Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

kajost: 17350864 said:
Mkuu Lissu anatumia advantage ya watu kama hawa ambao hawajawahi kuiona hata katiba inafananaje.

Lissu ni wa kawaida sana, kwa wale tunaoshinda mahakamani tunajua, Nchi hii kuna vichwa vingi tu Sema kinachompa kiki jamaa ni kwa vile ni mwanasiasa hivo kila anachofanya kinakuwa kwenye media, akiweka P.O watu wanajua, akishinda P.O watu wanajua, lkn kuna vichwa vipo na vinapiga hela kimya kimya!
Back on our Constitution, ni kwamba Lissu anawaeleza wanaukuta kuhusu haki zinazoelezwa on the bill of rights under part3, lkn hawawaelezi kuhusu limitations on the given rights ambazo the same constitution imeweka.
Kwa ufupi katiba hii inakupa haki upande mmoja na inakunyanganya kupitia upande wa pili.kwa mfano haki xote zilizoolozeshwa zinaweza kunyanganywa kwa sababu ya maslahi ya umma, ukifatilia vzr katiba hii haijadefine nini maana ya maslahi ya umma, yaani ni vitu vp vinakuwa counted as amounting into public interest.Hata mahakama hadi Leo hazijaweza kutoa msimamo wa nini hasa ni maslahi ya umma.

Kwa maana hiyo Rais anaweza kutumia kipengere hicho kuamua anavoona yeye na akasema ni kwa maslahi ya umma, mfano aliposema huu ni mda wa kutekelexa ahadi, anaweza akaidefine hiyo kama maslahi ya umma.
Lissu analijua hilo, na ukweli Rais anatumia katiba, hivyo kupambana na Rais badala ya kupambana na katiba inayompa na kutoa loopholes hizo wao wanapambana na matokeo yake! Wengi tulitegemea wangeenda mahakamani ili wapate nini msimamo wa mahakama, then tuone kama Rais ataenda kinyume na maamuz ya mahakama.
Katiba imetoa room ya mtu anayedhani haki hizo under part3 zimekiukwa aende mahakaman, cha ajabu nguli huyu wa sheria badala ya kuwaongoza wenzake kwenda mahakamani anahamisisha watu waandane.

Ikumbukwe utawala wa sheria si kwa upande wa serikali tu, hata ss raia inatuhusu.
Kwanini wasiende mahakamani kama katiba inavoelekeza badala yake wanaamua kuandaa maandamano, hapa ndipo unapoiona illmotives!
Ikumbukwe sheria ya vyama vya siasa haiwezi kuwa juu ya katiba, kama katiba imeweka limitations on the enjoyment of the provided rights under part 3, sheria nyingine haiwezi kutoa free enjoyment of the same rights!

Anyway haya mambo ni magumu ndo maana wengi wataishia kukutukana tu, na kutoa comment zisizo kuwa na vichwa wala miguu!
Aksante kwa elimu, mkuu.
 
Kinachofanywa na serikali kwasasa ni kujipindua .... A coup de tat against itself..
 
Soma preamble mkuu kwanza alafu tuendelee.. Ingawa umekataa kunijibu ila mimi nitakujibu
 
Kinachofanywa na serikali kwasasa ni kujipindua .... A coup de tat against itself..
Sasa umeenda nje ya mada sasa kwanini usiongelee jambo lililo mezani?
 
Soma preamble mkuu kwanza alafu tuendelee.. Ingawa umekataa kunijibu ila mimi nitakujibu
Labda rafiki unataka nikujibu utakavyo. Je unataka nikujibuje?
 
Uzi wako umedoda yaani saa mzima hakuna wachangiaji? Hovyo kabisa
Tatizo ni ku digest hivyo vifungu na kujenga hoja, kwa sababu wabongo wengi hawajazoea kuumiza vichwa, we nenda huko insta na facebook ukaone walivyojazana kwenye issue za udaku😀😀
 
Ibara ya 30 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inaongelea mipaka kwa Haki na Uhuru.
Chadema wanakuwa wanaongea sana huku Katiba ikiwaumbua wazi wazi.

Tuanze sasa:-

30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake
imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja
kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa
kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii
ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa
binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa
mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -

(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine
au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi
mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;
(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika
jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya
maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya
madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi
mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya
umma;
(c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya
mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai
au la jinai;
(d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine au
maisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri
mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunza
heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;
(e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji,
uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika ya
watu binafsi nchini; au

(f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo
linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.

(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii
ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au
wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na
mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza
kufungua shauri katika Mahakama Kuu.
Unajua mm baada ya kusoma hii nikajua leo weekend mkuu, nikajua umechangamka tu manake weekend si padlock karuhusu kuanza hata saa tatuuu....manake si kweli kwamba haujaelewa hicho kifungu hapo
 
Unajua mm baada ya kusoma hii nikajua leo weekend mkuu, nikajua umechangamka tu manake weekend si padlock karuhusu kuanza hata saa tatuuu....manake si kweli kwamba haujaelewa hicho kifungu hapo
Sasa hapa unataka kusema nini?
 
Unajua tatizo ni cause of limitations to enjoyment of rights, kwakuwa hakuna clear interpretation of what is/are public interest (s) basi kuwepo na liberty ya kila upande ku enjoy hii b. o. d na kwamba kusiwepo upande wenye kutumia msuli kukandamiza upande mwingine.

Kwa mfano, kwa nini serikali isipeleke hoja hii mahakamani ili ipate ufafanuzi wa kisheria na badala yake inaandaa majeshi kuua waandamanaji?

Au kwanini usiitishwe mdaharo wa kitaifa kujadiri what are the public interests of which the president can intervene in case they are endangered?
Laws are made to save the interest of the ruling class, katiba iliyopo inawafavour waliopo madarakani.
Ww unayehisi unakubinya ndo unatakiwa uende mahakamani. Ndo maana nasema UKUTA ni mkakati ambao wahusika wanafight against the wrong enemy!
Kama Rais ametoa kauli kinyume na katiba aliyoapa kuilinda kwanini wasiende mahakamani!? Katiba imeweka wazi kabisa kama unadhani katiba imevunjwa go the Court!
Badala yake wanapambana na matokeo ya katiba badala ya kupambana na katiba!
Katika ibara zote hizo ulizo taja ambazo ni limitstion of human rights ni kipengele kipi kimetaja chama cha siasa au maandamano au mikutano ya vyama vya siasa? Kitu gani kinaweza kuweka uhalali wa katazo la mikutano ya siasa kutoka na party three? Je kukataza mikutano ya siasa ni sababu tosha yakuwepo amani nchini? Unaweza ukatupa ushahidi mikutano mingapi, lini na wapi hapa Tanzania iliyosababisha vita na kukosekana kwa amani?
Mkuu ibara ya 18 inatoa right of association, japo ndipo msingi wa kuwepo vyama unapokuja,sheria ya vyama vya siasa inakuja kukazia ibara hiyo.
Kwa lugha nyingine sheria ya vyama vya siasa ni tawi la ibara hiyo, hivyo basi lazima izingatie matakwa ya katiba, sasa katiba kwenye ibara ya 30 inaweka limitations za kuenjoy hizo haki ikiwemo ibara ya 18 ambao ndipo mzizi wa sheria ya vyama vya siasa.
Kumbuka kunapotokea kukinzana kati ya katiba na sheria ya kawaida basi katiba inasimama, kwa maana hiyo haki ya kuandamana na kufanya mikutano kama ilivyowekwa ktk ibara ya 18 INA miaka take!
 
Katiba ya JMT inatambua mfumo wa vyama vingi tangu mosi july 1992.. Katiba hii inarejerea kuwepo hivi vyama pamoja na haki na wajibu wa vyama vya siasa.. Sheria nno4 na 5. Pia 2007 yapo marekebisho ambayo yaliongeza maadili ya vyama vya siasa. Je sheria hii ni haramu?
Inakuaje mchuano unakua baina ya CCM na CHADEMA wakati CCM ni chama kama vingine na UKUTA sio kua inaipinga CCM bali inaipinga dola?
Mawaziri wanapoenda kwenye ziara awafanyi mikutano ambayo pia ni mikusanyiko ya kisiasa na huku wanavalia sale za ccm?
Mikutano ya kampeini aikuweza kuleta vita na ata uliyo itaja sikusikia rais anatangaza hali ya hatari.
Jmn tusiaibishe au kuvisaliti vyeti vyetu na madarasa tuliopitia
 
Serikali pamoja na Rais wameapa kuilinda Katiba.Hivi ukiwapa Haki CDM ya kisheria ya kuandamna na kufanya mikutano wanapoteza nini??Wa kwanza kujishtaki ni Rais na Serikali yake ifuate Sheria na Katiba waliyoaapa kuilinda Mengine ni blahblah.
 
Madaraka ya Pekee ya Mamlaka ya Nchi


31.-(1) Mbali na masharti ya ibara ya 30(2), sheria yoyote
iliyotungwa na Bunge haitakuwa haramu kwa sababu tu kwamba
inawezesha hatua kuchukuliwa wakati wa hali ya hatari, au
wakati wa hali ya kawaida kwa watu wanaoaminika kuwa
wanafanya vitendo vinavyohatarisha au kudhuru usalama wa
taifa, ambazo zinakiuka masharti ya ibara ya 14 na ya 15 za
Katiba hii.
(2) Ni marufuku kwa hatua zilizotajwa katika ibara ndogo ya
(1) ya ibara hii kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria yoyote wakati
wa hali ya hatari, au wakati wa hali ya kawaida kwa mtu yeyote,
isipokuwa tu kwa kiasi ambacho ni lazima na halali kwa ajili ya
kushughulikia hali iliyopo wakati wa hali ya hatari au wakati wa
hali ya kawaida kushughulikia hali iliyosababishwa na mwenendo
wa mtu anayehusika.
(3) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii
hayataidhinisha mtu kunyang'anywa haki yake ya kuwa hai
isipokuwa tu kwa kifo kama matokeo ya vitendo vya kivita.
Kwani imetangazwa hali ya hatari! Upuuzi mtupu tuwe wakweli siyo kwa sababu ni wanachama wa kijana basi hata maovu tuyapigie makofi
 
Hoja ya msingi hapa ni kwamba ukiona haki zako zinavunjwa,kimbilio pekee ni mahakamani.siyo na wewe uvunje utaratibu na haki kwa kufanya yaliyokatazwa kwa amri halali.
 
Hoja ya msingi hapa ni kwamba ukiona haki zako zinavunjwa,kimbilio pekee ni mahakamani.siyo na wewe uvunje utaratibu na haki kwa kufanya yaliyokatazwa kwa amri halali.
Hapa hakuna hata mmoja anayeweza kutia timu.
Hawa jamaa wanawadanganya wananchi. Na jinsi sisi wa TZ tusivyopenda kusoma yaani tutaamini yale aliyosema Lisu
 
Mbona wewe upo hapa?
Wewe Tulia kunywa uji..umejichanganya mwenyewe .. Hakuna kitu..wala huelewi kilichoandikwaaa..kwa hiyo Marais woteee hawa kuona hayo Leo Hii ndo nyiee mmeona..VP kuhusu Jamhuri kuingilia mamlaka za Bungee.Ebu niambie Ni wapi Budget ya Bunge inarudishwa serikali ni bila kuidhinishwa popote..na wapi Naibu spika anateuliwa kwa shinikizo...Wapi Rais anatamka maneno kesho MTU mwingine anamsemea Eti hakusema na Ni utani..Implications zake unazijua Rais anapotamka kitu..Rudi Darasani..ungekuwa mwema ungeleta na ile inayosema hakuna aliye juu ya sheria..au wee unaona yoote afanyayo Ni sawa asiwepo MTU wa kumshauri..Poor you .
 
Wewe Tulia kunywa uji..umejichanganya mwenyewe .. Hakuna kitu..wala huelewi kilichoandikwaaa..kwa hiyo Marais woteee hawa kuona hayo Leo Hii ndo nyiee mmeona..VP kuhusu Jamhuri kuingilia mamlaka za Bungee.Ebu niambie Ni wapi Budget ya Bunge inarudishwa serikali ni bila kuidhinishwa popote..na wapi Naibu spika anateuliwa kwa shinikizo...Wapi Rais anatamka maneno kesho MTU mwingine anamsemea Eti hakusema na Ni utani..Implications zake unazijua Rais anapotamka kitu..Rudi Darasani..ungekuwa mwema ungeleta na ile inayosema hakuna aliye juu ya sheria..au wee unaona yoote afanyayo Ni sawa asiwepo MTU wa kumshauri..Poor you .
Hapa inahusiana na nini kwenye thread hii?
 
Mamlaka ya Rais

148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.
Elimu wameipata vyema
 
Hapa inahusiana na nini kwenye thread hii?
Unaona ulivyo mweupe kichwani...kwa hiyoo Mpaka Leo Hii hujui Katibu ndo inayotuongoza kutenda mambo na sio yanayotoka kichwani tu..sijibizani na wewe tena ngoja nikuache na akina BAK
 
Back
Top Bottom