Jinsi nilivyovalishwa sanda na mganga kisa mapenzi...

SUZANE

SUZANE

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Messages
746
Likes
56
Points
45
SUZANE

SUZANE

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2010
746 56 45
Leo sijui kwanini nimekumbuka hii stori!!!

Nawasalimuni nyote ndugu zanguni.

Nimiaka mingi kidogo imepita jambo hili lilinikuta.

Nilikua na boyfriend wng, siku zikaenda mpk akaja kuhitambulisha, baada ya muda wakanilipia mahari... Maisha yakawa yanasonga huku vikao vikiwa jikoni.

Nakumbuka cku moja rafiki yng Judy (rafiki wa moyo, msiba wake ni wangu, na shida yangu ni yake, siri zake zangu, zangu zake).

Basi siku moja Juddy akanipitia kazini kwangu, lkn alikua akilia sana na akilalamika kuwa anaumwa, basi niliomba ruhusa na boss wangu akaniruhusu nimpeleke hosp.

Basi tulipokua njiani Juddy akakataa kwenda hosp akasema nitaenda kesho, nilishangaa lkn ckua na la kufanya, tulikua tumekodi tax, ikamlazimu mwenye tax abadili njia tumpeleke mgonjwa nyumbani.

Basi tukafika kwa Juddy maeneo ya vatikan pale sinza, nikamuandalia maji ya kuoga na chakula cha usiku, then nikamuaga kuwa naondoka lkn Juddy hakuonekana kufurahi, alianza kulia na kulalamika kuwa nitamwachaje ndn peke yk wkt najua anaumwa!!! kiukweli nikawaza nikaona sio vema.

Basi nikamwambia ngoja niende nyumbani mara moja then ningerudi ili nikachukue na uniform za kazini kwa ajili ya cku inayofuata. Juddy alikataa kbs akidai kuwa nikimwacha lolote laweza tokea kwani hali yk sio nzuri.

Basi niliamua nilale, kilichofuata nilimpigia cm mchumba wng na kumweleza uhalisia kwakua anamfahamu Juddy hakuwa na neno. Nilioga kisha nikala nikalala lkn kwakua nililala na mgonjwa ckupata usingizi vzr kila mara niliamka na kumwangalia na nilimkuta macho hajalala basi nikapitiwa na usingizi tena, ila mara hii ulikua mzito sn nilipojaribu kumtizama juddy hakuwepo nilipotizama saa ilikua saa tisa kasoro, nilisubiri mpk saa 11 alfajiri juddy ndio alirejea tena akiwa uchi wa mnyama, alinikuta seblen kwake nikiwa nahangaika baada yakumtafuta nje tena kwa kusaidiana na majirani, tukipiga cm inaitia chini ya mto wake chumbani.

Kweli nilikasirika sana nikaita bajaji alfajiri ile nikasepa kwangu kwani ilikua c mbali napale. Ilonichukua kama dk 4 au tano kwa alfajiri ile mm kufika pale sinza madukani, nilijiandaa na kuelekea kazini kwangu.

cha ajabu ss, mchumba wangu akanipigia simu mida ya saa nne kuwa hanitaki tena, hiyo mahari nile na ndugu zangu yy haitaki wala hataidai...

Ilikua ni msiba kwng, Juddy akiwa mfariji no 1... , niliwaeleza ndg zng na hatua za mwanzoni za kutaka kuokoa uchumba huo zilianza, nilikua siwezi kufanya kazi tena wala kula, nilikua mtu wa kulia kila wakati, niliona huo nikama msiba mwingine. Mchumba wng hata wazazi wake walishangaa, dd zake walilia na mm, halikadhalika kk zk na wdg zk hakuna aliekua na jibu.

Baada ya kama wk 2 hivi yule mchumba wng akaenda kumtambulisha Juddy kwao kama mchumba wake mpya... tulipopata taarifa hiyo ndg zng wakaapa kuwa nasisi tukaloge mpk juddy aachike na yy...

Kwenye harakati za kuloga hapo ndipo tukajikuta tukiwa kwenye mikono ya mganga mmoja hivi huko tanga almaarufu DR MANDONDO, Niibaada ya wifi yng dd yk na mchumba wng kuagiziwa na rafiki yk. Tulifika ubungo na kulisaka basi la Burdani linalofika aliko mtaalam huyo.

Kiukweli nusu ya basi tulikua safari moja, tulifika usiku, tukaanza taratibu ambazo nasikia uvivu kuandika kwakua natimia cm.

ilifika zamu yng, nikaambiwa nilalie kitambaa cheupe ( sanda), nikawekewa kitu kama tunda fulani mdomoni, nikafungwa kama pipikifua, wakiniachia sehem ya kupumulia tu, nikabebwa kama maiti inavyobebwa mpk mahali fulani ckupajua ni wapi, nikawekwa juu ya kitu fulani hivi, wakaanza kusema maneno fulani ambayo sikuyaelewa.

Ngoja niishie hapa kwa leo... ila hivyo ndivyo mapenzi yalivyonifanya nivalishwe sanda kama mfu.

Msipende kuwaamini marafiki zenu kbs juu ya mahusiano yenu...

Usimpe mwanaume moyo wako wote, acha yy akupe wake.

Mungu humtafuta mtu kwa kuruhusu majaribu magumu...

Kwa kupitia hilo ndipo nilipomju Jehova vema, akanipa kila kitu kipya, biashara badala ya kazi, mume badala ya mchumba, nyumba badala ya kupanga, bd naendelea kumtumaini yy, japo Juddy amechezea tumbo lng nisipate mtoto lkn Mungu hana upendeleo ckumoja atanikumbuka...

Unataka kuuniuliza nn? mbona unasita?

imeandikwa amelaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu na moyoni amemwacha Bwana...

=====
Sehemu ya pili:
Ninayo kila sbb ya kumshukuru Mungu kwa kuwa amenipa kibali tena cku hii ya leo. Ninajua ni kwa Neema yake tu hata ww unasoma uzi wng huu. Nawashukuru nyote mliorushia sindano zenu kwenye ule uzi wng wa wk iliyopita ambayo mpaka leo bd uzi ule upo sokoni mkitaka kujua nn kilichoendelea.

Nachukua nafasi hii tena kuwashukuru wote walioniponda na kunisagia meno wakidai natunga, mara kusadikika, mara ooh, Nigerian movie nk, pia mmenifunza jambo jingune toka kwenu, hasa ww Faiza Foxy na wenzio wakina Mentor, Usiniguse na Fair Player...

Nawahakikishieni hii ni story ya kweli kbs wala sijaongeza chumvi zaidi nimeacha kuandika mengi tu.

Niliishia pale nilipokuwa nimeveshwa ile sanda. Baadae nilirudishwa kwenye chumba flani chenye mwanga hafifu sn kama vile kile kibatari kilikua kinaashiria kuwa mafuta yalikua ukingoni kuisha. Wakati bd naendelea kushangaa kile chumba nilistuka kidogo baada ya kusikia sauti moja nzito ikitokea upande wng wa nyuma ikiniamuru nimeze kitu flani alichokua amekishika, kwa mfadhaiko tena bila hata kuuliza swali nilipokea mkononi mwangu nikiwa bd nashangaa nikagundua zilikua mbegu za kitu flani ambacho sikujua ni nn, niliinua macho nikitaka niulize maji ya wapi lkn kbl cjauliza akaniambia meza bila maji alafu akageuka akasema nimfuate....

Nilifika nje nikakuta watu ni wengi mno, wanawake, wanaume, wazee, na watoto pia walikuwepo tena kwa wngi zaidi, basi tulichukuliwa tukagawanywa ktk makundi 3, wanawake, watt, na wanaume, kila kundi lilipelekwa upande wake, lkn hapa napo tukagawanywa tena, wakategwa wanawake wale wanao hitaji watoto, wanaotaka kinga kwa ajili ya kazi au biashara zao, waliokua wanahitaji kuizindika miili yao ili wasilogwe, mvuto wa biashara na mvuto kwa wanaume, wanaotaka limbwata, kuna wakina ss ambao tunataka ndoa kilazima, na makundi mengine mengi, tukatengwa, tulitembea km dk 15 hv, ikumbukwe kuwa ilikua ni usiku wa sa 7 hv, basi ktk kutembea tulijipanga mstari mmoja na kila mmoja alitakiwa atizame kichogo cha mwenzie ili mstari usipinde. Tulipofika kwenye eneo la tukio palikua na kundi la watoto wakiume waliofunga mishipi meupe kiunoni, tulitakiwa tupite kwao mmojammoja, zamu yng ilipofika nilienda nikafika kwa wakwanza akanichanja chale karibia 100 yaani zilikua hazina utaratibu mpk atosheke yy, ilifika mahali nilipigwa chale mpk za makalio mpk karibia na papuchi.

Tiba iliendelea mpk alfajiri tulipopanda Bus la Burdani kurejea dar, niliendelea na dawa zile bila mafanikio.

Baada ya mwezi tu Izok walihamia Mwanza na Juddy baada ya kupata uhamisho. Basi nilizimia moyo na ckuendelea tena na zile dawa!!.

Muda kama miezi 9 ilipita Izok alirudi kwao akisema kuwa Jud anataka kumfundisha uchawi, yy ndie alie toboa cri za Jud, ss tulijua lbd judy ni mshirikina tu, kumbe jud alikua mwanga vby sn, Izok anasema wkt mwingine wa usiku jud alikua anaondoka tng sa 7 anarudi alfajiri, jud alimweleza Izok jinsi ambavyo alivyotugombanisha siku ile, alimweleza kuwa cku ile nilivyolala kwake alivaa sura yng na kwenda kwa Izok, Izok akidhani ni ndoto alifanya na mm mapenzi, lkn kila akiingia na kutoka ilikua inatoka kama minyama iliooza ikinuka sn, Izok anasema ile harufu ilikua inamjia kila aliponikumbuka tu, Izok mbele ya mm na bb yk na familia yk alieleza huku akilia machozi, aliwaeleza ndg zk kuwa Jud alinichukua huku wakishirikiana na mm yk aliemfundisha uchawi na kunipeleka katika makaburi ya kinondoni na pale walifanya waliofanya ikiwa pamoja na kuzika chupi yng ktkt ya kaburi moja. Izok alilia machozi...

Baada ya kupigiwa cm na mama yake Izok akiniomba nipande basi niende Makanya alipokuwa anaishi, kwakua nilipedwa na kudhaminiwa kwenye familia yakina Izok sikua na mashaka, nilimpenda sn yule mm kwn alikua mpole, mnyenyekevu kwa watu na zaidi alikua mpole, keshoye nilipanda Kilimanjaro pale ubungo na safari ikaanza, majira ya saa 7 nilifika na nilikuta familia nzima wamekuja kunipokea, kiufupi hii familia ilikua ya ajabu walikua niwatu wenye uwezo, wakina Izok wote hakuna aliyesoma kayumba na vyuo wote walisomea nje lkn huwezi kuwajua mpk mtu akuambie.

Tulifika nyumbani, ndipo nilipomkuta Izok, nililia kwa uchungu sn, tukiwa tumekumbatiana kila mmoja alionyesha huzuni yk, baada ya muda tulitulia ndipo mm akaniambia alichoniitia, akasema hivi, tumehangaika sana, mpk mwenzio amerudi imetugharimu hivyo basi nataka mkaishi mbali kdg mpk mambo yatakapo tulia.

Nikaomba nipewe mda wa kufikiria kwanza, basi shangwe ziliendelea mok usiku tukaenda kulala na Izok, usiku ule tuliongea mambo mengi sn, alinielezea jinsi Jud alivyonifanyia mpk alivyotaka kumfundisha uchawi, tuliongea mpk saa 10 za usiku na muda uliobakia ulikua wa kukumbushana enzi za mwalimu, kwakweli nilijisikia raha sana na niliona fahari kwa kua na nimpendae..

Baada ya wiki tulisafiri mpaka Namibia tulipoanza upya maisha yetu... Baada ya mwaka tulirudi nyumbani na ghafla tu sikutaka kuendelea na Izok, nilikua nahisi ananuka kinyesi na wkt mwingine niliona sura yk inabadilika anakua kama mbwa, nilipata ugonjwa wa hofu na kila mara nilikua mtu wa kupiga mayowe, nilichakaa kiukweli, nilitia huruma.

Ndg zng walimshauri Izok atafute mke aoe aniache kwa kua walihofia kunipoteza, ktk kipindi hicho chote nilisomewa duaa mbalimbali na Mashehe kutoka ndn na nje ya Tanzania, nilikua nimtu wa kunywa makombe na mafusho ya kila aina, kwakua bd nilikua muislam na familia yng walishika dini sn waliamini ipo cku Allah angeniponya tu, lkn bdl yk nilianza kumenyeka magamba kama nyoka, papuchi ilikua inanuka kama mzoga wa panya... muda mwingi nilijitenga mwenyewe kuhofia watu wasisikie harufu mbaya wakaanza kunisema vby, nilikonda nikawa kama mkimbizi wa somalia, pua na mdomo navyo vilianza kutoa harufu, chumba nilichokua nakaa aliekua anaingia ni dd yng tunayeongozana kuzaliwa tu, aliniogesha, alinifusha dawa, akanitia moyo kuwa kuna ostadhi mmoja kiboko wamemtumia nauli anakuja kutoka msumbiji, yy ni kiboko wa kutoa majini, kweli alikuja baada ya cku 4, aliponiangalia akasema huyu amechukuliwa na anatumikishwa mahali, wanataka wamuue ili wamchukue mojakwamoja, basi inshort akaanza kunitibia baada ya wk niliweza kutoka sebleni kwa msaada wa fimbo, nilikua kama kikogwe flani kilichokosa huduma.

Miaka 2 nikiwa na hali ile, ndipo cku moja Namkunda dd yk na Izok aliporudi toka chuo alinitembelea, alistuka na kuanza kulia baada ya kuniona nilivyo, ndipo dd yng akamwambia mbona ss anaafadhali? Nilimuuliza hbr za kk yk lkn alianza kulia, akasema Izok alipata watoto mapacha wazuri sn na yule msukuma lkn baada ya mwaka wale watoto wamekua taahira wote! ss wanakaribia miaka 2 hali zao zinatia mashaka. Izok amepata strok ya ghafla amepooza mkono na mguu, mkewe nae alikua anapeta mchele akaingiwa na kipumba jichoni chakushangaza akapofuka jicho moja. Nililia kwa uchungu sn,nilimuhurumia Izok kwn hakua mtu wa maneno mengi...alikua ni mwenyehuruma sn na mwepesi wa kusamehe... nilitamani nikamwone lkn hakuna aliekua tayari kunisapot.

Baada ya mda cku moja alikuja Alice, huyu nilisoma nae chuo cha uhazili huko Nairobi, ni mtoto wa mch mmoja dar, alivyoniona akampigia daddy yk cm kumweleza hbr zng, mch yule alikuja kwa dd na akamuomba nikaishi kwake kwa muda kwakua vita niliyokua nayo ilikua kubwa, dd akakubali lkn akanisisitiza usikubali kubadili dini mdg wng...., basi.

Baada ya kama wk mbili nilianza kuona mabadiliko ya afya yng, nikaanza kupona kitu kimojakimoja, nilikua nafanyiwa deliverency kila cku, nywele zikaanza kuota kichwani,ile harufu ikakoma, ngozi yng ikawa inarudia asili yk, Alice akaniambia ss naliona tabasamu lako!!! Ckutaka kurudi tena kwa dd yng maana niliambiwa nikijinajisi tu yale mapepo yanaweza kurudi tena. Ilifika siku watu wanaenda kubatizwa na mie nikapita mbele, mch akasema jina la kitu ni kitu chenyewe, akafundisha kwa hbr ya majina nikaamini, akanipa jina jingine, akasema sitaitwa CHAUSIKU tena, huu ni mwaka wa tano tangu mambo hayo yaliponipata, cjawahi kubanduka knsn wala kumdharau yule mch ambaye ni kama bb yng kwa ss, Maisha yalibadilika kbs imebakia tu story kuwa niliwahi kuugua mpk nikafanana na kizee.

Izok nae alipata muujiza wake kutoka kwa TB Joshua baada ya kupelekwa na wazazi wk, mkewe na watoto wote walifariki mwaka jn. Izok alipoona nimeolewa aliamua akaishi nje ya nchi huko atafute maisha yk upia...

Nihivi majuzi tu nimeambiwa Juddy nae amefariki dunia.

Kwnn nisiishie hapa!! inatosha jamani...
CC watu8 IDUNDA kichomiz @Sucu MankaM SIRJENITO Nivea Crystal clear, Sista mischa Himidini Smile mwallu deepsea honey Faith utafiti chakii Preta kabanga amu Katavi Kifulambute binamutz Little Angel, Mapi Saint Ivuga, elifa nadili tabia ram DEMBA charminglady LILENDI mwanawao The Boss, Kongosho @Jizz1 kibella24 Valentina
 
Last edited by a moderator:
mischa

mischa

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Messages
375
Likes
73
Points
45
mischa

mischa

JF-Expert Member
Joined Mar 29, 2012
375 73 45
Mchumba wa zamani ikawaje sasa??yeye na juddy waliendelea?
 
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Messages
5,554
Likes
189
Points
145
Himidini

Himidini

JF-Expert Member
Joined May 8, 2013
5,554 189 145
^^
Umeongea mambo matatu ya muhimu sana,
Urafiki, Laana na Uzao
.
Ukumbuke kuwa mkono wa aliyekutendea hivyo hautaondoka duniani pasipo kulipwa (what goes around comes around) na kama hahusiki basi mapito hutuandaa kuthamini mema yatujiayo.
^^
 
Smile

Smile

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Messages
15,407
Likes
233
Points
160
Smile

Smile

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2011
15,407 233 160
duuuh sasa unaitaji kufufuliwa maana ulishazukwa zamani ujue?
 
mwallu

mwallu

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2013
Messages
6,779
Likes
166
Points
160
mwallu

mwallu

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2013
6,779 166 160
sasa Judy kakufungaje tumbo usizae wakati na yeye kaolewa huko?
halafu umeanza vizuri si ungemalizia tu bana...
 
deepsea

deepsea

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2013
Messages
3,257
Likes
226
Points
160
deepsea

deepsea

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2013
3,257 226 160
pole sana watu wa karibu ndo wanatuumiza siku zote
 
D

Dillish wa kwetu

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2013
Messages
227
Likes
3
Points
0
D

Dillish wa kwetu

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2013
227 3 0
Yesu ndio amekutoa katika hilo jaribu na yeye ndie atakaekupa huyo mtoto,hakuna kisichowezekana kwake,wanasema majaribu ni mtaji wa imani na kuna watu wanakuja katika maisha yetu kama baraka na wengine wanakuja kama funzo tu.usijute wala usilalamike kwa kuachwa na huyo mchumba huwezi juwa Mungu amekuepushia nini.
NB:asilimia kubwa ya marafiki si watu wazuri atakuchekea usoni lakini moyoni anatamani akutoe roho,tujifunze kuwa na kifua si lazima kumshirikisha kila kitu rafiki yangu,u have ur own mind and heart,u dnt need other people to make decisions for u.
 
Honey Faith

Honey Faith

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2013
Messages
15,844
Likes
5,762
Points
280
Honey Faith

Honey Faith

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2013
15,844 5,762 280
mi naomba kuuliza judy yeye aliolewa?
 
utafiti

utafiti

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Messages
12,817
Likes
111
Points
0
utafiti

utafiti

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2013
12,817 111 0
Pole lakini hongera kwa kushinda nguvu ya moyo wako
 
chakii

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Messages
17,010
Likes
14,861
Points
280
chakii

chakii

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2013
17,010 14,861 280
stori tamu hii ila mimi kama mwanaume vilevile sitokubali kumpa mwanamke moyo wangu au binadamu awaye yeyote maana nitakufa bila kuwa na huo moyo mimi mwenyewe,...
 
Preta

Preta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
24,203
Likes
3,349
Points
280
Preta

Preta

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
24,203 3,349 280
umenikwaza SUZANE............
 
Last edited by a moderator:
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Messages
31,647
Likes
5,065
Points
280
kabanga

kabanga

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2011
31,647 5,065 280
ah... ukija kumaliza uniambie...
 
MankaM

MankaM

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
9,485
Likes
434
Points
180
MankaM

MankaM

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
9,485 434 180
Leo sijui kwanini nimekumbuka hii stori!!!

Nawasalimuni nyote ndugu zanguni.

Nimiaka mingi kidogo imepita jambo hili lilinikuta.

Nilikua na boyfriend wng, siku zikaenda mpk akaja kuhitambulisha, baada ya muda wakanilipia mahari... Maisha yakawa yanasonga huku vikao vikiwa jikoni.

Nakumbuka cku moja rafiki yng Judy (rafiki wa moyo, msiba wake ni wangu, na shida yangu ni yake, siri zake zangu, zangu zake).

Basi siku moja Juddy akanipitia kazini kwangu, lkn alikua akilia sana na akilalamika kuwa anaumwa, basi niliomba ruhusa na boss wangu akaniruhusu nimpeleke hosp.

Basi tulipokua njiani Juddy akakataa kwenda hosp akasema nitaenda kesho, nilishangaa lkn ckua na la kufanya, tulikua tumekodi tax, ikamlazimu mwenye tax abadili njia tumpeleke mgonjwa nyumbani.

Basi tukafika kwa Juddy maeneo ya vatikan pale sinza, nikamuandalia maji ya kuoga na chakula cha usiku, then nikamuaga kuwa naondoka lkn Juddy hakuonekana kufurahi, alianza kulia na kulalamika kuwa nitamwachaje ndn peke yk wkt najua anaumwa!!! kiukweli nikawaza nikaona sio vema.

Basi nikamwambia ngoja niende nyumbani mara moja then ningerudi ili nikachukue na uniform za kazini kwa ajili ya cku inayofuata. Juddy alikataa kbs akidai kuwa nikimwacha lolote laweza tokea kwani hali yk sio nzuri.

Basi niliamua nilale, kilichofuata nilimpigia cm mchumba wng na kumweleza uhalisia kwakua anamfahamu Juddy hakuwa na neno. Nilioga kisha nikala nikalala lkn kwakua nililala na mgonjwa ckupata usingizi vzr kila mara niliamka na kumwangalia na nilimkuta macho hajalala basi nikapitiwa na usingizi tena, ila mara hii ulikua mzito sn nilipojaribu kumtizama juddy hakuwepo nilipotizama saa ilikua saa tisa kasoro, nilisubiri mpk saa 11 alfajiri juddy ndio alirejea tena akiwa uchi wa mnyama, alinikuta seblen kwake nikiwa nahangaika baada yakumtafuta nje tena kwa kusaidiana na majirani, tukipiga cm inaitia chini ya mto wake chumbani.

Kweli nilikasirika sana nikaita bajaji alfajiri ile nikasepa kwangu kwani ilikua c mbali napale. Ilonichukua kama dk 4 au tano kwa alfajiri ile mm kufika pale sinza madukani, nilijiandaa na kuelekea kazini kwangu.

cha ajabu ss, mchumba wangu akanipigia simu mida ya saa nne kuwa hanitaki tena, hiyo mahari nile na ndugu zangu yy haitaki wala hataidai...

Ilikua ni msiba kwng, Juddy akiwa mfariji no 1... , niliwaeleza ndg zng na hatua za mwanzoni za kutaka kuokoa uchumba huo zilianza, nilikua siwezi kufanya kazi tena wala kula, nilikua mtu wa kulia kila wakati, niliona huo nikama msiba mwingine. Mchumba wng hata wazazi wake walishangaa, dd zake walilia na mm, halikadhalika kk zk na wdg zk hakuna aliekua na jibu.

Baada ya kama wk 2 hivi yule mchumba wng akaenda kumtambulisha Juddy kwao kama mchumba wake mpya... tulipopata taarifa hiyo ndg zng wakaapa kuwa nasisi tukaloge mpk juddy aachike na yy...

Kwenye harakati za kuloga hapo ndipo tukajikuta tukiwa kwenye mikono ya mganga mmoja hivi huko tanga almaarufu DR MANDONDO, Niibaada ya wifi yng dd yk na mchumba wng kuagiziwa na rafiki yk. Tulifika ubungo na kulisaka basi la Burdani linalofika aliko mtaalam huyo.

Kiukweli nusu ya basi tulikua safari moja, tulifika usiku, tukaanza taratibu ambazo nasikia uvivu kuandika kwakua natimia cm.

ilifika zamu yng, nikaambiwa nilalie kitambaa cheupe ( sanda), nikawekewa kitu kama tunda fulani mdomoni, nikafungwa kama pipikifua, wakiniachia sehem ya kupumulia tu, nikabebwa kama maiti inavyobebwa mpk mahali fulani ckupajua ni wapi, nikawekwa juu ya kitu fulani hivi, wakaanza kusema maneno fulani ambayo sikuyaelewa.

Ngoja niishie hapa kwa leo... ila hivyo ndivyo mapenzi yalivyonifanya nivalishwe sanda kama mfu.

Msipende kuwaamini marafiki zenu kbs juu ya mahusiano yenu...

Usimpe mwanaume moyo wako wote, acha yy akupe wake.

Mungu humtafuta mtu kwa kuruhusu majaribu magumu...

Kwa kupitia hilo ndipo nilipomju Jehova vema, akanipa kila kitu kipya, biashara badala ya kazi, mume badala ya mchumba, nyumba badala ya kupanga, bd naendelea kumtumaini yy, japo Juddy amechezea tumbo lng nisipate mtoto lkn Mungu hana upendeleo ckumoja atanikumbuka...

Unataka kuuniuliza nn? mbona unasita?

imeandikwa amelaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu na moyoni amemwacha Bwana...
daaaa imeniuma nakunishtusha nimeumia zaidi uliposema huyo rafiki yako amekuchezea tumbo usiweze kupata watoto aisee naumia sana dada SUZZANE nimekumbuka ule uzi niloandika kuwa nahitaji dawa za asili za kuzuia mimba isiingie na nikakumbuka ulicomment kwamba wew unaomba usiku na mchana uipate lakin wapi. Nimeumia sana jaman nimejuta sana kwani nadhan nilikuumiza sana na ule uzi duuu mungu anisamehe bure. Nakuombea kwa mwenyezi mungu baba wa rehema akujalie uweze kupata mtoto nawe uwe na furaha maishani. Amen
 
Billie

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Messages
7,332
Likes
5,555
Points
280
Billie

Billie

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2011
7,332 5,555 280
Maana yake tuokoke au sio? Maana kama promo ya kwenda kwa Mwingira
 
usiniguse

usiniguse

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
1,454
Likes
515
Points
280
usiniguse

usiniguse

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
1,454 515 280
ndipo nilipomju Jehova vema, kwahiyo judi ni zaidi ya jehova kwa kukufunga tumbo siyo?Mwambie Yesu tabibu wa kweli afanye kazi yake siyo unakiri kirahisi tu
 
Forum statistics

Threads 1,237,180
Members 475,465
Posts 29,280,523