Super human
JF-Expert Member
- Feb 26, 2015
- 1,147
- 752
dah mi niliuziwa sabun kipande cha sh 100 elf 20 mwaka 2006
Hawa jamaa viberiti vitatu ni ujanja tu, hawana dawa wala hirizi, isipokuwa wako makini na kazi yao, viberiti viwili havina njiti na kimoja kina njiti zilizopunguzwa urefu, ukifungua kwa upande mmoja unaziona, ila ukifungua kwa upande mwingine hauzioni, kwa sababu kimewekwa kaboksi katikati kutenganisha upande wenye njiti na upande usio na njiti, sasa anakuwa mjanja mchezeshaji, ukiweka pesa tu azingua anakufungulia upande mwingine wa kiberiti kilekile unakuta njiti hakuna, unakuwa umeliwa, halafu pale kundi kubwa wanakuwa ni wao tu, kwa hiyo kuchomoka inakuwa ngumu.Nilikuwa form two kipindi flani nkapewa hela ya kwenda kununua viatu vya shule nkafika kwa jamaa wa kiberiti wakazimaliza,sijawahi kucheza tena huo ujinga
Daahhh nikikumbuka siku niliyotapeliwa huwa najiona mpumbavu kweli kweli.Ilikuwa maeneo ya mmanzi mmoja style ya utapeli huu ni ile ya kuopoa vikoponi kwenye kijimfuko ambavyo huwa na number ya bidhaa walizozipanga kama tv,deki,pasi,radio,jiko na vikorombwezo vingine kibao basi bwana nikatia mkono ndani nikaibuka na kuponi yenye number za music system wakadai thamani yake ni kama 1.7 ila sasa mimi itanipasa kutoa 150000K bahati nzuri sikuwa na hiyo hela nikikuwa na usd 30 na 10000k nikawapatia yote maana nilikuwa na njaa ya pesa kinyama pale pale nikaanza kuipigia hesabu ya matumizi ile 1.7ml ikaisha hata kabla sijajua kama nitaipata ama la,basi wakaendelea kunishawishi niongeze hela ifike mia hamsini bila mafanikio.Pembeni ya ile meza alikuwa amesimama kijana mmoja hivi akawa ananipa mahope kuwa nimeshawakamata hawana ujanja pesa nimepata basi mimi huku mapigo ya moyo yanaenda kasi kama saa ya automatic maana nikiangalia kikuponi number ndo ile ile nikajua mwanaume nimeula kumbe nimeliwa daahh kumbe yule jamaa aliyekuwa anani pump ni member pale,basi nikawakabizi ile $30 na 10000k ile wanafua vile vikupon nakuta number ni tofauti kabisaaaaaaaa pale ndo nikagutuka kuwa nimetapeliwa wala sikuuliza niliondoka maana ningeanzisha malumbano pale wangeweza pita watu wanaonifahamu wakaniona ikawa aibu mara mbili.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]Nakumbuka ilikuwa miaka ya tisini mwanzoni,brother wangu alitapeliwa mnazi mmoja pale. Siku hiyo asubuhi aliaga anaenda shule boarding iringa,akaondoka na baraka zote za wazazi,ghafla saa nne asubuhi asharudi home anahema kichizi,wazee wakamuuliza kulikoni hujaenda shule?akawakusanya wazazi chumbani wakajifungia mi nikawa nachungulia ,bro akatoa kidude flan hivi nikamsikia anasema dhahabu,aisee wazee wakaenda funga mageti yote nje,bro akawaambia alikutana na msukuma stand eti aliokota hiko kidude ila yeye hakitaki kimeandikwa GOLD FIRST CLASS FROM ..nimesahau jina la mgodi akaamua mpa nauli ya ke ya bus to iringa na poketi money yote. Aisee ile ishu iliwachanganya wazee wakajua utajiri huu. Milango imefungwa home hamna wa kutoka mpaka mimi wanani ignore,ikafika usiku wa saa nne wakatoka kwenda kwa mzee jirani yeye mtaalam wa madini hahaha,yule mzee akawasha stovu akayaiunguza yale mawaya dooh yakawa meupe na biashara ikaishia hapo.
Hata mimi navijua acha wapigwe si ujinga wao,usiharibu kabisa watu wanaishi kwa dili hizo!!kiberiti,sabuni,bahasha,mkanda na korokoro ninautaalamu navyo ila ninawasiwasi wa kuharibu biashara ya watu.mnanishaurije nimwage hapa?
Haaahaaa hawajakutoa na moshi?!Mi nishawahi temeshwa nywele na simu wakabeba hhahaaaaa mweee
Aisee umenifungua akili nilikuwa najiuliza huwa wanatumia ujanja gani hawa watu? Kumbe hiyo ndo trick yao.. Thank you mkuu.Hawa jamaa viberiti vitatu ni ujanja tu, hawana dawa wala hirizi, isipokuwa wako makini na kazi yao, viberiti viwili havina njiti na kimoja kina njiti zilizopunguzwa urefu, ukifungua kwa upande mmoja unaziona, ila ukifungua kwa upande mwingine hauzioni, kwa sababu kimewekwa kaboksi katikati kutenganisha upande wenye njiti na upande usio na njiti, sasa anakuwa mjanja mchezeshaji, ukiweka pesa tu azingua anakufungulia upande mwingine wa kiberiti kilekile unakuta njiti hakuna, unakuwa umeliwa, halafu pale kundi kubwa wanakuwa ni wao tu, kwa hiyo kuchomoka inakuwa ngumu.
Mwaga mkuu. Mwaga bila ajizi uokoe wadau.kiberiti,sabuni,bahasha,mkanda na korokoro ninautaalamu navyo ila ninawasiwasi wa kuharibu biashara ya watu.mnanishaurije nimwage hapa?
Mkuu hapo hakuna utahira! Utakapo kuja tapeliwa ndo utaelewa"wewe ni taira jinga kabisa unatapeliwa mara 3 same game unakuja kubwabwaja hapa tukusaidie nini sasa.
swissme
Umejuaje best!!! Alilamba kidole chake akasugua kwenye vumbi then akanisugua mkononi ukatoka moshi mwingiiiiiii huku anaongea makorokocho, hapo akili ikapaaa akanambia niende karibu na kanisa fulan eti nikifika niseme utukufu juu mbinguni na amani dunian ntaona Pete ya Bahati inashushwa! Daaah waliniweza wale jamaaa nikikumbuka nachekaa😀Haaahaaa hawajakutoa na moshi?!
Yaani ule moshi aliutengeneza mwezio ambaye tayari alishakwenda kanisani kuna namna alivyorudi alimpa huyo muombeaji bila wewe kujua,hakuna uganga wala nini ni ujanja tu.Umejuaje best!!! Alilamba kidole chake akasugua kwenye vumbi then akanisugua mkononi ukatoka moshi mwingiiiiiii huku anaongea makorokocho, hapo akili ikapaaa akanambia niende karibu na kanisa fulan eti nikifika niseme utukufu juu mbinguni na amani dunian ntaona Pete ya Bahati inashushwa! Daaah waliniweza wale jamaaa nikikumbuka nachekaa😀
Yaani ule moshi aliutengeneza mwezio ambaye tayari alishakwenda kanisani kuna namna alivyorudi alimpa huyo muombeaji bila wewe kujua,hakuna uganga wala nini ni ujanja tu.
Hiyo inakuwaje?Du wanapigwa Sana pale msimbazi Makoro pgo za cmu unauziwa sabuni.au unanunua kiatu kumbe ugali wa juzi huwa nacheka Sana..
Hahaaaa inakuwaje hapoYaani ule moshi aliutengeneza mwezio ambaye tayari alishakwenda kanisani kuna namna alivyorudi alimpa huyo muombeaji bila wewe kujua,hakuna uganga wala nini ni ujanja tu.