Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,502
- 15,239
Habari JF members
Nimeona leo nielezee tabia ya kukurupuka ilivyonipa hasara mara kadhaa. Nimejifanyia tathmini nkagundua huwa nikitaka kufanya jambo lolote huwa napenda nilifanikishe kwa haraka sana ili niruhusu akili iweze ku focus na vitu vingine. Lakini tabia hii imenigharimu sana nakuepelekea kupata hasara ambazo ningeweza kuzizuia.
Mwaka 2022 na 2023 hii miaka nlinunua plots kadhaa za viwanja kutoka kwenye haya makampuni ambayo yanafanya promotion sana siku hizi mitandaoni, kununua haikua shida ila kwavile sikutuliza akili nkajikuta nimenunua viwanja haraka haraka bila kufanya hata research kidogo ila niweze kufanya comparison ya bei, hapa kwa haraka haraka 10m nkawa nimeipoteza ambayo ningetuliza akili nsingepigwa.
Kwenye kufatilia hati miliki hapa napo nimepoteza hela nyingi sana lakini sikuwa na namna.
Mwaka 2023 kipindi nafatilia passport ya kusafiria, hapa nlijikuta nimetumia karibu 750k sababu ya tabia hii hii ya kufanya vitu haraka haraka, kilichotokea hapa ni kwamba cheti changu cha kuzaliwa kilikua na makosa tarehe ya kuzaliwa, sasa kule uhamiaji wakaniuliza kama naweza kutumia tarehe ile ile ya makosa nkakubali bila hata kufikiria athari zake passport ikatoka, baadaye kufatilia nkashauriwa nitengeze cheti kingine cha kuzaliwa nirekebishe information zangu ziwe sahihi ntengeneze passport nyingine.
Manunuzi yangu ya vitu vingi, hasa vifaa vya electronics nimepoteza sana hela kwa tabia hii hii ya kufanya mambo haraka haraka.
Kuanzia sasa kwenda mbele nimeshaji-commit ntatuliza akili kwa kila kitu nnachotaka kufanya kuepusha hasara zinazoweza kuzuilika.
Karibuni na nyie mtoe uzoefu wenu