Jinsi nilivyo keketwa na kunusurika kifo

Jinsi nilivyo keketwa na kunusurika kifo

SUZANE pole sana;

Pole kwa kumpoteza mama R.I.P mama suzane.

Pole pia kwa huo ukatili waliokufanyia hao wabibi.

Ni heri hivi ulivyofunguka walau
tusaidiane katika kukupunguzia machungu.

Je, huyo bibi bado yupo?
 
mnyikungu 14:45 Today
So sad, nina girlfriend ambaye yamemkuta yaliyokukuta,
kiukweli siku naongea naye alilia kwa uchungu, alisema
siwezi kuishi naye na siwezi kumkubali kisa kakeketwa,
nilimuonea huruma, nilimkuta bikra akiwa na umri wa
miaka 24, muda wote alikuwa anawaogopa wanaume
kisa tarizo lake hilo, nilimuhaidi nitampenda kadri ya
uwezo wangu, toka siku ile kidogo anajihisi mtu, japo
muda mwingine huwa analia bila sababu kila
akikumbuka, mara nyingi humlaumu mama ake,
natumia muda mwingi sana kumuliwaza, sitaweza
kumuacha kisa kakeketwa, na mimi nitakuwa
nimeungana na mangariba, anahitaji sana faraja yangu,
hakika haya mambo tuwe tunasimuliwa tu

wanaume wachache waliio kama ww, be blessed
 
Tamaduni zingine tuziandike tu iwe historia.
Mi nakumbuka siku nilipotahiriwa ambapo govinda langu lilifyekwa pyuu... hadi leo nimebaki kichwa wazi... dah..
 
Daa, pole ya dhati kutoka ndani ya moyo wangu.

Hawakukutendea haki hata kdg.
Mungu awalipe shari hapahapa duniani kabla hata hawajafika mbinguni.

Laanakum zao.
 
Aisee nimepiga picha eti wale wanangu wawili wa kike wakeketwe, mngesikia nimeanzisha westgate huko kwa ngariba, uzuri kwetu hatuna hiyo mila potofu! Pole sana dada angu, walikufanyia jambo la ukatili sana!
 
pole sana dada... yakubidi uwe balozi wa kweli...naamini hata hapa JF wapo na inawauma sana...poleni wote kwa ujumla
 
kwani ulishajua ladha ya kuwa nacho na kutokuwa nacho?
 
pole sana dada kwa mkasa huo.nakushauri ujiunge na wanaharakati wa kupinga unyama huo (ikiwa ni pamoja na TAMWA) ili kukomesha hili. by the way, nakuhurumia pia wakati uwapo faragha na mumeo. nahisi (kama tunavyosoma athari za FGM) husikii ile raha ya hadi 'kisogoni'. waweza tupa evidence katika hilo? mumeo hana shida kwani hamna tofauti ktk starehe anayoipata - ni ile ile.
 
Dangire 15:17 Today
pole sana dada kwa mkasa huo.nakushauri ujiunge na
wanaharakati wa kupinga unyama huo (ikiwa ni pamoja
na TAMWA) ili kukomesha hili. by the way, nakuhurumia
pia wakati uwapo faragha na mumeo. nahisi (kama
tunavyosoma athari za FGM) husikii ile raha ya hadi
'kisogoni'. waweza tupa evidence katika hilo? mumeo
hana shida kwani hamna tofauti ktk starehe anayoipata -
ni ile ile.

kiukweli kbs, kuhusu raha ya tendo la ndoa ukilinganisha na wanawake wengine ni mara chache sana naisikia, kwakua kila mara mumewangu akitaka kupeleka mkono nakosa amani kbs
 
Naikumbuka siku ile nilipoitwa nyuma ya nyumba kule kijijini kwetu. nikaambiwa nitanue miguu then wabibi flan wakanitazama kwa makini sana, ckujua kitu kilikua kinaendelea....

Baada ya cku kadhaa, asbh sn nikaamshwa nikavalishwa kanga moja inatopita shingoni, kwetu inaitwa (maleleta)

safari ikaanza kuelekea msituni kwa kua nilikutana na wenzangu kama 10 hivi tuliiokua tunasoma pamoja darasa la pili sukuogopa wala kujali chochote.

Baada ya muda tulilifikia pori fulani walilokua wameandaa hapo tukawekwa mapumziko.

Haikuchukua muda akachukuliwa wa kwanza..., 2, 3 ... lkn hawakurudi pale tulipokua, mimi zamu yangu ilikua ya sita...
Niliingizwa kwenye pori lililojitenga, nilianza kupata hofu baada ya kumuona bibi mmoja akiwa amelowa damu karibia mwili mzima, mama mmoja akanivua ile kangha yng, nikaanza kulia, nikitaka kukimbia lkn ckufua dafu...

nikakukumbuka wazazi wangu waliofariki, nilimwita mm yng aniokoe lkn hakutokea, hakukua na msaada wowote ule kwa wakati ule...

nililazwa chini, nilimuona yule ngariba akiwa na kisu kilichopinda kdg mithili wa vile vya kukatia majani, akanisogelea na kupeleka mkono wake moja kwa moja kwenye papuchi yangu, huku nikiwa chini nimeshikiliwa siwezi hata kujitingisha nilisikia maumivu makali yakipenya ktk mwili wangu, ngariba alikua anakiondoa kiungo kimoja kwenye mwili wangu bila ya ganzi, damu nyingi sana zilinitoka mpk kupoteza fahamu...

ckujua tena kilichoendelea kwa muda wa cku mbili... nilivyopata fahamu nilikua dhaifu sana. cwezi kucheza tena na wenzangu, cwezi kwenda shule, nilikua mtoto wa kukaa ndani mpaka mwezi ulivyoisha...

hivyo ndivyo nilivyonusurika na kifo baada ya kufanyiwa tohara, sasa naishi kwa matumaini kama wanawake wengine, mume wangu amenikubali hivihivi nilivyo...

nailaani tohara mwanzo na mwisho, nawalaani mangariba wote...
:amen: :amen:
 
Mimi pia huwa nalaani kwa nguvu zote hii tabia ya kukeketa wanawake,sio kwamba wana tofauti sana katika love making na hawa ambao hawajafanyiwa ila kinachonitia huzuni ni ukatili unaotumika kufanya kitendo chenyewe.My take,kama serikali zimeshindwa kuitokomeza hii mila potofu kwanini wasibuni utaratibu ambapo hili jambo liwe linfanyikia kwenye ma-hospitali kama ilivyo kwa wanaume!!!
 
So sad, nina girlfriend ambaye yamemkuta yaliyokukuta, kiukweli siku naongea naye alilia kwa uchungu, alisema siwezi kuishi naye na siwezi kumkubali kisa kakeketwa, nilimuonea huruma, nilimkuta bikra akiwa na umri wa miaka 24, muda wote alikuwa anawaogopa wanaume kisa tarizo lake hilo, nilimuhaidi nitampenda kadri ya uwezo wangu, toka siku ile kidogo anajihisi mtu, japo muda mwingine huwa analia bila sababu kila akikumbuka, mara nyingi humlaumu mama ake, natumia muda mwingi sana kumuliwaza, sitaweza kumuacha kisa kakeketwa, na mimi nitakuwa nimeungana na mangariba, anahitaji sana faraja yangu, hakika haya mambo tuwe tunasimuliwa tu

Wewe ni mtu mwema sana
 
inasikitisha, pole sana SUZANE
 
Last edited by a moderator:
nawashukuru sana sana... japo sio rahisi kusahau kwa kua lazima nijisafishe kila wakati, hua kila nikipeleka mkono ikulu lazima nikumbuke tu...
yaani pole sana mamii .. mnara una raha yake asikuambie mtu ! unakosa chanel nyingi sana jamani...tbc,radio ya wafu,radio one hadi bbc ila bila mnara hata tbc inakwaruza mweee
 
Tamaduni zingine tuziandike tu iwe historia.
Mi nakumbuka siku nilipotahiriwa ambapo govinda langu lilifyekwa pyuu... hadi leo nimebaki kichwa wazi... dah..
sasa ulitaka ubaki nalo na wewe?
 
inasikitisha sana,kama katika karne na dunia ya leo ya digitali watu wamekumbatia mila potofu,hasa wa baba ndio wanasisitiza watoto wao wa kike wakakeketwe hasa mkoa wa mara
 
pole sana bidada,mila zingine kwa kweli hazifai ila basi tu.2005 nilishawahi kuwa na girlfriend aliyefanyiwa hivyo,tulikuwa chuo kimoja hivi,nilipata tabu sana,yaani unaweza kuwa unaweza kukaa hata mwezi mzima hajakupa mambo anadai hajisikii,ila siku akijiskia hata iwe wapi ni lazima utampa tu.akijiskia tu atataka kwa nguvu zote.ilinipa tabu sana,wakati mwingine mko kwenye mitihani,inakuwa hamna jinsi,ule muda mchache wa kujisomea inabidi mtafute faragha tu kwani bidada ameshataka.sometymz naumia nahitaji but bidada anasema hawezi coz hana feelings zozote.na hata umshike vipi mdada mkavu mkavu,sana sana inakuwa kama vile unabaka hivi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom