Jinsi mitumba inavyotuunganisha na watu tusiowapenda!

Mtoa mada sijui akili zako zipoje,umekuja kutangaza ushoga ama? Kwani ukienda mgahawani huwezi kula chakula kilichopikwa na Shoga? Hiyo suti mpya unayovaa je haijashonwa na Shoga? Chumba ulichopanga hajawahi kupanga kahaba kabla yako? au mwizi? au yeyote yule usiyempenda? Usihukumu usije ukahukumiwa.
wewe na mtoa mada mnagombania ushoga ama?😭
 
Ndiyo. Ulitumiwa na binadamu kama mimi. Ila Hoja ya kwamba eti alikuwa-kuwaje tabia yake havinihusu.
Sasa huo ni mtizamo wako. Hebu fikiria Kuna watu wanawachukia Sana watu wengine hadi kujiapiza kuwaua. Sasa jee mtu kama anachukia majambazi hajisikii hatia kutumia kitu cha aliyekuwa jambazi??
 
Nilidhani unazunugumzia Psychometry/Psychic touch ability to sense things, information and such, just by touching things.
 
Mitumba upande wa nguo zinazoletwa Africa kwanza mitumba imechoka , imechakaa michafu

Ndo tunaleta ili tuvae ni umasikini tu.

Kukuta nguo ya mtumba ya maana ni Nada Sana.

Tukubali kuwa sisi ni dark country
Mkuu huna taarifa sahihi. Mitumba ina grades 1,2,3 etc. Grade 1 huwa ni kama mpya au mpya. Mtu anaweza kupewa zawadi ya nguo asiipende basi anaipeleka charity huko inakusanywa na mitumba au fashion imepita wenye maduka wana donate, uchakavu au ubora wa nguo ni nyinyi kama nchi mnaamua. Mfano Kenya wanaruhusu mitumba grade 1 tu na Tz wanaruhusu takataka zote kiasi kwamba mtu akitaka kuuza mitumba quality inabidi aifuate Nairobi hapo bei unafikiri itakuwa?
 
Asubuhi ya leo wakati navua raba nilipotoka mazoezini, ghafla lilinijia wazo la ni nani alikuwa anaivaa raba hiyo kabla haijaletwa Tanzania kama mtumba?

Nikaanza kuangalia jinsi mitumba ilivyotawala maisha ya Watanzania kwa kiasi kikubwa Sana. Lakini huwa tunajiuliza hiyo mitumba ilikotoka ilikuwa inatumiwa na nani?

Kwa mfano magari ingawa hatupendi sana kuyaita mitumba, badala yake tunayaita "Used" lakini ukweli wa mambo na yenyewe pia ni mitumba.

Unaweza kuwa unachukia watu wenye tabia ya ushoga, lakini una hakika mitumba unayotumia hakuna ambao ulikuwa unatumiwa na shoga kabla ya wewe kuununua?

Ipo mitumba toka kwa wezi, majambazi, makahaba, watu wa dini tofauti na sisi, wabaguzi, wauwaji, wafungwa, wabakaji, matapeli na lundo jingine kubwa sana la watu tusiowapenda.

Unapotumia mtumba jua kuwa inawezekana kabisa kabla ya kuletwa Tanzania huko ulikotoka ulikuwa unatumiwa na mtu/watu usiowapenda kabisa.
da!! mwanangu wewe ni jiniazi,,,umenifanya niichukie mitumba lakini sina jinsi kipato changu kidogo,,kumbe ndo manake MAGUFULI alitaka kupiga marufuku mitumba!!!!
 
Mitumba upande wa nguo zinazoletwa Africa kwanza mitumba imechoka , imechakaa michafu

Ndo tunaleta ili tuvae ni umasikini tu.

Kukuta nguo ya mtumba ya maana ni Nada Sana.

Tukubali kuwa sisi ni dark country
Dark Country maana yake ni nini?

Mbona Unalazimisha? Kama umechoshwa si unahama tu? Aisee.
 
Baniani mbaya... Mjadala ni kumbe unaweza kuchukia tabia ya mtu ila vitu vyake ukavipenda na kuvitumia!!
Nimekuelewa vyema. Ukimuondoa huyo baniani.

Bwana Allen una shauri lipi lifanyike?

Tupige marufuku?

Tuwapende na tuvivae, ama.
 
Back
Top Bottom