Nakumbuka nilikuwa Zanzibar 2011 nikiwa kwa shughuli zangu nikapigiwa simu na mtu aliyejifanya yuko kigoma na amepewa namba yangu na rafiki yangu aliye uingereza, baada ya kumuuliza kama kuna mtu mwaninifu na anaeweza kuwasaidia kupata dawa za kuhifadhia chakula, cha wakimbizi huko kigoma.! Kifupi alidai yeye anafanya kazi hapo na kuna dawa inahitajika sana ya kuhifadhi hicho chakula imeadimika huko isipokuwa inapatikana Znzbr sbbu inaingizwa kutoka commoro kuhusu bei. Walidai wao walikuwa wakinunua tsh 1.5 milion kwa chupa kwa mletaji wao. Lakini kawapandishia sana bei mpaka 2.5 million.. Hivyo Hugo mzungu ambaye ndio mkuu anatafuta mletaji Mpya Wa bei nafuu. Nikapewa namba ya Dr. Anayejiita Mohammed. Yupo mahonda kilipokuwa kiwanda cha sukari.. Kuwa ndie alikuwa na huo mzigo yeye ni mtaalam Wa hizo dawa . niwasiliane nae kama anazo na bei yake kisha wakanisihi. Niwajulishe.. Huyu Mohammed akaniambia mzigo anao na bei ni tsh 900000. Kwa chupa. Na kama ntachukua mzigo mkubwa atafanya. 850000. Kwa kila chupa, akaniuliza je unahitajika kiasi gani? Nikamwambia asubiri niwaulize wanaohitaji.. Wakaniambia chupa 1000. Ila kama bei ndio hiyo nisubiri wanipe namba ya huyo mzungu yupo zamani kepinsik hotel kiwengwa Znzbr au wampe namba yangu anipigie.. Ila bei nimwambie. Na ning'ang"anie pale pale Kwenye 1.5 kwa chupa. Baada ya dakika kama kumi hivi nikapokea simu ya huyo anayejiita mzungu.. Kwa jinsi alivyokuwa akiongea sikua na shaka ni mmarekani. Au mwingereza. Akaniuliza kuhusu hizo dawa na kama Nina uhakika ndizo na kama naweza kuwa mletaji wao Mpya. Akaniuliza bei kama kawa nikamtajia ile niloyoambiwa.. Akaniuliza ningependa zilipwe kwa dollar au tsh nikamwambia vyovyote akajibu wana dollar. Nisubiri wachange au kama Niko radhi nimpelekee sampuli aende akaione kisha ikibidi niondoke nae tukauchukue mzigo tumalize biashara.. Wakati huo huyu Wa kigoma muda wote anapiga simu kuulizia kila hatua akisisitiza nisimsahau kwa chochote. Ngoma ilikuwa kupata hiyo sampuli ya dawa bwana Mohammed akasema yuko busy hawezi toka kwenda onana na Hugo mzungu.. Ila kama nataka biashara nichukue sample nimpelekee. Lakini hiyo sample hatoi bure lazima ilipiwe. Ili nikipotea pesa yake ibaki. Na wakati huo yule mzungu ananipigia simu kuwa niokoe muda maadam mzigo umepatikana angependa aondoke mchana huohuo kurudi kazini kwake hivyo nifanye haraka kupeleka hiyo sample.. !! Nikawa sins budi kulipa hiyo pesa tsh 850000. Badala ya 900000. Nikatumiwa akaleta hiyo chupa nikiambiwa Huyo Dr yuko busy kiasi. Nikampa pesa Hugo kijana na kuanza mbio za kwenda huko hotel.nikiwa njiani akanipigia mwingine kutoka eti Kenya nipeleke sample mbili nikakataa. Nilipofika getini. Nikauliza kuhusu Hugo mzungu Mr Thompson wakabaki wananishangaa nikaulizwa room namba sikuwa na jibu nikaambiwa nimpigie simu.. Hapo ndio nikipogundua ulikuwa mchezo namba zote zikawa hazipatikani. Siyo ya kigoma, ya Dr mohammed, yule mkenya wala kijana aliyeniletea huo mzigo...!!! Nilipopeleka kwa mkemia mkuu wa serikali znbr nikaambiwa nimepigwa. Costic food product. Sikumbuki vema jina la hiyo dawa. Kama ni hilo hapo juu ama laa.!