tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,765
- 29,209
Wakuu naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Ukweli ni kwamba There is no free lunch in Africa. Kwa kuzingatia hili, hebu tujiulize hawa wafanyabiashara walioichangia CCM mabilioni ya pesa kwa mbwembwe na hadharani watarejeshaje fedha zao walizochanga? Tukumbuke kwamba hawa wachangiaji ni wafanyabiashara na fedha walizochangia wamezinyofoa kwenye mitaji ya biashara, tena kwa ghafla kwa kushtukizwa kwani uchangiaji huu haukuwa kwenye malengo yao ya kibiashara. Na pia tukumbuke kule CCM hakuna biashara yoyote itakayofanikisha marejesho ya haya mabilioni ya fedha za mtaji wa biashara ambazo wamezimwaga ndani ya CCM.
Sijafuatilia sana jambo hili lakini, katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati nikipita social media, nimeshangazwa kusikia kampuni moja kubwa ya biashara hapa nchini ikitangaza kuchangia Tsh bilioni 10, ambazo ni sawa na 10% ya fedha zilizokadiriwa kuchangwa.
Kabla tujiulize wafanyabiashara hawa watarejeshaje hizi fedha zao, tunapaswa kujiuliza kuhusu matumizi ya michango hii. Hivi karibuni tumeshuhudia CHAUMMA wakinunua maelfu ya magari na kuyasambaza nchii nzima wakati kinafahamika ni chama masikini na hakijawahi kuitisha mchango wowote. Isije ikawa CCM wanajenga kwa jirani huku kwao kukizidi kuporomolewa na akina Polepole na genge lake. Je, CHAUMMA wamepata wapi ghafla fedha za kununua magari haya? Baada ya michango hii huenda CHAUMMA watanunua magari mengi zaidi au watapata fedha za kutosha kukodi chopa za kuzunguka kwenye kampeni nchi nzima. Tusubiri tuone itakavyokuwa.
Tukirejea kwenye jinsi fedha za wafanybiashara zitakavyorudi nimeangalia katika nyanja tofauti. Uwanja wa kwanza ni kupitia ukwepaji kodi wa makusudi. Hawa wachangiaji kuanzia sasa watakuwa wakwepaji wakubwa wa kodi kwani wanajua fika kuwa wameishajipenyeza kwenye mfumo wa chama na serikali kama ambavyo Rostam Aziz amefanya. Sasa hivi Rostam hagusiki kabisa. Anaogopeka zaidi ya Rais. Rostam na Kikwete sasa hivi utadhani ndio wanaongoza nchi kwa remote.
Namna ya pili ya kurejesha hizo fedha ni maelekezo kutoka juu. Kwa kuwa sasa hawa wachangiaji wameingia sebuleni mwa CCM watakuwa wanafanya biashara bila kulipa kodi kwa maelekezo kutoka juu.
Namna nyingine ni kwa kuogopwa na maofisa wa TRA na kuachiwa wapite bila kulipa kodi kwa nidhamu ya uwoga. Wakaguzi wa TRA watakapogundua kuwa mizigo inayopita bandarini ni ya mchangiaji wa CCM, hawatamgusa....watamuachia apite bila kulipa kodi.
Mwisho, njia nyingine maarufu itakayotumiwa na mafisadi hawa walioichangia CCM ni kwa kupandisha bei za bidhaa au kupunguza kipimo kwani sasa wanajua fika kuwa wanaogopwa na TRA na wakala wa vipimo na uzito. Hii nchi ukitaka kuila vizuri kaa karibu na CCM.
Je, wewe mdau wa JF, ukitafakari vizuri na kwa utulivu, unadhani ni jinsi gani hawa wafanyabiashara watarejesha mabilioni yao waliyochomoa kutoka kwenye mitaji ya biashara na kuichangia CCM, ukizingatia kuwa CCM hawafanyi biashara itakayozalisha fedha ili wazirejeshe.