Jinsi nilivyowahi kutapeliwa, Wewe je?

Jinsi nilivyowahi kutapeliwa, Wewe je?

Kuna fal.a mmoja alikua na michezo ya kutuchanganyia hela bandia dukani kwetu kkoo....tukamnote tukamlia ganzi tu. Kuna siku tukamuwekea mtego akajaa....

Taratibu tukamuingiza chemba na vijana kadhaa alikula kipondo cha kushiba haja siku hiyo....lile duka letu mpaka kesho kutwa analiogopa kama ukimwi.

Mambo mengine polisi tunawachosha tu. Huku huku kitaa tunamalizana.
 
Nakumbuka ilikuwa miaka ya tisini mwanzoni,brother wangu alitapeliwa mnazi mmoja pale. Siku hiyo asubuhi aliaga anaenda shule boarding iringa,akaondoka na baraka zote za wazazi,ghafla saa nne asubuhi asharudi home anahema kichizi,wazee wakamuuliza kulikoni hujaenda shule?akawakusanya wazazi chumbani wakajifungia mi nikawa nachungulia ,bro akatoa kidude flan hivi nikamsikia anasema dhahabu,aisee wazee wakaenda funga mageti yote nje,bro akawaambia alikutana na msukuma stand eti aliokota hiko kidude ila yeye hakitaki kimeandikwa GOLD FIRST CLASS FROM ..nimesahau jina la mgodi akaamua mpa nauli ya ke ya bus to iringa na poketi money yote. Aisee ile ishu iliwachanganya wazee wakajua utajiri huu. Milango imefungwa home hamna wa kutoka mpaka mimi wanani ignore,ikafika usiku wa saa nne wakatoka kwenda kwa mzee jirani yeye mtaalam wa madini hahaha,yule mzee akawasha stovu akayaiunguza yale mawaya dooh yakawa meupe na biashara ikaishia hapo.
 
Utapeli upo wa aina nyingi.......watu weng wamesha pitia hayo ila kila m1 ana namna yake na inawezekana umetapeliwa kijinga.
Maisha yapo hivyo weka hapa tupate kuzijua mbinu zao.

1.Ilikuwa siku 1 nipo Tanga.... Eneo maarufu kama tangamano wakawepo wachezesha kamari.
Uoneshe kasha lenye kiberiti hapo anakuwa anavichanganya vyote.... Vipo vi3.... Uoneshe ki1 chenye njiti.
Mtu mzima nikawa nafuatilia kwa macho..... Nikawa nakiona.... Ile tu kiweka ela yangu... Ikawa nimekosea... Nikaliwa.

2 Wakaja wale wenye mkanda..... Nako kabla hujaweka ela unakuwa unapatia lkn ukisha weka tu ela... Inakula kwako....

3 Nikaenda dar... Nikaona mchezo ule wa vyombo vyiingi na mara friji... Jiko... Tv... Laptop...na vikoro koro viiiingi.
Wanakupa mfuko wa kadi... Then unazilipia.... Ili kama ukipata inayoendana na iliyopo kwenue kifaaa unakuwa umepatia. Xo unapewa fedha zenye thaman ya hiyo kitu.....
Mwanaume nikapiga hesabu hapo nina kadi 4... Hapo kuna ya frij.... Jiko... Na vingne... Nikapiga hesab pale ikaja kama 1.2mil....ha nikaona kiwewe niakaambiwa lipia ndo zifunguliwe zile kadi.... Huku nimezishika mimi.
Nilipolipia 40000 tu wakasoma sikuona cha namba wala nn zipkuwa zimeandikwa utajiju... Mwenye wivu.... Na mengine mengi na kwa hapo nimebakishiwa buk 2 tu.......aisee nilichoka yan.

NB hawa watu wanatumia nguvu gani? Kiini macho?
Mbona unaibiwa kizembe sana? Umetokea kijiji gani ndugu?
 
nilishaga wahi kulizwa kwa njia ya mitandao m-pesa.
jamaa mmoja alihack(mpaka leo sijajua aliwezaje) namba ya bosi wangu, kisha jamaa akanitumia ujumbe huu' NITUMIE 130,000/= KWENYE NAMBA HII 075.......(nishaisahau) simu yangu imeshiwa moto".
siku ile sikuwa na balance salio kwenye simu, na niliona uvivu kuweka ili nimuulize, na kwa vile haikuwa mara ya kwanza kupokea ujumbe kama huo kutoka kwa boss wangu nikatuma kweli. daaah nilikuja kugundua kuwa nimeibiwa baada ya yule jamaa(tapeli) anani text sms ya kuniomba nimtumie tena 120,000/= ndipo nikastuka kwa vile boss wangu ataombaje hela nyingine ilihali fedha ya mauzo hata yeye anaijua ilikuwa 140K. NILILIA SANA kwa vile ndio kwanza nilikuwa natoka kijijin na mshahara wenyewe ni 50,000. ndipo iliponibidi nifanye kazi miezi mitatu bila malipo SITASAHAU!!
Daaaah!! Pole sana mdogo angu!! Huyo boss kashindwa kukusamehe wkt anajua kabisa hukukusudia!
 
Utapeli upo wa aina nyingi.......watu weng wamesha pitia hayo ila kila m1 ana namna yake na inawezekana umetapeliwa kijinga.
Maisha yapo hivyo weka hapa tupate kuzijua mbinu zao.

1.Ilikuwa siku 1 nipo Tanga.... Eneo maarufu kama tangamano wakawepo wachezesha kamari.
Uoneshe kasha lenye kiberiti hapo anakuwa anavichanganya vyote.... Vipo vi3.... Uoneshe ki1 chenye njiti.
Mtu mzima nikawa nafuatilia kwa macho..... Nikawa nakiona.... Ile tu kiweka ela yangu... Ikawa nimekosea... Nikaliwa.

2 Wakaja wale wenye mkanda..... Nako kabla hujaweka ela unakuwa unapatia lkn ukisha weka tu ela... Inakula kwako....

3 Nikaenda dar... Nikaona mchezo ule wa vyombo vyiingi na mara friji... Jiko... Tv... Laptop...na vikoro koro viiiingi.
Wanakupa mfuko wa kadi... Then unazilipia.... Ili kama ukipata inayoendana na iliyopo kwenue kifaaa unakuwa umepatia. Xo unapewa fedha zenye thaman ya hiyo kitu.....
Mwanaume nikapiga hesabu hapo nina kadi 4... Hapo kuna ya frij.... Jiko... Na vingne... Nikapiga hesab pale ikaja kama 1.2mil....ha nikaona kiwewe niakaambiwa lipia ndo zifunguliwe zile kadi.... Huku nimezishika mimi.
Nilipolipia 40000 tu wakasoma sikuona cha namba wala nn zipkuwa zimeandikwa utajiju... Mwenye wivu.... Na mengine mengi na kwa hapo nimebakishiwa buk 2 tu.......aisee nilichoka yan.

NB hawa watu wanatumia nguvu gani? Kiini macho?
MCHAGA AIBIWI MARATATUU MUULIZE HUYO BABA KAMA KWELI KAZALIWA.MOSHI AMA WALE WAKUFIKIA
 
Namshukuru MUNGU sijawahi kutapeliwa hata siku moja Zaidi ya kuwaokoa watu wengine, nimeshaokoa watu Zaidi ya wane kwa utapeli wa Simu/dawa za kutunzia samaki/Matrekta n.k. Sijisifu ila namshukuru MUNGU tu huwa nachezwa na machale mwanzoni kabisa mwa gemu.... kiasi kwamba na mimi nimegeuka kuwa mtaalamu sasa hasa nikikutana na Traffic......

Sikiliza nilivyomtapeli Traffic, natoka Dar naenda Morogoro, mbele kidogo ya Chalinze kuna vibwana mdogo vinashinda pale na nguo zao nyeupe na Kitochi chao wanakua wamejificha infact wanakuvizia! Ghafla hawa hapa, nikasimama, wakanifuata wakaanza maelezo marefuuuuuu ila nikawasihi sana Sanaa kuwa kwa muda ule sikua na kitu na kwamba wanisamehe tu, wakakomaa kabisa, nikaona isiwe shida. Nikamwambia kuwa nauza simu kwahio kama atakubali nimapatie ile simu halafu yeye aniongeze pesa kidogo baada ya ku-deduct pesa yake ya Fine, Dogo akajaa, kuangalia kitu iTel kubwaaa, screen kubwa, hahahahahaaa. Akaitest inawaka safi kabisa nini, nikamwambia anipe mia themanini tu, akaanza kulialia paleee, tukashushana hadi hadi mia ishirini, ukikata fine yake 30 elfu inabaki 90 elfu, nikaona haina shida.

Akafungua Kofia yake (kumbe pesa wanafichia kwenye kofia) akanihesabia change, nikaweka mguu kati nikatimka! Hahahahaha nadhani mpaka kesho atakua ananisubiri wakati nilirudi Dar saa moja kasoro. The issue is, ile simu ukiweka chip haifanyi kazi, hai-detect simcard, nimepeleka kwa mafundi kibao imeshindikana. Ngoja nae apeleke kwa mafundi wake pia. akome kupenda vya dezo na rushwa
 
Haahaha hapo hujatapeliwa umejtapeli mara 3 mwenyewe.
 
  • Thanks
Reactions: Ok9

Ukitapeliwa sana na ww unakuwa tapeli.
Mimi nina uzoef sana na matapeli.
Nikimwona tu najua hapa pa bov
 
MCHAGA AIBIWI MARATATUU MUULIZE HUYO BABA KAMA KWELI KAZALIWA.MOSHI AMA WALE WAKUFIKIA
Hapo nilijitapeli mkuu.
Maana nilijipa matumain pasipo kitu.
Na ukiwa nje ya mchezo unaona ntapata.... Ukiona mwenzio amepata unaona sawa kumbe ni hao hao
 
Back
Top Bottom