Jinsi tunavyoibiwa petrol station

Kuna vituo wako vizuri saana. Kuna Total Mlimani City na PUMA mandela road. Vingine huwa siwaelewi.
Vituo hivyo ulivyotaja hata kwa muonekano tu,unajua kuna biashara halali,hawa wengine nahisi mabosi wanajua,pengine wanagawana %
 
Ha ha ha,umenena vema,aibu itatufanya tushindwe kufika malengo
 
Hao ni big bon tuu kwa jinsi ulivyoelezea
 

Uko sahihi kabisa mkuu tena kuna sheli pale mwanamboka ukiwaambia waanze na zero hawakubali kabisa tena ukifka wanakutolea pampu ile wanayoipenda madereva bodaboda
 
Asante mkuu
 
Na wewe kwanini usishuke kuhakikisha zimesoma lita 5
Tatizo siyo meter reading,tatizo ni ujazo unaotoka kwenye kila mililitre au lita ndiyo inakuwa imepungua.
Anaejaza fulltank katika pump inayoiba basi anapoteza zaidi.
 
Kwa wakala wa VIPIMO ni muhimu kuzikagua hizi pump kila kituo mara kwa mara.
 
Reactions: cdc
Vitajeni vituo kwa majina tusaidiane madereva
Mimi kile cha Sinza Kijiweni kilishaga nitumbukia nyongo kuna Siku walinitenda
Mambo yote Siku hizi ni Gbp
Hapo nilienda,kuna mama mmoja bonge ana mkorogo hivi,huyo ukigeuka tu anaunganisha na ile hesabu isiyofutwa aliyotangulia kupewa mwenzio,hasa akiwa wa pikipiki.
 
Inatakiwa mipira ambayo ni transparent. Wese likipita tu unaona
 
Kumbe ndio maana huwa nahamishwa pump..., aisee nimeshtuka, kuanzia leo naenda pump ambayo hawataki.., wakinilazimisha nashuka natoa dumu la lita 5 tuone sasa
 
Kuibiwa tutaibiwa tuu cha msingi ni kuangalia Pump za kisasa hizi kidogo zipo ok na kitu cha pili angalia sehemu ambayo dala dala au gari za abiria kwa wingi zikijaza mafuta katika garage yeyote jua hapo mafuta kwa kiasi fulani wanatoa kwa usahihi maana hawa wa hiace wana hesabu sana mafuta yao kwa kila Route wanajua watatumia kiasi gani tofauti na private car..
 
Inatakiwa mipira ambayo ni transparent. Wese likipita tu unaona
Hiyo si suluhisho sana,vipimo wasimame katika ukaguzi wa mara kwa mara,katika mpira itayaona yanapita ila ujazo kwa lita ukipungua hautajua kama unaibiwa.
 
bado hujaeleza namna tunavyoibiwa. umeeleza hisia zako. nilidhani umegundua namna wanavyoiba.kumbe hamna kitu.
Acha ukilaza wewe, hayo mazingira yanaonyesha dhahiri kwamba kuna wizi, kugundua wizi kwa kuthibitisha ni kazi ya wakala wa vipimo, siyo kazi yake. Wewe utakuwa mfanya kazi wa filling station sio bure
 
Mimi nawaambiaga tu weka full huku nikihakikisha inaanza kusoma kwenye zero baada ya hapo nasinzia nakuja kuamshwa wameshajaza...nafuta kilometers kuanzia zero zikifika 390km naenda tena...ole wao isifike 390km wananijua maana gauge ilishakufa
 
Acha ukilaza wewe, hayo mazingira yanaonyesha dhahiri kwamba kuna wizi, kugundua wizi kwa kuthibitisha ni kazi ya wakala wa vipimo, siyo kazi yake. Wewe utakuwa mfanya kazi wa filling station sio bure
Uko sahihi sana mkuu
 
Nimejifunza kitu japo wa mkoa nitakua nanunua kwenye dumu naweka mwenyewe umbwa kabisa hao in manji's voice
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…