Jinsi Kikundi cha Al Shabaab kinavyotengeneza fedha

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,438
Jinsi Kikundi cha Al Shabaab kinavyotengeneza fedha. Kinakusanya kodi sehemu nyingi kuliko Serikali ya Mogadishu, Somalia.

Wana mashushushu bandarini. Kila shehena zinapoingia, wao wanajulishwa. Mmiliki wa shehena hatoi mzigo bandarini mpaka Al Shabab walipwe chao.

Maeneo yote yanayoshikiliwa na Al Shabab, wafanyabiashara wanalipa kodi kwa Al Shabab, Serikali ya Mogadishu haichukui.

Maeneo ambayo yanashikiliwa na Serikali, wafanyabiashara hulazimika kulipa kodi mara mbili. Serikalini na kwa kuwalipa Al Shabab.

Vilevile, Al Shabab hukusanya zaka kwa lazima kwa wafanyabiashara. Kila mfanyabiashara hupaswa kuonesha rekodi zake za biashara kwa mwaka. Kisha hutakiwa kulipa asilimia 2.5 ya faida walizopata kwa mwaka kama zaka.

Usisahau jamaa hawajaacha utaratibu wao wa kuteka meli hasa za mafuta na kupora. Al Shabab ni matajiri sana na wana nguvu. Ndio maana imekuwa vigumu kuwashinda.

©Luqman MALOTO
 
Makundi mengi ya organised crime wanatumia style hiyo......
Hata mungiki kenya wanakusanya viushuru fulani ktk maeneo kadhaa

Ova
 
Aina ya maisha waliyochagua ndio sio nzuri. Maisha ya kukosa uhuru
 
Back
Top Bottom