SoC02 Jinsi kilimo kilivyobadili maisha yangu

Stories of Change - 2022 Competition

King Nabora

New Member
Jul 18, 2022
2
3
Guzman ni miongoni mwa vijana wachache wenye umri wa miaka 30 ambaye amefanikiwa sana kimaisha, haikuwa rahisi kwake kijana huyu aliyeanza mapambano ya kimaisha akiwa na umri wa miaka 23 kufanikiwa kama ilivyo rahisi kuandika simulizi hii, ilikuwa ni safari ngumu sana kwa kijana huyu msomi mwenye shahada ya usimamizi biashara, kama kijana naamini simulizi hii itazidi kukupa nguvu ya kupambana hivyo fuatilia hadi mwisho kujua namna alivyoweza kufanikiwa.

Harakati za kimaisha za Guzman zilianza toka kipindi akiwa kwenye masomo yake ya elimu ya chuo kikuu kwani alifanya shughuli tofauti za kiuchumi ikiwemo biashara ndogo ndogo pamoja na ufugaji wa kuku, mara tu baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu ya chuo kikuu alikuwa tayari anamwanga wa maisha ya nje ya masomo, ni suala la kawaida kwa vijana wengi kujisahau wakati wakiwa masomoni hata wale wa elimu ya juu kama vyuo vikuu, wengi tumekuwa na Imani za kuamini tukimaliza masomo zipo kampuni na mashirika ya umma ya kutuajiri ivyo watu wengi wameishi bila kujiongeza na kua vipofu wa fursa fursa mbali mbali za kufanikiwa kimaisha na kusababisha kua na idadi kubwa ya vijana wasio na ajira wala kujiajiri. Licha ya usomi wake tofauti na wasomi wengi wa kitanzania, Guzman hakua muumini wa ajira ila alijiamini kua anauwezo wakufanikiwa kupitia biashara na kua ipo siku atakuja kuajiri vijana wenzake.

Kutokana na elimu yake ya biashara pamoja na uzoefu aliopata kwa kufanya shughuli mbalimbali ilikuwa ni wakati sahihi kwake kuchagua biashara moja atakayoanza nayo Ivyo alianza utafiti wa kibiashara na akachagua kufanya kilimo cha biashara kwa kuwa aliona kuna fursa nyingi sana za kukuwa na kufanikiwa kimaisha tena kwa kuanza na mtaji mdogo.

Je! Kwanini kilimo kati ya biashara zote?

1. Guzman katika malezi yake amekulia kijijini hadi alipokua na umri wa miaka 12 ivyo maisha yake yote ya awali yameendeshwa na pesa zilizotokana na kilimo,

2. Kilimo ni sekta huru ambayo haiitaji vyeti au urasimu wowote kuingia na kuanza shughuli zako,

3. Kilimo hakiitaji mtaji mkubwa sana kama zilivyo biashara nyingine,

4. Kilimo kina nafasi kubwa za kukua hata kama ulianzia chini kabisa na

5. Kilimo kinakupa uhuru wakufanya shughuli zingine za kiuchumi na pia kijamii.

Hivyo chaguo la kufanya kilimo lilikua ni sahihi kwake kijana uyu mwenye moyo wa kupambana, ila kutokana na changamoto mbali mbali kama mabadiliko ya tabia nchi, mbegu zisizo na ubora, madawa feki ya kilimo, na masoko ya sio ya uhakika na pia kukosa uzoefu wa kilimo cha kisasa, kilimo kimekuwa na changamoto ya kimisimu kitu kulichofanya kilimo kuonekana kama bahati nasibu, ila siku zote palipo na nia hapokosi njia.

Kama ilivyo kawaida mafanikio yoyote hayajawahi kua rahisi au ya usiku Mmoja kua umelala maskini na uamke tajiri, kunahitaji moyo wa simba moyo wa kutokata tamaa, na ilikuwa ivyo kwa kijana huyu ambaye alipitia changamoto nyingi sana ila aliweza kuuona mwanga tena.

Katika safari yake ameanguka mara nyingi ila haikuwa sababu ya yeye kukata tamaa, na kama unavyojua makosa kidogo kwenye kilimo yanaweza kuathiri mwaka mzima au msimu mzima na makosa yake huweza kurekebishwa mwakani au baada ya msimu mwingine na pia hiyo haikupi garantii ya kusema utapata pia mwakani au msimu unaofuata haswa pale unapokua unapambana ukiwa huna mtaji wa kutosha kumudu mradi wako au ukiwa huna ujuzi kamili wa mradi unaofunya na pia usipokua mwepesi kurekibisha makosa yako, lengo la aya hii sio kukutisha au kukukatisha tamaa ila yakupasa kujua ukweli kua yakupasa kua makini sana kama umechagua kilimo kama biashara yako vinginevyo ni ngumu sana kuona mafanikio.

Katika harakati zake za kujikwamua baada ya anguko la mara kwa mara ndani ya kipindi cha miaka mitatu yake ya mwanzo kijana alihangaika sana kupata namna ya kuendesha miradi yake ila mambo yalikuwa magumu kutona na historia ya familia yake kuwa ametokea katika familia duni ambayo haikua na msaada mkubwa wa kifedha ivyo ili mlazimu kufanya mambo mengine yaliyomwezesha kupata fedha za kuendesha miradi yake hadi pale alipoona fursa ya shindano la kuandika na kushinda lilipokuja kubadili historia ya maisha yake. Ikumbukwe kua Guzman ni msomi mzuri ivyo hufanya mambo yake kwa mpangilio mzuri kitu kilichomuwezesha kufungua ukurasa mpya wa historia ya maisha yeke.

Fursa moja haiwezi kuzuia fursa nyingine ila fursa moja huweza kuleta fursa zingine, vivyo hivyo katika kipindi kigumu kwa kijana guzman hakuacha kuangalia fursa zingine zakuweza kumuongezea nguvu katika shughuli zake za kilimo, ndipo ilipotekea fursa kama hii ya Story of Change ya Jamii Forums ilikua mwaka 2019 Kijana huyu alipoweza kupata fursa iliyobadilisha maisha yeke na kumfanya kua kijana aliyefanikiwa hivi sasa.

Guzman ni miongoni mwa washindi wachache kutoa hapa Tanzania aliyeweza kushinda katika programu maalumu inayoandaliwa na mfanyabiashara na mfadhili mkubwa kutoka nchini Nigeria ambaye huwapa vijana wengi wa kiafrika fursa za kufanikiwa kwa namna moja ama nyingine.

Fursa ilikuwa ni kuandika wazo la kibiashara na ukifanikiwa kuwasilisha wazo zuri unapata ufadhili wa mradi wako kwa dola za kimarekani 5000/= ili kuwa ni programu kubwa ambayo pia ni endelevu mwaka hadi mwaka. Washiriki ni wengi sana na washindi pia ni wengi ila inahitaji umakini na ufasaha kwenye uandishi.

Watu wengi wanakuaga na desturi ya kuupudhia fursa kama hizi na huisi kama ni utapeli ila kwa guzman ilikua tofuti andiko hili ndio limekua mwakozi wa maisha yake, Fedha hizi zilikua nyingi mno kwa mahitaji ya kijana huyu ili kufikia malengo yake ivyo aliweza kuzipangilia vizuri sana na kwa weledi mkubwa ivyo kumfanya kufanikiwa katika safari yake ya kilimo.

Ukurasa mpya wa historia ya maisha yake ulifunguka na pia kufungua kurasa mpya kwa vijana wengi kwa ajira mbali mbali zile za muda na za kudumu Zaidi ya watu 50 kila mwaka tokea mwaka 2020 wameweza kunufaika na miradi ya kijana Guzman. Kilimo ni ajira, kilimo kinalipa, kilimo ni uhai na kilimo kinaweza kuinua taifa letu na kuondokana na umaskini na uhaba wa ajira.

Kazi iendelee

Imeandaliwa na kuchapishwa na BERNARD E. NABORA
 
Back
Top Bottom