Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

A

cha kusoma kamstari kamoja tu kwa ajiri ya kujifurahisha. Soma kipengere chote hapa:-

148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.
Nili quote ka sehemu ako peke kurahisisha suala langu kwako, kwakuwa msingi mzima wa section na sub one yake inajenga preamble ya hicho nilichocopy na closure yake ni msisitizo wa hoja ya mamlaka ya rais.

Ndio maana nauliza tena je? Kuzuia mikutano ya siasa ni mambo yanayohusiana na vita?
 
Umenena vyema mkuu. Ila umesahau kuwa kuna njia nyingi za ku lodge case mahakamani ikiwemo ya kumfanya defendant wako kuwa complainant.
Kwa hiyo Ukuta una create case of public interest with curiosity, hii itazifanya mahakama zetu ku act promptly katika kutoa maamuzi yenye tafsiri ya vifungu vya katiba yetu
Mkuu soma vzr nilichokiandika usikurupuke!
Nimesema pamoja na katiba kutoa haki kadhaa ikiwemo kuandamana, lkn pia imetoa limitations, and one of the limitations ni readons of public interest.
Kwamba there are tymes when those rights can be taken away for reasons of public interest, na nikasema bahati mbaya katiba na sheria zingine hazija define what amounts into public interest hivyo kitu hiki kinatoa room kwa watu Ku limit hizo haki ikiwemo haki ya kuandamana kwa muamvuri wa public interest, na ni katiba imetoa loophole hiyo.
Kwahiyo kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara inapata baraka chini ya kifungu hicho cha 30(1) mkuu.
It is for public interest, what are they?! No body knows bcoz katiba haisemi wala hakuna sheria inayosema!
 
Kama ujui ungeomba ushauri na sio kuja na full concluded thread afu utegemee tuje kukutoa tongotongo ishi nazo siku ukitumbukia tutakuja wanasheria tukutoe afu utulipe kwa ukilaza wako haahhahahahaha ila usipaniki ndugu ntakutoa tongo tongo ukiwa serious kukiri umekosea
Hebu ona sasa umekuja mzima mzima. Kwikwi. Rudi sasa kwenye mada tukadili.
Kwanza haki zako unazijua? Je mbele ya rais wewe una haki gani kikatiba?
 
Nili quote ka sehemu ako peke kurahisisha suala langu kwako, kwakuwa msingi mzima wa section na sub one yake inajenga preamble ya hicho nilichocopy na closure yake ni msisitizo wa hoja ya mamlaka ya rais.

Ndio maana nauliza tena je? Kuzuia mikutano ya siasa ni mambo yanayohusiana na vita?
Rais akiwa kama amiri jeshi mkuu anaweza kutumia vyombo vya ulinzi kulinda nje au ndani si kutokana na vita pekee bali akiona usalama wa raia unaathiliwa au yeye akiona inavyofaa.

Soma tena using'ang'anie kwenye vita wakati katiba imempa uhuru wa kutumia majeshi anavyoona inafaa.
 
Mjadala huu ni mzuri sana kama utakua umeuvua uchama au wewe unavyojiona na ulivyo katika nafasi yako.
Kuna watu humu mnatamba kua mko vizuri kwenye sheria na mnapiga hela sasa najiuliza wewe ni mwanasheria au jizi tu!
Wengi mnajikita kwenye haki za binadamu katika kujadiri issue iliyo hot leo lkn sheria ya vyama vingi mnaikacha... Tuongelee katiba na sheria ya vyama vingi... UKUTA sio issue ya HR no..
 
Tatzo vijana wengi mmeshikiwa akili, akishasema Lissu basi nyie mnadhani ni sawa, Lissu anatumia Article 18 ya katiba inayotoa right of Association, anatumia pia sheria ya vyama vya siasa ambayo imefafanua haki inayozungumziwa chini ya kifungu cha 18 cha katiba.
Hivyo sheria ya vyama vya siasa unapata uhali kutoka kwenye katiba, which means, sheria ya vyama vya siasa is applicable subject to the constitution ambayo ndo sheria mama from which all other laws derives their legitimacy!

Sasa mtoa maada ameainisha Article 30 ambayo imelay down limitations on the enjoyment of the basic rights under part3 including Article 18.
Article 30 inatueleza the rights provided under the same same constitution are not absolute, they are subject to limitations, they can be taken away in some circumstances, one of those circumstances and which is very complicated one is the issue of public interest.
Wanasiasa wanatumia ujinga wenu wa kutikuijua katiba kuwaaeleza mna haki, lkn hawawaambii kuwa haki hizo zinaenda na wajibu na pia zina miaka take!
Unajua tatizo ni cause of limitations to enjoyment of rights, kwakuwa hakuna clear interpretation of what is/are public interest (s) basi kuwepo na liberty ya kila upande ku enjoy hii b. o. d na kwamba kusiwepo upande wenye kutumia msuli kukandamiza upande mwingine.

Kwa mfano, kwa nini serikali isipeleke hoja hii mahakamani ili ipate ufafanuzi wa kisheria na badala yake inaandaa majeshi kuua waandamanaji?

Au kwanini usiitishwe mdaharo wa kitaifa kujadiri what are the public interests of which the president can intervene in case they are endangered?
 
Mjadala huu ni mzuri sana kama utakua umeuvua uchama au wewe unavyojiona na ulivyo katika nafasi yako.
Kuna watu humu mnatamba kua mko vizuri kwenye sheria na mnapiga hela sasa najiuliza wewe ni mwanasheria au jizi tu!
Wengi mnajikita kwenye haki za binadamu katika kujadiri issue iliyo hot leo lkn sheria ya vyama vingi mnaikacha... Tuongelee katiba na sheria ya vyama vingi... UKUTA sio issue ya HR no..
Hapa ndugu tunaongelea katiba iliyozaa sheria.
Vyama vya siasa na haki zake zipo chini ya haki za jumla kikatiba. Sheria ya vyama vya siasa ni kitabu kingine kabisa ambacho mzazi wake ni katiba.

Hata kama sheria ya vyama vya siasa imetaja kufanya mikutano kwa mujibu wa katiba ibara ya 30(1) mamlaka inaweza kuondoa haki hiyo kwa maslahi ya umma.

Kwahiyo kudai haki ya kufanya mikutano wakati mamlaka imekataa kwa maslahi ya umma ni kuvunja katiba.
 
Mleta mada nadhani huijui Constitution Law au umeisoma hiyo ibara lakini hujaielewa.

Soma ibara hiyo hiyo ya 30 lakini kipengele (2)

(30)
(2)
Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii
ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa
binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia"
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa
mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -
.....
....
...
"

Hiyo Ibara ya (2) Inaelezea kuwa Mambo yote ambayo yanalimit Freedom ambazo zimetolewa na Katiba HII ni LAZIMA YAPATE UHALALI KUTOKA KATIKA SHERIA FULANI ILIYOTUNGWA NA BUNGE . Siyo holela holela tu

Sasa kwa mujibu wa Sheria zetu, Ni Sheria ya Hali ya hatari tu inayoweza kususpend Hizo freedoms.

Kiufupi ni kwamba, Ukiachilia mbali energency law, Hakuna Kifungu cha Katiba kinachompa powers
Raisi Kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya siasa.

Version ya Kiingereza ya Katiba iko very clear, na hii ya Kiingereza ndo huwa inatumika mahakamani
Ndio maana nasema kuwepo mdaharo/makongamano kama ya kigoda cha mwalimu ili watu tukutane ana kwa ana kwenye jambo la katiba hii hii maana kuna misconceptions za wasomaji wengi wa katiba japo ni kosa la mitaala ya elimu zetu kushindwa kuweka somo la katiba kama elimu ya msingi kwa raia.
 
Msisahau kuwa kila wakati inasema bila kukiuka katiba ama katika hali ya emergency siyo wakati wowote. Hatuna vita sasa hivi. Na pia huwezi kuweka sheria kwa ajili ya opposition ukiacha chama tawala. Hakuna sheria ya namna hiyo.
Nadhani tujadili kwa kufikiria je itakuwaje kiatu kikienda katika upande mwingine? Je bado utatetea? Kama jibu ni hapana basi acha kutetea.
 
Soma katiba wewe hakuna sehemu katiba imesema kama hakuna haki uandamane.
Umeshasoma Sheria ya Vyama vya Siasa ambayo inaakisi Katiba unayoi quote hapa? Hizi ni Taaluma za Watu, not every Harry Tom n Dick can read, understand, and give the correct construction of Laws! Ulichofanya hapa ni kubwabwaja tu!
 
Msisahau kuwa kila wakati inasema bila kukiuka katiba ama katika hali ya emergency siyo wakati wowote. Hatuna vita sasa hivi. Na pia huwezi kuweka sheria kwa ajili ya opposition ukiacha chama tawala. Hakuna sheria ya namna hiyo.
Nadhani tujadili kwa kufikiria je itakuwaje kiatu kikienda katika upande mwingine? Je bado utatetea? Kama jibu ni hapana basi acha kutetea.
Hapa hatuongelei vita rafiki. Hapa tunaongelea jinsi haki yako inavyonyima haki wengine.
Kama haki yako inanyima haki wengine kwahiyo mamlaka itaangalia public interest na haki yako itaondolewa ili public ipate haki.
 
Umeshasoma Sheria ya Vyama vya Siasa ambayo inaakisi Katiba unayoi quote hapa? Hizi ni Taaluma za Watu, not every Harry Tom n Dick can read, understand, and give the correct construction of Laws! Ulichofanya hapa ni kubwabwaja tu!
Mbona unakurupuka tu kama umetoka shimoni!!!. Tulia uelewe watu tunajadili nini hapa.
 
Katika ibara zote hizo ulizo taja ambazo ni limitstion of human rights ni kipengele kipi kimetaja chama cha siasa au maandamano au mikutano ya vyama vya siasa? Kitu gani kinaweza kuweka uhalali wa katazo la mikutano ya siasa kutoka na party three? Je kukataza mikutano ya siasa ni sababu tosha yakuwepo amani nchini? Unaweza ukatupa ushahidi mikutano mingapi, lini na wapi hapa Tanzania iliyosababisha vita na kukosekana kwa amani?
 
Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi

31.-(1) Mbali na masharti ya ibara ya 30(2), sheria yoyote
iliyotungwa na Bunge haitakuwa haramu kwa sababu tu kwamba
inawezesha hatua kuchukuliwa wakati wa hali ya hatari, au
wakati wa hali ya kawaida kwa watu wanaoaminika kuwa
wanafanya vitendo vinavyohatarisha au kudhuru usalama wa
taifa, ambazo zinakiuka masharti ya ibara ya 14 na ya 15 za
Katiba hii.
(2) Ni marufuku kwa hatua zilizotajwa katika ibara ndogo ya
(1) ya ibara hii kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria yoyote wakati
wa hali ya hatari, au wakati wa hali ya kawaida kwa mtu yeyote,
isipokuwa tu kwa kiasi ambacho ni lazima na halali kwa ajili ya
kushughulikia hali iliyopo wakati wa hali ya hatari au wakati wa
hali ya kawaida kushughulikia hali iliyosababishwa na mwenendo
wa mtu anayehusika.
(3) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii
hayataidhinisha mtu kunyang'anywa haki yake ya kuwa hai
isipokuwa tu kwa kifo kama matokeo ya vitendo vya kivita.
Unaifahamu Hali ya Hatari? Utaishia ku quote provisions irrelevant to the situation! Pole, Law is not for every Hary Tom n Dick!
 
Mkuu soma vzr nilichokiandika usikurupuke!
Nimesema pamoja na katiba kutoa haki kadhaa ikiwemo kuandamana, lkn pia imetoa limitations, and one of the limitations ni readons of public interest.
Kwamba there are tymes when those rights can be taken away for reasons of public interest, na nikasema bahati mbaya katiba na sheria zingine hazija define what amounts into public interest hivyo kitu hiki kinatoa room kwa watu Ku limit hizo haki ikiwemo haki ya kuandamana kwa muamvuri wa public interest, na ni katiba imetoa loophole hiyo.
Kwahiyo kupiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara inapata baraka chini ya kifungu hicho cha 30(1) mkuu.
It is for public interest, what are they?! No body knows bcoz katiba haisemi wala hakuna sheria inayosema!
Nimekusoma vizuri mkuu ndio maana in contents ume emphasize nilichojibu.
Tuko pamoja hapa kiongozi.
 
Derogation/limitation of human rights.. How is it connected to the rights and freedom of political parties in Tanzania ? Allein
 
Katika ibara zote hizo ulizo taja ambazo ni limitstion of human rights ni kipengele kipi kimetaja chama cha siasa au maandamano au mikutano ya vyama vya siasa? Kitu gani kinaweza kuweka uhalali wa katazo la mikutano ya siasa kutoka na party three? Je kukataza mikutano ya siasa ni sababu tosha yakuwepo amani nchini? Unaweza ukatupa ushahidi mikutano mingapi, lini na wapi hapa Tanzania iliyosababisha vita na kukosekana kwa amani?
Kwa mujibu wa taarifa toka vyombo vya usalama kuna taarifa ya hatari kutokana na mikusanyiko ya kisiasa.
Pili Mambo hayo ya mikusanyiko ya kisiasa yewahi kuathiliwa huko Arusha kutokana na mlipuko wa mabomu.
Matamko ya viongozi wa siasa yanahamasisha uvunjifu wa amani.
Vilevile kulingana na kikao cha juzi cha CUF kimeonesha namna ya vurugu zilivyotokea kwenye vikao vya ndani

Kwa mujibu wa taarifa hizo mamlaka inavizuia vyama vya siasa kutokufanya mikutano ya ndani na nje mpaka mamlaka itakapo toa muongozo. Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ibara ya 30(1) mamlaka inaweza kuondoa haki kwa maslahi ya umma.
 
Rais akiwa kama amiri jeshi mkuu anaweza kutumia vyombo vya ulinzi kulinda nje au ndani si kutokana na vita pekee bali akiona usalama wa raia unaathiliwa au yeye akiona inavyofaa.

Soma tena using'ang'anie kwenye vita wakati katiba imempa uhuru wa kutumia majeshi anavyoona inafaa.
Umemisread hicho kifungu mkuu, ebu ukiwa unasoma weka kituo ili upate comprehensive meaning ya kinachokusudiwa katika maelezo hayo.

Mimi sina ugomvi na mtu hapa nina ugomvi na misinterpretation ya hivi vifungu vya katiba, pale ambapo vinaonekana kukinzana vyenyewe kwa vyenyewe ndipo mkanganyiko wa msomaji unapotokea.

Napendekeza mdaharo wa wazi wa katiba hii iliyopo kabla hata ya hiyo pendekezwa au ya warioba.
 
Derogation/limitation of human rights.. How is it connected to the rights and freedom of political parties in Tanzania ? Allein
Hebu niambie ibara ipi kwenye katiba inaongelea haki ya vyama vya siasa?
 
Back
Top Bottom