Jinsi Tundu Lissu Alivyojikaanga Kwa "Mafuta ya Taaluma Yake!!"

Wakuu,
Haina shaka kwamba Hotuba ya Tundu Lissu imevuta hisia za washabiki wengi wa "Serikali 3/Nchi 3!" Pia nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa huyo kwa kuwasilisha maoni ya wachache na kuchambua Sheria akienda sambamba na historia ya Muungano wetu tangu kuundwa kwake mpaka leo.
Mwanasheria huyo nguli, kama baadhi wanavyomwita ameenda mbali sana, bila kuuma maneno akidai kwamba Muungano wetu wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar hauna uhalali wowote wa kisheria kwa kuwa haukuridhiwa na Baraza la Wawakilishi, hata kama uliridhiwa na Bunge la Tanganyika tu!

Amedai pia kwamba kwa sasa tufute Sikukuu ya Muungano wetu na kuanzisha
"Siku ya Shirikisho!"Kwa hoja hizo za Lissu mimi sina ubavu wa kuzipinga kwa kuwa ametaja na vifungu vya kisheria vya wakati huo, tukubali tu kwamba Muungano HAUNA UHALALI WOWOTE WA KISHERIA!

Hata hivyo, Tundu Lissu alifikiri kwamba hoja hiyo inamu-implicate tu Nyerere ambaye amemtaja mara nyingi kwamba mambo mengi ameyafanya kwa AMRI YA RAIS. Mambo hayo ni kamba vile:
1. Jina la Nchi,
2. Kuiua Tanganyika,
3. Nembo ya Taifa, nk.

Kama Muungano hauna uhalali wowote maana yake nini?

1. Ni kwamba Tundu Lissu alifanya makosa kugombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano "BATILI," kwa hiyo Ubunge wa Lissu mpaka sasa ni "BATILI!"
2. Kwamba, hata mchakato huu wa kuandika Katiba Mpya ni "BATILI" kwa kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imetungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano" BATILI,"
3. Kwamba, Tundu Lissu amechangia kutunga Sheria "BATILI" za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa Bunge nalo ni "BATILI,"
4. Kwamba CHADEMA nacho ni chama "BATILI" kwa kuwa kimeundwa kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa ambayo imetungwa na Bunge "BATILI" la Muungano,
5. Kwamba, shughuli zote za kisiasa za Tundu Lissu hazina uhalali wowote wa Kisheria kwa kuwa zimefanywa kwa kufuata Sheria za Muungano "BATILI,"
6. Kama Lissu ana vyeti vya Shule za Tanzania navyo ni "BATILI" kwa kuwa vimetolewa na Serikali "BATILI,"
7. Kama Tundu Lissu amezaliwa baada ya Muungano na kupewa Cheti cha Kuzaliwa ahesabu kuwa ni "BATILI" mpaka sasa,
8. Kesi zote alizoshinda Tundu Lissu mahakamani ajue kwamba ni "UBATILI" mtupu maana" MUUNGANO HUU NI BATILI," kwa hiyo hata mahakama za Muungano ni "BATILI,"
9. Kama Tundu Lissu ameoa baada ya Muungano ajue kuwa ameumia, ni ndoa "BATILI" hiyo!!!
10..................

Hongera sana Tundu Lissu kwa Hotuba Murua...............Ila usiendelee kuwepo kwenye BUNGE hilo "BATILI" kwa kuwa limeundwa na Sheria "BATILI!!!" Tafadhali sana, I am not joking, this time around!

.....Panya kanywa mchuzi, Paka kala panya, kumbe paka kanywa mchuzi indirect.......?
 
Swali gumu hawezi kujibu. Kama atasema tuendelee hivyo hivyo basi mirembe itakuwa inamhusu!!

Unamaanisha wale wanaoendelea na Bunge Maalum huku wakidai kuwa Sheria zilizounda Bunge hilo ni za Muungano "Haramu?"
 
Wakuu,
Haina shaka kwamba Hotuba ya Tundu Lissu imevuta hisia za washabiki wengi wa "Serikali 3/Nchi 3!" Pia nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa huyo kwa kuwasilisha maoni ya wachache na kuchambua Sheria akienda sambamba na historia ya Muungano wetu tangu kuundwa kwake mpaka leo.
Mwanasheria huyo nguli, kama baadhi wanavyomwita ameenda mbali sana, bila kuuma maneno akidai kwamba Muungano wetu wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar hauna uhalali wowote wa kisheria kwa kuwa haukuridhiwa na Baraza la Wawakilishi, hata kama uliridhiwa na Bunge la Tanganyika tu!

Amedai pia kwamba kwa sasa tufute Sikukuu ya Muungano wetu na kuanzisha
"Siku ya Shirikisho!"Kwa hoja hizo za Lissu mimi sina ubavu wa kuzipinga kwa kuwa ametaja na vifungu vya kisheria vya wakati huo, tukubali tu kwamba Muungano HAUNA UHALALI WOWOTE WA KISHERIA!

Hata hivyo, Tundu Lissu alifikiri kwamba hoja hiyo inamu-implicate tu Nyerere ambaye amemtaja mara nyingi kwamba mambo mengi ameyafanya kwa AMRI YA RAIS. Mambo hayo ni kamba vile:
1. Jina la Nchi,
2. Kuiua Tanganyika,
3. Nembo ya Taifa, nk.

Kama Muungano hauna uhalali wowote maana yake nini?

1. Ni kwamba Tundu Lissu alifanya makosa kugombea ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano "BATILI," kwa hiyo Ubunge wa Lissu mpaka sasa ni "BATILI!"
2. Kwamba, hata mchakato huu wa kuandika Katiba Mpya ni "BATILI" kwa kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imetungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano" BATILI,"
3. Kwamba, Tundu Lissu amechangia kutunga Sheria "BATILI" za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa Bunge nalo ni "BATILI,"
4. Kwamba CHADEMA nacho ni chama "BATILI" kwa kuwa kimeundwa kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa ambayo imetungwa na Bunge "BATILI" la Muungano,
5. Kwamba, shughuli zote za kisiasa za Tundu Lissu hazina uhalali wowote wa Kisheria kwa kuwa zimefanywa kwa kufuata Sheria za Muungano "BATILI,"
6. Kama Lissu ana vyeti vya Shule za Tanzania navyo ni "BATILI" kwa kuwa vimetolewa na Serikali "BATILI,"
7. Kama Tundu Lissu amezaliwa baada ya Muungano na kupewa Cheti cha Kuzaliwa ahesabu kuwa ni "BATILI" mpaka sasa,
8. Kesi zote alizoshinda Tundu Lissu mahakamani ajue kwamba ni "UBATILI" mtupu maana" MUUNGANO HUU NI BATILI," kwa hiyo hata mahakama za Muungano ni "BATILI,"
9. Kama Tundu Lissu ameoa baada ya Muungano ajue kuwa ameumia, ni ndoa "BATILI" hiyo!!!
10..................

Hongera sana Tundu Lissu kwa Hotuba Murua...............Ila usiendelee kuwepo kwenye BUNGE hilo "BATILI" kwa kuwa limeundwa na Sheria "BATILI!!!" Tafadhali sana, I am not joking, this time around!

mkuu haujaamua kuwa serious na mimi siwezi kumemorise vitu visivyo seriois....OK tukubaliane, kila kitu cha nchi hii ni batili, kwa iyo? ok ubunge wa lissu ni batili so what?

Kama kila kitu ni batili then ndo tunapaswa kuanza upya.
Nani aliyekuambia sheria ya uchaguzi imeanza baada ya kuwa na muungano?
Nani amekuambia elimu ta taifa ili imeanza baada ya muungano batili?
Nani aliyekuambia wanasheria na maadvocate wameanza kuhudhuria mahakamni baada ya muungano?
Kwa kukusaidia, tuelewane kuwa muungano sio nchi, muungano ni wa kidola yaani state, na zaidi a State is not a country.

Lissu anaweza kuwa na maoni batili, elimu batili, na kazi batili ila ilo halibatilishi uwepo wa nchi ya Tanganyika.
Mnapaswa kumjibu lissu, je Zanzibar iliungana na nchi ipi? kisha mjibu kwa hoja si vihoja kama ivi mnavyoleta!
 
Unaonekana una uwezo mdogo sana wa kuelewa mambo na kujenga hoja. Unaacha hoja za msingi na kurukia za kijinga.
Jenga hoja kutokana na zilizopo. kwa hali hii wajinga ni wengi sana nchi hii.Mnafaidika nini na kuunga mkono hoja za kijinga kama zinavyotolewa na wajumbe walio wengi bungeni?

Sasa wewe hapo umejenga hoja au umetukana? Kazi ipo kweli kwa sisi mashabiki.
 
mkuu haujaamua kuwa serious na mimi siwezi kumemorise vitu visivyo seriois....OK tukubaliane, kila kitu cha nchi hii ni batili, kwa iyo? ok ubunge wa lissu ni batili so what?

Kama kila kitu ni batili then ndo tunapaswa kuanza upya.
Nani aliyekuambia sheria ya uchaguzi imeanza baada ya kuwa na muungano?
Nani amekuambia elimu ta taifa ili imeanza baada ya muungano batili?
Nani aliyekuambia wanasheria na maadvocate wameanza kuhudhuria mahakamni baada ya muungano?
Kwa kukusaidia, tuelewane kuwa muungano sio nchi, muungano ni wa kidola yaani state, na zaidi a State is not a country.

Lissu anaweza kuwa na maoni batili, elimu batili, na kazi batili ila ilo halibatilishi uwepo wa nchi ya Tanganyika.
Mnapaswa kumjibu lissu, je Zanzibar iliungana na nchi ipi? kisha mjibu kwa hoja si vihoja kama ivi mnavyoleta!

Sheria ya Vyama vya Siasa ni ya mwaka 1992, Sheria ya Elimu ni ya Mwaka 1978, xote ni baada ya Muungano! Sheria ya Vyuo Vikuu ni ya Mwaka 2005 kama sikosei, hiyo nayo ni ya baada ya Muungano!
Kama unataka tuanze upya sijui unamaanisha tuanzeje maana Sheria iliyoanzisha Bunge Maalum la Katiba nayo ni BATILI maana imetungwa na Bunge la Muungano BATILI!
Yaani kwa kifupi Lissu angejua athari za kauli yake mapema asingefungua mdomo wake aisee!
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa endapo mume na mke hawajafunga ndoa halali basi chochote watakachofanya ni batili? Kwa maana hiyo hata wakizaa watoto watakuwa batili, wakijenga nyumba itakuwa batili, wakinunua shamba litakuwa batili, wakianzisha kampuni nayo itakuwa batili? Acha pumba bhanaasa!
 
Waheshimiwa..mchungaji aliye bora ni yule mwenye kukaa na wakosaji na kuwasafisha na kamwe sio yule anayetazama walio wasafi tu na kunyooshea vidole walio wachafu...mistakes have alredy done....na kama unafuatitia.upuuzi wote huo ulifanywa hata kabla ya uzao wa Tundu lisu...sasa he need support kurekebisha haya na sio kunyooshewa vidole...atawezaje kurekebisha uchafu ulio ndani ya usafi pasipo kushika vyote uchafu na usafi?tunatumia hizihizo mamlaka batili na kuzikomboa kua halali na kuondokana na ubatili
 
Alitazama na kusikiliza bunge la jioni hii.
Wachache wamemtambu nani Ngariba na nani Kungwi. Ngoma za watoto hazikeshi, usingizi lazima.
Hati ni hiyo, tuleteeni jipya.
Kodi yetu rudisheni.
Watoto wadogo wabishi kama ......
Kisa chuo Kikuu
 
Back
Top Bottom