Jinsi nilivyoongea na viumbe wa ajabu

Jinsi nilivyoongea na viumbe wa ajabu

Nawasalimia kwa pamoja ndungu zangu wana JF.
Muda mrefu umepita nimekuwa nikiwaza sana kuhusu jambo hili lililonitokea tarehe 11/9/1990. Kila nikijaribu kumwambia mtu moyo unakataa nahisi kwamba hata nielewa na anaweza akaanza kuniogopa. Kipindi kile nilikuwa nilikuwa nimeingia kidato cha sita shule ya sekondari ya ILBORU nikiwa nasoma masomo ya sayansi.

Leo nimeona niandike humu huenda wapo watu watanielewa maana jambo hili nimekuwa nikiliwaza sana. Siku hiyo wanafunzi wote walikuwa wamelala ilikuwa usiku wa manane. Ghafla usingizi ulikata na nikapata msukumo wa kutoka kwenda nje. Basi nilifanya hivyo. Nikaenda kukaa kwenye mti ambao tulikuwa tunapendelea kukaa ili kupiga soga.

Ghafla nilipigwa mwanga usoni na kitu kilichotokea mbele yangu. Mwili wangu ukawa kama umepigwa shoti ya umeme, nywele zangu zote zikasimama, nikawa na jiona kama nimo ndani ya maji nikielea. Nikasikia sauti ikiniita jina langu J J J mara tatu. Naami nikaitika na kusema naam!!

Viumbe wawili wa ajabu walinisogelea mmoja akanigusa kichwani ndipo nguvu zikanijia. Wakaanza kunena na mimi; ni mambo mengi sana waliongea na mimi, lugha tuliyokuwa tunaongea nao kwakweli mpaka leo hii siwezi kuijua kuwa ni lugha gani. Bali tulikuwa tunaelewana. Walinipatia kanuni kadha wa kadha, ilinichukua muda kuzielewa.

Viumbe hao walinibeba kwenye chombo chao kilikuwa kinafanana na meli ambayo ni ya duara. Tuliondoka mpaka tukafika sehemu. Wakaniambia hapa ndipo chanzo cha nishati, wewe umeweza kuyaona haya tutakufunulia siri nyingi ili uweze kuwapatia wengi wajue ulimwengu huu. Wakasema sisi tunawaona mnahangaika sana elimu na ujuzi wenu bado upo chini sana maana hamuwezi hata kutuona sisi tukija huko. Uwezo wa macho yenu kuona ni mdogo sana, hata masikio yenu hayawezi kutusikia.

Viumbe hao wakanipatia formula mbalimbali na namna nitakavyo wafundisha wengine jinsi ya kujua siri nyingi. Nimejaribu kuzitumia formula kadha wa kadha naona zinafanya kazi.

Ninajitolea sasa kuanza kuwafundisha watu watakaokuwa tayari.

Kama kuna mtu mwenye swali karibu sana.
Picha?
 
Endelea tunafatilia kwa karibu, tukifika tutashukuru na bandiko lako nzuri, usiogope kutupiwa mawe.
 
Sasa wewe si zaidi yake mkuu, ndiyo maana ninakuaminia nikakuomba hata kapicha. Do black holes really exisist? Je black matter mkuu vipi?
Mzee si kila kitu lazima utupiwe picha. Einstein alileta General Relativity hatukuona picha. Unajua unanipotezea muda tupo na safari ndefu watu wanasubiri mengi toka kwangu.
 
Tatizo wewe mwenyewe ndo unazingua! Shusha mzigo wako hapo wa safari yako ataeamini sawa asieamini atalala mbele...
 
Mzee si kila kitu lazima utupiwe picha. Einstein alileta General Relativity hatukuona picha. Unajua unanipotezea muda tupo na safari ndefu watu wanasubiri mengi toka kwangu.
Mimi nimekusema wewe sijamsema Einstein wala Newton nimekusema wewe maana wewe si bora zaidi yao, hapo ni kusema huna au hutupii picha as simple as that siyo kujicompare na wao.
 
Ndio mana wafrica hatuendelei formula umepewa miaka ya 90 leo ndio unawapa wenzio.
Umeshajua ni formula gani au mihemko tu, kama ni formula ya kuwa mchawi na wewe unataka kuwa mchawi, wa bongo banah ni warahisi sana kuaminishwa ndiyo maana wanasiasa wanatudanganya kila siku na tunawapa tena kura zetu hata kama hawafanyi vizuri,
 
Nawasalimia kwa pamoja ndungu zangu wana JF.
Muda mrefu umepita nimekuwa nikiwaza sana kuhusu jambo hili lililonitokea tarehe 11/9/1990. Kila nikijaribu kumwambia mtu moyo unakataa nahisi kwamba hata nielewa na anaweza akaanza kuniogopa. Kipindi kile nilikuwa nilikuwa nimeingia kidato cha sita shule ya sekondari ya ILBORU nikiwa nasoma masomo ya sayansi.

Leo nimeona niandike humu huenda wapo watu watanielewa maana jambo hili nimekuwa nikiliwaza sana. Siku hiyo wanafunzi wote walikuwa wamelala ilikuwa usiku wa manane. Ghafla usingizi ulikata na nikapata msukumo wa kutoka kwenda nje. Basi nilifanya hivyo. Nikaenda kukaa kwenye mti ambao tulikuwa tunapendelea kukaa ili kupiga soga.

Ghafla nilipigwa mwanga usoni na kitu kilichotokea mbele yangu. Mwili wangu ukawa kama umepigwa shoti ya umeme, nywele zangu zote zikasimama, nikawa na jiona kama nimo ndani ya maji nikielea. Nikasikia sauti ikiniita jina langu J J J mara tatu. Naami nikaitika na kusema naam!!

Viumbe wawili wa ajabu walinisogelea mmoja akanigusa kichwani ndipo nguvu zikanijia. Wakaanza kunena na mimi; ni mambo mengi sana waliongea na mimi, lugha tuliyokuwa tunaongea nao kwakweli mpaka leo hii siwezi kuijua kuwa ni lugha gani. Bali tulikuwa tunaelewana. Walinipatia kanuni kadha wa kadha, ilinichukua muda kuzielewa.

Viumbe hao walinibeba kwenye chombo chao kilikuwa kinafanana na meli ambayo ni ya duara. Tuliondoka mpaka tukafika sehemu. Wakaniambia hapa ndipo chanzo cha nishati, wewe umeweza kuyaona haya tutakufunulia siri nyingi ili uweze kuwapatia wengi wajue ulimwengu huu. Wakasema sisi tunawaona mnahangaika sana elimu na ujuzi wenu bado upo chini sana maana hamuwezi hata kutuona sisi tukija huko. Uwezo wa macho yenu kuona ni mdogo sana, hata masikio yenu hayawezi kutusikia.

Viumbe hao wakanipatia formula mbalimbali na namna nitakavyo wafundisha wengine jinsi ya kujua siri nyingi. Nimejaribu kuzitumia formula kadha wa kadha naona zinafanya kazi.

Ninajitolea sasa kuanza kuwafundisha watu watakaokuwa tayari.

Kama kuna mtu mwenye swali karibu sana.
Sasa mkuu tangia mwaka 90 mpaka Leo ni zaidi ya miaka 30 umeshafanya nini cha maana baada ya kupewa hizo formula? By this time jina lako lingekuwa miongoni mwa wavumbuzi kama tunavyowasoma kina Galileo, Tesla, Sir Isac Newton tungekuwa tunajivunia kuwa Tanzania tuna mvumbuzi wa vitu fulani vinginevyo hii ni chai au una nia yako maalumu.
 
.
JPEG_20210203_073400_201437880166723458.jpg
 
Hongera mkuu
Za mida ndugu zangu.
Naona kuna watu wanaanza kutoa maoni yao. Wengine maenza kusema ninawatisha. Ninashukuru kwakuwa mmoja amejaribu kuleta picha za structure ya Insulin.
Ninauhakika anajua structure but hawezi kufanya manufacturing ya kitu hata kimoja.

Watu wengi wamekariri vitu ukiwaletea elimu nyingine wanakuwa wakari. Watu wanakuwa siyo wavumilivu. Nimejaribu tu kuleta insulin genome mtu mwingine amesoma medical analeta insulin structure.

Hapa nilikuwa naongelea genome. Unajua kuwa kuna project ilifayika miaka zaidi ya 5 wanasayansi wanajaribu kusoma genome ya Human!? Project hiyo ilikamilika mwaka 2003!?

Waligundua kuwa genome ya mtu ipo na sequence more than 3 billion.
Genes zilizotambuliwa ni more than 30,000. Sasa mimi najaribu kurahisisha ili watu wapate basics tuweze kwenda mbele.

NAOMBA TUVUMILIANE TU MIMI NIPO KWAAJILI YA KULETA SOLUTION. USITEGEMEE NITAONGELEA ISSUE YA PESA. TUNAMALIZANA HAPA HAPA.
 
Hizo formula nafundishia telegram kingilio buku,karibuni Sana.
 
Mtu nimescroll down from page 1 to 180 burnt my time apa nikitegemea nitakutana na formular konki alaf nakutana na propaganda tu... Uzi uhamishiwe kwenye jukwaa la siasa kule
 
Back
Top Bottom