Jinsi nilivyo keketwa na kunusurika kifo

Jinsi nilivyo keketwa na kunusurika kifo

SUZANE

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Posts
740
Reaction score
502
Naikumbuka siku ile nilipoitwa nyuma ya nyumba kule kijijini kwetu. nikaambiwa nitanue miguu then wabibi flan wakanitazama kwa makini sana, ckujua kitu kilikua kinaendelea....

Baada ya cku kadhaa, asbh sn nikaamshwa nikavalishwa kanga moja inatopita shingoni, kwetu inaitwa (maleleta)

safari ikaanza kuelekea msituni kwa kua nilikutana na wenzangu kama 10 hivi tuliiokua tunasoma pamoja darasa la pili sukuogopa wala kujali chochote.

Baada ya muda tulilifikia pori fulani walilokua wameandaa hapo tukawekwa mapumziko.

Haikuchukua muda akachukuliwa wa kwanza..., 2, 3 ... lkn hawakurudi pale tulipokua, mimi zamu yangu ilikua ya sita...
Niliingizwa kwenye pori lililojitenga, nilianza kupata hofu baada ya kumuona bibi mmoja akiwa amelowa damu karibia mwili mzima, mama mmoja akanivua ile kangha yng, nikaanza kulia, nikitaka kukimbia lkn ckufua dafu...

nikakukumbuka wazazi wangu waliofariki, nilimwita mm yng aniokoe lkn hakutokea, hakukua na msaada wowote ule kwa wakati ule...

nililazwa chini, nilimuona yule ngariba akiwa na kisu kilichopinda kdg mithili wa vile vya kukatia majani, akanisogelea na kupeleka mkono wake moja kwa moja kwenye papuchi yangu, huku nikiwa chini nimeshikiliwa siwezi hata kujitingisha nilisikia maumivu makali yakipenya ktk mwili wangu, ngariba alikua anakiondoa kiungo kimoja kwenye mwili wangu bila ya ganzi, damu nyingi sana zilinitoka mpk kupoteza fahamu...

ckujua tena kilichoendelea kwa muda wa cku mbili... nilivyopata fahamu nilikua dhaifu sana. cwezi kucheza tena na wenzangu, cwezi kwenda shule, nilikua mtoto wa kukaa ndani mpaka mwezi ulivyoisha...

hivyo ndivyo nilivyonusurika na kifo baada ya kufanyiwa tohara, sasa naishi kwa matumaini kama wanawake wengine, mume wangu amenikubali hivihivi nilivyo...

nailaani tohara mwanzo na mwisho, nawalaani mangariba wote...
 
Duuuh pole sana sistee, ni janga kubwa sana hilo. Wengine huwa wanadevelop PTD (post traumatic disorder) hali inayowafanya kutotamani hata kuja kuolewa maishani! God is gud!
 
pole sana dada umenisikitisha sana hapa machozi yananidondoka! I am so sorry my dear!Mwenyezi Mungu halali na ni mwema atakufanyia wepesi na kukulinda ktk maisha yako yote inshaallah!
 
So sad kwa.kweli inaumiza sana sana!!!!!!

Nimewahi kumsikia mdada mmoja kwa masikio yangu akisimulia hii kitu yeye akiwa muhanga kuna mambo yanatisha na kuhuzunisha sana hapa duniani na hili ni moja wapo!!!!

Pole sana.dada Suzane na hongera kwa mumeo pia!!!!!!!
...that true love is everything
 
Dah! pole sana nina imani utakuwa balozi mzuri wa maswala hayo
 
Hivi kwanini wanawake wanafanyiwa tohara?? huwa najiuliza hili swali lakini sijawahi kupata jibu?? hata waliofanyiwa kitendo hiki huwa hawana jibu! SUZANE naomba uwe BALOZI mzuri wa kueleza madhara ya tohara. Tena siku hizi mangariba wamegundua kuwatahiri watoto wangali wachanga.
 
Mmmm! mazito pole sana mrembo,mwili unanisisimka kwa khofu,mie nilikua nasema nimepelekwa mdogo unyagoni na niloyaona kule niliapa sitompeleka mwanangu mpaka afikie wakati wakuolewa,lakini haya yakwako mazito mungu akupe wepesi shogo na ampe mumeo ujasiri wakua na wewe maisha....
 
nawashukuru sana sana... japo sio rahisi kusahau kwa kua lazima nijisafishe kila wakati, hua kila nikipeleka mkono ikulu lazima nikumbuke tu...
 
story inaumiza yaani mesisimka
 
nawashukuru sana sana... japo sio rahisi kusahau kwa kua lazima nijisafishe kila wakati, hua kila nikipeleka mkono ikulu lazima nikumbuke tu...

Wahoji hao vibibi kwa nn wanatoa ving'amuzi
 
Pole sana ndg kwa ukatili uliokumbana nao ktk umri mdogo wa kutafakari upendo wa wazazi. Wasamehe bure kwani wengi wao hawajui wanalofanya ila wanasukumwa na mazoea.
 
Pole sana..inauma aisee kufanyiwa jambo bila kuwa na ufahamu nalo au ridhaa nalo

Mshukuru sana Mungu kukupatia mwenzi wa maisha aliyekupenda na kukujal ukiwa hivyo

Hongera kwa kupata ujasiri wa kusema hili kwani kwa kiasi fulani unakuwa umepunguza hasira na uchungu,pole sana
 
So sad, nina girlfriend ambaye yamemkuta yaliyokukuta, kiukweli siku naongea naye alilia kwa uchungu, alisema siwezi kuishi naye na siwezi kumkubali kisa kakeketwa, nilimuonea huruma, nilimkuta bikra akiwa na umri wa miaka 24, muda wote alikuwa anawaogopa wanaume kisa tarizo lake hilo, nilimuhaidi nitampenda kadri ya uwezo wangu, toka siku ile kidogo anajihisi mtu, japo muda mwingine huwa analia bila sababu kila akikumbuka, mara nyingi humlaumu mama ake, natumia muda mwingi sana kumuliwaza, sitaweza kumuacha kisa kakeketwa, na mimi nitakuwa nimeungana na mangariba, anahitaji sana faraja yangu, hakika haya mambo tuwe tunasimuliwa tu
 
Pole sana dada Suzan....according to your explanation hicho kitendo kimekutokea ukiwa uchaggani tena Rombo!! This is inhuman na kama wanafanya hivyo hadi leo it is a shame!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom