Naikumbuka siku ile nilipoitwa nyuma ya nyumba kule kijijini kwetu. nikaambiwa nitanue miguu then wabibi flan wakanitazama kwa makini sana, ckujua kitu kilikua kinaendelea....
Baada ya cku kadhaa, asbh sn nikaamshwa nikavalishwa kanga moja inatopita shingoni, kwetu inaitwa (maleleta)
safari ikaanza kuelekea msituni kwa kua nilikutana na wenzangu kama 10 hivi tuliiokua tunasoma pamoja darasa la pili sukuogopa wala kujali chochote.
Baada ya muda tulilifikia pori fulani walilokua wameandaa hapo tukawekwa mapumziko.
Haikuchukua muda akachukuliwa wa kwanza..., 2, 3 ... lkn hawakurudi pale tulipokua, mimi zamu yangu ilikua ya sita...
Niliingizwa kwenye pori lililojitenga, nilianza kupata hofu baada ya kumuona bibi mmoja akiwa amelowa damu karibia mwili mzima, mama mmoja akanivua ile kangha yng, nikaanza kulia, nikitaka kukimbia lkn ckufua dafu...
nikakukumbuka wazazi wangu waliofariki, nilimwita mm yng aniokoe lkn hakutokea, hakukua na msaada wowote ule kwa wakati ule...
nililazwa chini, nilimuona yule ngariba akiwa na kisu kilichopinda kdg mithili wa vile vya kukatia majani, akanisogelea na kupeleka mkono wake moja kwa moja kwenye papuchi yangu, huku nikiwa chini nimeshikiliwa siwezi hata kujitingisha nilisikia maumivu makali yakipenya ktk mwili wangu, ngariba alikua anakiondoa kiungo kimoja kwenye mwili wangu bila ya ganzi, damu nyingi sana zilinitoka mpk kupoteza fahamu...
ckujua tena kilichoendelea kwa muda wa cku mbili... nilivyopata fahamu nilikua dhaifu sana. cwezi kucheza tena na wenzangu, cwezi kwenda shule, nilikua mtoto wa kukaa ndani mpaka mwezi ulivyoisha...
hivyo ndivyo nilivyonusurika na kifo baada ya kufanyiwa tohara, sasa naishi kwa matumaini kama wanawake wengine, mume wangu amenikubali hivihivi nilivyo...
nailaani tohara mwanzo na mwisho, nawalaani mangariba wote...