Jinsi nilivyowahi kutapeliwa, Wewe je?

Jinsi nilivyowahi kutapeliwa, Wewe je?

Mi nishawahi temeshwa nywele na simu wakabeba hhahaaaaa mweee
Hahahah nakumbuka pia mm mwaka 2008 Ubungo nilifanyiwa hv hv nilitemeshwa nywele mzee, halaf wakanidanganya weka karama yako hapa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah enzi hzo nlikuwa na Nokia 6300 wakanipiga
 
Mimi majamaa ya vikadi yalinila buku 3 ya mboga ikanibidi nichane mifuko ya suruali na kwenda kudanganya nyumbani nimedondosha tukala mchicha badala ya samaki, ilikuwa 2007 shy town.
 
Hahaha umetapeliwa nawe ukatapeli....
 
Hahahah nakumbuka pia mm mwaka 2008 Ubungo nilifanyiwa hv hv nilitemeshwa nywele mzee, halaf wakanidanganya weka karama yako hapa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] dah enzi hzo nlikuwa na Nokia 6300 wakanipiga

Hahaha naona hapo hawakupati tena....
 
Mimi yaliyoo nikuta hata miezi 5 sina yaani nimelipa pesa kubwa mnoo na kufukuzwaa kazi maan nilipigwaa mzigo wa kampuni nikaonekana nimeibaa Mimi yaanii huyuu mpumbafu ningekuwaa naujuwaa uchawii angefanyiwaa. Kitu ambachoo sijui kingekuajee
Ntakuja isimulia nikija pata kazi tenaa maana nimeuonaa huu uzii yaanii nimekumbuka. Mbali sana ndo maana nikionaga mwizi lazima sheria mkononi nichukue

Mkuu mzigo ulipigwaje?
 
[QUOTE="ms nnana, post: 19166302, member: 40746wanalizwi hawa wanauza simu online... Walikua na duka Fulani LA simu hapa mjini.... Lakini mteja anatoa oda then wanaenda kuchukua simu nje... Nikalipa hela nikapewa na receipt ... Ebana nilizungushwa mpaka nikakata tamaa na duka likafungwa na kwenye duka alitokomea coz alitapeli wengi sana[/QUOTE]

Na huu utaratibu wa kuagiziana bado upo watu wanalizwa lkn hawana pa kusemea.
 
[QUOTE="ms nnana, post: 19166302, member: 40746wanalizwi hawa wanauza simu online... Walikua na duka Fulani LA simu hapa mjini.... Lakini mteja anatoa oda then wanaenda kuchukua simu nje... Nikalipa hela nikapewa na receipt ... Ebana nilizungushwa mpaka nikakata tamaa na duka likafungwa na kwenye duka alitokomea coz alitapeli wengi sana

Na huu utaratibu wa kuagiziana bado upo watu wanalizwa lkn hawana pa kusemea.[/QUOTE]
Kabisa na Mara nyingi ushahidi kunakua hamna
 
Hjajibu ya nywele bhana we mrembo.
Baada ya kumaliza form six niliamua kusoma computer course, sasa siku hiyo nimetoka zangu home kama kawaida, njiani nikakutana na rafiki yangu tulisoma nae tukapiga stori stori then tukabadilishana namba, sasa kumbe wakt naisave mwizi akanilia mingo.

Nimepiga hatua mbili mara tapeli akanisimamisha na kunisalimia, "dada habari, samahani mimi mgeni naulizia kwa mama mwanajeshi" nikamwambia mimi sipajui mara akapita mwenzie lkn akajifanya kama hawajuani akamsalimia kaka habar samahani naulizi kwa mwanajeshi, yule kaka wa pili akachangamka eeh huyo namjua hata huyu dada anapajua maana ndio njia anayopita kwenda kwenye masomo ya kompyuta. Mimi nikaguna we kaka umejuaje ?akasema nakuonaga sana kila siku ila sio shida twende niwasindikize tukikaribia mi ntakuelekeza ili umpeleke huyu kaka.

Basi njiani akamuuliza yule tapeli wa kwanza, " kwan kaka unamtafuta mwanajeshi wa nini? Tapeli akajibu mimi ni mganga na huyu mama tuliwahi kumsaidia kipindi fulan alikua anaumwa ss aametuita tena ana shida nyingine". Tapeli wa pili akadakia hee kumbe nyie ndio mlioneshwa TBC mmevaa majoho mekundu mkapewa zawadi, basi akajisifia sifia pale kumbe wananichota akili! Yule tapeli akanambia eti nyota yangu imefungwa watu wamenichezea , akaniambia" form six umepata div two ila ulitakiwa upate one" nikashangaa amejuaje nimepata two akanambia ww mguu wako mmoja wa kushoto unakuaga mzito kunyanyuka na bla bla zingne ila vyote alivyosema vilikua ni vya kweli .

Basi akauliza hauna kipande cha karatasi? Nikamwambia sina mara tapeli wa pili akampa gazeti, tapeli wa kwanza akalichana vipande akatupa tutafune kam dk tano akasema tuteme, kutema nywele nyingiiii akasema kohoa sana uteme zote zikatoka telee! Akadai watu wabaya wamenijaza nywele😀 Mara tena akatema mate kwenye kidole chake akasugua kwenye mkono wangu ukatoka moshi mwingii, badae akanambia niende kanisa lilikua karibu nikachukue pete ya bahati😛😛😛😛nikifika niseme utukufu juu mbinguni na aman duniani ila sitakiwi kwenda na vitu vya thamani so nimuachie yule mwenzangu yani tapeli mwenzie. Nikawapa kisamsung changu daaah na hela elf20 kufika kanisani hamna chchte akili ikazinduka nimeibiwa😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀Ila nikiwaona ntawakumbuka hawajanitoka akilini mpk leo
 
Hahhaa... Daaah pole sana , ila kila mtu ananjia yake ya utafutaji
 
Na wewe unatunywesha tu chai hapa ni vitu gani vya mjerumani vya million 500
Na humu jamii forum matapeli wapo wengi tu kuna jamaa mmoja wa humu jamii forum kuna jamaa alikuwa anatafuta vitu vya mjeruman vya kale sasa mzee wangu hivyo vitu alikuwa navyo nikawa nimeongea nae mimi nilikuwa tabora hiyo ilikuwa mwaka jana mwez wa kumi na mbili nikimwambia nikiludi mbeya likizo ntakutafuta ili unipe maelekezo kama ni vyenyewe au la tukakubaliana jamaa nikawa namtafuta yupo kimya nikaamua kutafuta mtu mwingine kweli wale watu wakaja nyumbani na mzungu wakaona vitu vile ni kweli vya kijerumani kwa hiyo biashara ikafanyika mzee alipewa kiasi kingi tu cha pesa kama milioni mi tano hivi na kidogo yule jamaa nikampotezea mwanzoni mwa mwezi wa kwanza akanitafuta kuulizia nikamwambia mbona biashara ilisha fanyika na wewe nilikuwa nikikupigia simu haupokei mara unasema nikutafute siku nyingine kwa hiyo mi nikatafuta mtu mwingine jamaa alisikitika sana tukawa tumemaliza hivyo nilikaa kama siku tano hivi jamaa yule yule akanipigia sim kwa namba nyingine akajitambulisha kwa jina la peter kisumo nikamwambia mbona sikufaham akasema tulikutana wilayani nikamjib sikufahamu kaka basi akaanze ehee sisi ni kampun tunao suply vifaa vya kilimo kwa hiyo tunaomba uwe wakala wetu nikamuuliza maswali ikaonekana anajikanyaga kanyaga eti tuma laki tatu afu si tutakuludishia kama milion hivi nikamuuliza wewe unataka kufanya biashara na mimi laki tatu ya nini kwa kifupi ni kamwambia utapeli wa kijinga huo watu walisha acha hayo jamaaa alikata simu na hakupatikana tena nazani na laini alitupa.
 
Ebw eeh, tuache utani, ingekuwa nguvu ya elimu inayotumika kutapelia ni kwa ajili ya maendeleo,kusema ukweli umasikini tungekuwa tulishaupiga kibuti kitambo. Matapeli wanatumia nguvu nyingi sana kuchora model ya uhalifu wao.
Nilivyostaafu nilisotea malipo yangu ya kiinua mgongo yapata miezi6.
Ulipofika mwezi wa saba mafao yakaingia kwa njia ya acct ya benki ya Nmb.
Sikumwambia mtu nikitarajia kwamba ni siri yangu na mke wangu.
Haikupita wiki wakaja vijana wawili wamevaa nadhifu kabisa, wakanipigia hodi. Nilivyowakaribisha wakajitambulisha kuwa wameagizwa na boss wangu kuwa ile hela mil5 aliyoniingizia kwenye acct yangu anataka msaada wangu nimuongezee mil3 aweze kununua eneo kwa ajili ya uwekezaji wa kimaendeleo. Ndiyo wao kawatuma kufuata kiasi hicho cha pesa.
Kwa kweli huyo boss tulikuwa tunaelewana nae sana, nisingeweza kumyima kumkopesha kiasi hicho cha pesa.
Cha ajabu boss huyo alikuwa hajawasiliana namimi kuhusu hiyo shida yake. Pia sikufahamu kama kwenye acct yangu kaingiza kiasi hicho cha pesa.
Nilipoanza kujihoji, wale vijana wakanidaka kuwa hakupata mawasiliano yangu kunijulisha adhima yake hiyo, lakini hana wasiwasi na mimi kumsaidia katika mpango wake huo kutokana na tunavyoaminiana, ndiyo maana kawatuma.
Ndipo nilipoanza kumtafuta kwa njia ya simu bila mafanikio. Simu yake haipatikani hewani.
Nikachukua simu kusachi salio kwenye acct Nmb mobile, nikakuta tarakimu ya kiasi cha fedha walichoniaminisha hao vijana kuwa mzee alikiingiza kwangu kwa lengo la kumuongezea, nikakuta hicho kiasi kimo.
Sasa kimbembe kilikuja pale kwenye kanuni niliyojiwekea kuhusu miamala ya pesa kukwama.
Nina acct mbili za benki. Ya kwanza ni acct ya Nmb. Hii ilikuwa imesajiliwa kwa ajili ya kupokelea mshahara wakati nikiwa mtumishi na ndiyo iliyokuwa imeingiziwa tarakimu ya kiasi hicho.
Ya pili ni ya Crdb. Hii hutumika kuhamishia fedha zozote ninazoingiziwa kwa njia yotote ile. Ni kama zizi la kufugia pesa zangu.
Kwa hiyo pesa zangu zote za mafao nilikuwa nilisha kisundia huko. Nmb ikawa inasoma 00.
Nilipoangalia salio la Nmb, kuona kiasi hicho na kabla sijaanza mchakato mwingine wa kuweza kumsaidia "mzee wangu" huyo, nikazikomandi hizo fedha kuhama kutoka Nmb kwenda Crdb, ndipo
Nilijibiwa kielctroniki kuwa salio halitoshelezi, nikaona hakuna ubaya, labda kwa kuwa ilikuwa 00 inahitaji kiwango cha kubakiza, hivyo nipunguze kiasi cha kuhamisha.
Nikakomandi ihame mil 4.5, ikagoma pia. Tena safari hii siyo kwa kauli ya salio lako halitoshelezi, bali " hatutaweza kukusaidia, kwa msaada zaidi piga…… huduma kwa wateja"
Ndipo nilisikia kama kuguswa na panya nikiwa usingizini nikashituka. Nikaelewa wazi kabisa kuwa kumbe nipo vitani na tayari nimeishazungukwa na adui.
Kwa kuficha kisirani changu na tamaa ya kudhalilisha tapeli ikanipanda.
Kwa haiba ya kinafiki na upole wa bandia, nikajifanya mjinga na ninamhurumia sana huyo jamaa yangu asije kukosa eneo alilokusudia kulipata.
Hivyo hakuna jinsi tuondoke pamoja kwenda benki ili nikatoe kiasi hicho cha pesa niwakabidhi.
Ebw,eeh kumbe walishanisoma dhamira yangu kwao, kwamba nilishashitukia dili na kinachofuata ni kucheza muziki.
Ndiyo hapo niliponza kuoneshwa kiburi cha wazi wazi.
Wakadai wao wanataka pesa keshi, mambo ya kwenda benki ni yangu. Na kama sina kiasi hicho cha fedha niwafahamishe ili wakauze kwingine na jamaa yangu akose.
Kwa upole uliojaa ghadhabu, nikawajibu kwamba, kiasi hicho cha pesa nnacho, ila kipo benki, tuongozane nikachukue niwakabidhi. Ushauri huo wakaukataa pia kwamba hawana muda.
Nikazidi kutetemeka kwa ghadhabu. Nikawaambia kwa kuwa mawasiliano ya simu hayapatikani baina yangu na huyo boss, basi tuongozane pamoja hadi kwa boss nikajikabidhi kwa kumhamishia salio kwa njia ya mtandao ili asikose eneo. Cha ajabu hata ushauri huo nao pia wakawa hawautaki.
Sasa hapo kwa kujiamini kabisa nikaona niwageuzie kibao kwa kuwaweka arrest.
Ebw ee ndipo kwa mara ya kwanza nilipoona tapeli akitimua mbio kama kibaka wa kawaida wa mtaani.
 
Daaaah hapo ungejutia kukaa kazini kwa miaka yote.
Lkn naamini kina nguvu ya ziada inayotumika maana haiwezekani mtu akusome una waza nn na una nn.
Hali hiyo ilishanitokea jamaa nataja kias ulichonacho direct. Duh
 
Baada ya kumaliza form six niliamua kusoma computer course, sasa siku hiyo nimetoka zangu home kama kawaida, njiani nikakutana na rafiki yangu tulisoma nae tukapiga stori stori then tukabadilishana namba, sasa kumbe wakt naisave mwizi akanilia mingo.

Nimepiga hatua mbili mara tapeli akanisimamisha na kunisalimia, "dada habari, samahani mimi mgeni naulizia kwa mama mwanajeshi" nikamwambia mimi sipajui mara akapita mwenzie lkn akajifanya kama hawajuani akamsalimia kaka habar samahani naulizi kwa mwanajeshi, yule kaka wa pili akachangamka eeh huyo namjua hata huyu dada anapajua maana ndio njia anayopita kwenda kwenye masomo ya kompyuta. Mimi nikaguna we kaka umejuaje ?akasema nakuonaga sana kila siku ila sio shida twende niwasindikize tukikaribia mi ntakuelekeza ili umpeleke huyu kaka.

Basi njiani akamuuliza yule tapeli wa kwanza, " kwan kaka unamtafuta mwanajeshi wa nini? Tapeli akajibu mimi ni mganga na huyu mama tuliwahi kumsaidia kipindi fulan alikua anaumwa ss aametuita tena ana shida nyingine". Tapeli wa pili akadakia hee kumbe nyie ndio mlioneshwa TBC mmevaa majoho mekundu mkapewa zawadi, basi akajisifia sifia pale kumbe wananichota akili! Yule tapeli akanambia eti nyota yangu imefungwa watu wamenichezea , akaniambia" form six umepata div two ila ulitakiwa upate one" nikashangaa amejuaje nimepata two akanambia ww mguu wako mmoja wa kushoto unakuaga mzito kunyanyuka na bla bla zingne ila vyote alivyosema vilikua ni vya kweli .

Basi akauliza hauna kipande cha karatasi? Nikamwambia sina mara tapeli wa pili akampa gazeti, tapeli wa kwanza akalichana vipande akatupa tutafune kam dk tano akasema tuteme, kutema nywele nyingiiii akasema kohoa sana uteme zote zikatoka telee! Akadai watu wabaya wamenijaza nywele😀 Mara tena akatema mate kwenye kidole chake akasugua kwenye mkono wangu ukatoka moshi mwingii, badae akanambia niende kanisa lilikua karibu nikachukue pete ya bahati😛😛😛😛nikifika niseme utukufu juu mbinguni na aman duniani ila sitakiwi kwenda na vitu vya thamani so nimuachie yule mwenzangu yani tapeli mwenzie. Nikawapa kisamsung changu daaah na hela elf20 kufika kanisani hamna chchte akili ikazinduka nimeibiwa😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀Ila nikiwaona ntawakumbuka hawajanitoka akilini mpk leo

Hapo walitumia nn uchawi au mazingaombwe.?
 
Asikuambie mtu ukishatapeliwa halafu ukaja ukafikiria jinsi walivyokutapeli lazima ucheke tu na kujiona kama mjinga yaani mimi nikikumbuka mawe ndani ya mfuko naambiwa ni Gearbox ya Rav4 huwa nacheka sana nikaunguza mafuta yangu na 30000/= zikaenda duh mjini timing tu ukiwahiwa huna ujanja
 
Mimi nilitapeliwa na wanaijeria wale wa mtandaoni. Walinitapeli laki tano mwaka2008.Kuna mna ijeria mmoja mdada aliomba urafiki fb akadai yeye ni mtoto wa mchungaji nk, eti wazazi wake wamefariki na wameacha pesa benki kwa hiyo nimsaidie aweke kwenye akaunti yangu. Urafiki uliendelea,nilikuja kujitambua baada ya kuibiwa, kumbe yalikuwa matapeli sugu, nilijuta kuwafahamu
 
Back
Top Bottom