Jinsi nilivyoongea na viumbe wa ajabu

Jinsi nilivyoongea na viumbe wa ajabu

Nawasalimia kwa pamoja ndungu zangu wana JF.
Muda mrefu umepita nimekuwa nikiwaza sana kuhusu jambo hili lililonitokea tarehe 11/9/1990. Kila nikijaribu kumwambia mtu moyo unakataa nahisi kwamba hata nielewa na anaweza akaanza kuniogopa. Kipindi kile nilikuwa nilikuwa nimeingia kidato cha sita shule ya sekondari ya ILBORU nikiwa nasoma masomo ya sayansi.

Leo nimeona niandike humu huenda wapo watu watanielewa maana jambo hili nimekuwa nikiliwaza sana. Siku hiyo wanafunzi wote walikuwa wamelala ilikuwa usiku wa manane. Ghafla usingizi ulikata na nikapata msukumo wa kutoka kwenda nje. Basi nilifanya hivyo. Nikaenda kukaa kwenye mti ambao tulikuwa tunapendelea kukaa ili kupiga soga.

Ghafla nilipigwa mwanga usoni na kitu kilichotokea mbele yangu. Mwili wangu ukawa kama umepigwa shoti ya umeme, nywele zangu zote zikasimama, nikawa na jiona kama nimo ndani ya maji nikielea. Nikasikia sauti ikiniita jina langu J J J mara tatu. Naami nikaitika na kusema naam!!

Viumbe wawili wa ajabu walinisogelea mmoja akanigusa kichwani ndipo nguvu zikanijia. Wakaanza kunena na mimi; ni mambo mengi sana waliongea na mimi, lugha tuliyokuwa tunaongea nao kwakweli mpaka leo hii siwezi kuijua kuwa ni lugha gani. Bali tulikuwa tunaelewana. Walinipatia kanuni kadha wa kadha, ilinichukua muda kuzielewa.

Viumbe hao walinibeba kwenye chombo chao kilikuwa kinafanana na meli ambayo ni ya duara. Tuliondoka mpaka tukafika sehemu. Wakaniambia hapa ndipo chanzo cha nishati, wewe umeweza kuyaona haya tutakufunulia siri nyingi ili uweze kuwapatia wengi wajue ulimwengu huu. Wakasema sisi tunawaona mnahangaika sana elimu na ujuzi wenu bado upo chini sana maana hamuwezi hata kutuona sisi tukija huko. Uwezo wa macho yenu kuona ni mdogo sana, hata masikio yenu hayawezi kutusikia.

Viumbe hao wakanipatia formula mbalimbali na namna nitakavyo wafundisha wengine jinsi ya kujua siri nyingi. Nimejaribu kuzitumia formula kadha wa kadha naona zinafanya kazi.

Ninajitolea sasa kuanza kuwafundisha watu watakaokuwa tayari.

Kama kuna mtu mwenye swali karibu sana.
Itakuwa walinzi wakimasai walikubananisha
 
Ndio mana wafrica hatuendelei formula umepewa miaka ya 90 leo ndio unawapa wenzio.
Ahaaaaaaaaaaaa mbavu zangu dah jf.labda alitaka kwanza uzaliwe na usome ujiunge jf uje kusoma uzi huu
 
Kuna formula rahisi naimalizia kuiandika inahusiana na Virus to Body Integration and Differentiation.
Hahahah!

Hii bonge ya chai aisee...

Halafu pale Umenyeni, ni sehemu gani kuna mti ambao madenti wamezoea kukaa chini yake na kustorisha?

Huo mti upo wapi, kule pitch, pale chapel, oldonyo, rungwe, kwa mama tony????
 
Mkuu kwa nini unawadanganya watu? DNA structure ya Insulini ina 51 amino acids ambazo zimegawanyika ktk chain A na B. Chaina A ina 21 AA na chain B ina 30 AA.

Hizi formula hazina uhusiano wowote na mtu kuweza kufanya body differentiation & integration.

Sema kwa sababu unaona kuna novice wengi wa haya mambo umeamua kuwakusanya na kuwatishatisha na hivi viformula vya DNA sequence.

Ndio maana kila ukiambiwa ulete formula ya kufanya hizo science ulizofundishwa na hao viumbe unakwepa kwepa kwa kuleta vitu visivyo na uhusiano kabisa.

Hii hapa structure ya insulin[emoji116]



View attachment 1692954

View attachment 1692960
Sisi tulosoma HGL kazi tunayo tunasoma comments tu😁😁
 
CAUSALITY

Ili tuweze kwenda ndani zaidi na tuweze kuelewa formula niliyoiweka ni muhimu tukajua causality jinsi ilivyo.

Kwanza kabisa napenda kuongelea kuhusu milango ya fahamu na namna inavyo athili hii formula na hatimaye kuathili genome.

MEMORY

Kwenye miili yetu kuna memory za aina mbili:

  • Brain Memory
  • DNA Memory
Kwa wale wanaotumia computer wanaweza kuelewa ninachoongelea. Kwenye computer kuna taarifa zinakuwa zinehifadhiwa kwenye HDD, ROM na RAM. Vivyo hivyo kwenye miili yetu kuna taarifa ambazo huhifadhiwa maeneo tofauti tofatu.

Taarifa hizo zinaweza kuongezwa, kufutwa au kubadilishwa. Hatua hiyo inategemea taarifa hizo zinazofutwa au kuongezewa zinakuwa na umuhimu gani.

DNA Memory

Hizi ni taarifa zinazohifadhiwa na zinaweza kupitishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine. Hizi taarifa zinakuwa zimehifaziwa na kama ninavotendelea kuongea kuhusu genome.

Matukio mbalimbali yanayotokea yanaweza kuathili genes na kufanya zipite mpaka kwa kizazi kinachokuja.

Kuna vitu vingi vinaweza vikaathili kufanya information ziweze kupelekwa mpaka kwenye kizazi kingine vitu hivyo:-

  • Tamaduni
  • Hali ya hewa
  • Aina ya vyakula
  • Mazoea ya tabia fulani
  • Mlipuko wa magonjwa
Vitu hivyo vinaweza kuathili taarifa zinazohifadhiwa kwenye genome na kufanya zipitishwe toka kizazi kimoja kwenda kwenye kizazi kingine.

Ikitokea utajijegea tamaduni ambazo zinakuwa na negative impact kwako; siku baada ya siku itasababisha modification kwenye genome sequence. Ukifanya kitu mfululizo kwa muda wa siku 7 utajenga mazoea na mazoea yakikomaa itakuwa tabia na hiyo tabia ikiendelea kuwepo itasababisha modification kwenye genome na ukitokea ukazaa mtoto baada ya tabia hiyo uwezekano wa mtoto kuwa na tabia hiyo ni 50%.

Wazungu wameweza kweli kutuathili sisi waafrika katika suala hili na limeweza kupita kwenye vizazi vyetu. Wametuzoeza kuwa tegemezi kwao; sasa inakuwa ngumu sana kwetu sisi watu weusi kuweza kufanya mambo kwa kujiamulia sisi maana ipo kwenye DNA zetu. Kinachotakiwa ni kuanza kufanya mazoezi ya kujitegemea na kuwa wewe na ndipo tutazalisha kizazi cha watu wenye uelewa mkubwa.

NInajaribu kuongea kwa kifupi ili tuweze kujua causality namna gani inavyofanya. Pale tutakavyo improve causality positively tunaongeza uwezo wa Physical Experience. Lakini causality pekee haiwezi kukamilisha hicho maana lazima factors zote tatu ziende kwa pamoja. Causality ikiwa negative inapunguza P.

BRAIN MEMORY

Brain memory imegawanyika katika makundi mawili.

  • Temporary memory
  • Permanent memory
Sitaki niongelee sana kuhusu hili swala, maana watu wengi tunalijua. Lakini ninachotaka kuongelea hapa ni mambo mawili:

  • Intellectual
  • Intelligence
Ninataka niongelee masuala haya katika context hii ya causality. Kwahiyo sasa Intellectual ni speed ya kuchukua taarifa kutoka kwenye memory na kuziweka wazi. Intelligence ni uwezo wa kuafuta namna ya kuzitumia taarifa zilizohifadhiwa kwenye memory.

Katika Context hii tunaweza kujifunza mambo yote haya mawili namna ya ku improve na kufanya causality iweze kuongezeka.

Inatakiwa kujua ni taarifa gani tunazozihifadhi kwenye Brain. Kama ni taarifa negative kwahiyo kitakacho tokea ni kupata taarifa za namna hiyo.

Kuna milango sita ya fahamu: -

  • Macho
  • Masikio
  • Ulimi
  • Ngozi
  • Pua
  • Fikra(Thought)
Hii milango ya fahamu tunatakiwa kuitumia vizuri maana vinaigiza taarifa kwenye brain na zingine zinahifadhiwa permanently. Mtu akijizoeza kuingiza kwenye brain vitu vibaya automatically vitu hivyo vinaweza vikaathili namna ya anvyoishi.

Hata katika hili wazungu wamefanya kitu kikubwa katika kuhakikisha wanatufanya tuathilike katika matukio ya kila siku.

Mfano: Mtu anapokuwa mpenzi sana wa mpira always atakuwa amehifadhi mambo hayo.

Jinsi ya kuweza kujitibu sisi wenyewe ni kuanza kujizoesha kufanya vitu vingine vinavyokuwa na positive. Nitapo anza kuongelea SP nitagusia haya maana SP nayo kwa sehemu huwa inatumia milango ya fahamu. Nitaongelea namna ya kuodoa negative data zilizohifadhiwa kwenye ubongo.

Sasa basi ninapoongelea causality ninaogelea physical activities vinavyoathili mwenendo wa Maisha.



NITAENDELEA…


Mkuu unakuja kuja... embu tuendelee tuone
 
Kama alivyoanza marehemu dr shika. Na pia Nalimi balimi tunaye humu naye huwa dish likiyumba channels zina scratch sana. Unaona kidogo mara ina stuck ndo miasha yalivyo.

Halafu jamaa kasimuliwa sana hbr za Aliens kiasi kwamba sasa anaanza hallucinations.
 
Chombo hakiwezi kufanana na Meli halafu tena kiwe cha mviringo

Myth,
 
Kama jambo hili limemtokea mtoa mada mwaka 1990, nina imani kwasasa ni mtu mzima anayejielewa, na kufikia maamuzi ya kuanzisha uzi ni kwa lengo la ku-share yale yaliyomtokea kwa lengo la wote kujifunza na hata kutoka na kitu ambacho kinaweza msaidia mmoja au mwingine.

Kitendo cha wengi kusema huyu mwamba ana matatizo siyo sawa na siyo sahihi na haya anayoelezea sio rahisi kwa mtu wa kawaida na asiye kuwa na uelewa hata kidogo wa masuala ya ulimwengu na yote yaliyomo (ulimwengu ni tofauti na Dunia hivyo usitafsiri neno hilo kwa kufikiria dunia tunayoishi).

Mhusika katoa utofauti mzuri sana kati ya intellectual na intelligence hapa panawasumbua hadi wasomi wetu wakubwa yaani wengi wapo kundi la intellectual na kuna baadhi wametoa comment zao hapa.

Wengi tumefanikiwa kukusanya taarifa na kuziweka kichwani (kusoma) ila kuzitumia na zilete matokeo ndiyo shida ilipo.

Elimu bahari na kuna mengi ambayo hatuyajui hadi leo japo yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kuathiri maish yetu ya kila siku.

Anapojitokeza mtu kwa hiari yake ku-share kitu kwa lengo la watu kujifunza basi tumuhukumu mwishoni baada ya kuona amemaliza na aliyotoa ni tofauti.

Mkuu Venus Star usisahau jf iliingiliwa na vijana wengi wadogo ambao bado hata hawaelewi namna maisha yalivyo na jinsi mambo yanavyotokea, hivyo baadhi puuzia na uendelee kutoa shule. Kuna shule kubwa sana kwako hata ukiacha hizo formula ambazo wengi ndo wanasubiria, ila ndani ya maelezo yako kuna shule pana sana.
 
Back
Top Bottom