Kuna kitu nilifanya mwaka jana ambacho watu wengi waliniona kama nacheza mchezo wa ajabu kidogo.
Nilikaa siku 100 nzima bila kuangalia saa.
Hakuna sababu maalum. Sikuamka asubuhi nikasema tu moyoni, “leo naanza.” Nikajiambia nione kama inawezekana kuishi kawaida kabisa bila kujua muda ni saa ngapi.
Kitu cha kwanza nilifanya ni kuacha kabisa kuvaa saa ya mkononi. Ile saa ya ukutani nayo niliiondoa pale sebuleni kwa sababu nilijua macho yangu yataikimbilia tu bila kufikiria.
Simu yangu nayo nilijitahidi sana nisiangalie sehemu inayoonyesha muda.
Mwanzoni ilikuwa inanisumbua kidogo. Unajikuta mkono unaenda mfukoni kuchukua simu halafu ghafla unakumbuka, “hapana, leo siangalii saa.”
Lakini baada ya siku chache nikaanza kuzoea.
Nilianza kuamka tu bila kujua ni saa ngapi. Nikihisi njaa nakula. Nikihisi usingizi nalala. Siku zinaenda tu bila mimi kujua muda umefika wapi.
watu wengi walikuwa wanashangaa.
Mtu anakwambia, “sasa hivi ni saa ngapi?”
namwambia sijui.
Wengine walidhani natania.
Lakini ukweli ni kwamba kwa zile siku 100 sikujua kabisa muda ni saa ngapi kwa siku yoyote.
Na kitu nilichogundua ni hiki: baada ya muda mwili unaanza kujipangia mambo yake tu. Unahisi tu muda wa kula umefika, muda wa kupumzika umefika, au muda wa kwenda nje umefika.
Kuna siku nilikaa na watu wakawa wanabishana muda umeenda haraka au polepole. Mimi kichwani kwangu siku ilikuwa inaenda kawaida kabisa.
Changamoto pekee ilikuwa pale mtu anaponiambia tukutane saa fulani. Hapo nilikuwa namwambia tu anipigie au anifuate maana mimi sina habari na saa.
Baada ya kufika siku ya 100 ndipo nilipoamua kuangalia saa tena.
Nilihisi kama nimeingia tena kwenye ulimwengu ambao kila mtu anaishi akifuatilia namba tu ukutani.
Lakini ukweli ni huu…
Inawezekana kabisa kuishi bila kuangalia saa.
Na saivi nampango wa kukaa siku 300 kwamaana inatuliza akili