 140 kulingana na ukubwa wa shamba. So tunapima kwa mita urefu na upana hakuna habari ya kuhesabu hatua na kuibiana.
Mkuu kama umezoea kufanya hivyo basi huwa unajiibia mwenyewe teh teh teh!
Hili somo la vipimo naona wengi wenu limewapita kando.
 
nafikiri bongo tumezoea mita. watu wengi hasa wa kitunguu hulalamika kuwa mavuno kwa hekari siyo kama walivyoambia lakini kumbe walilima 70% ya eka na si ekari kamili. vipi miti mkuu, hupanda mingapi kwa ekari?
nafikiri bongo tumezoea mita. watu wengi hasa wa kitunguu hulalamika kuwa mavuno kwa hekari siyo kama walivyoambia lakini kumbe walilima 70% ya eka na si ekari kamili. vipi miti mkuu, hupanda mingapi kwa ekari?
Mkuu upandaji wa miti unatofautiana kutokana na aina ya miti unayopanda.
Mathalani ikiwa kama unapanda miembe au minazi. Unashauriwa uipande kwa upishano(interval) ya walau mita8 mstari na shina. Kwa hesabu za haraka kwenye ekari moja ni 4000/(8*8)=

Vivyo hivyo kwa mitiki na syprus mimi hupishanisha 2.5metres kwa ekari moja itakuwa 4000/(2.5*2.5)=miche640 baadae utaipunguzia kadri inavyokuwa hadi hatua ya mwisho ibaki miti100-320/acre.

Tumieni vipimo, enzi za kuchana msamba mmh
 
Mkuu Red Giant umenikumbusha vituko vya mama mmoja anaitwa MamaShomii, yeye siku ya kwenda kuwapangia kazi vibarua wake huwa "havai kitu ndani" ili imrahisishie kupiga hatua ndefu zaidi pinda anapo pima plots kwa kila mtu!! Basi wafanyakazi huwa wanamgwaya sana the way anavyochana msamba!!
 
Mkuu kama umezoea kufanya hivyo basi huwa unajiibia mwenyewe teh teh teh!
Hili somo la vipimo naona wengi wenu limewapita kando.

Dah kama kutumia futi kamba VS kuhesabu kwa hatua za miguu naibiwa mkuu niko tayari kuelimishwa kwani nashughulika sana na mashamba so utakuwa umeniokoa...
 
Yaani bwashe uliyeleta mada naona kila unavyokoment unazidi kunipoteza. Mimi Nina futi kamba....nikinunua shamba la 70*70m kwa hesabu za haraka nina 4900m2. Hizo 4000 za yard unazileta za Nini hapa bongo???? Nieleweshe
 
kifupi ekari moja ni 4000m2 hizo 4900 ni kama unatumia yard.
 
Back
Top Bottom