Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

angalau kwa kuweka vifungu hivi vya katiba na sheria mtoa mada umepanua mjadala na uwe fikirishi. naomba wataalamu wa sheria waje hapa kutufafanulia vifungu hivi. kama hujui sheria na tafsiri zake kaa pembeni. ushabiki wa vyama wekeni pembeni kwanza....
 
Bwana mkubwa hiyo ni sheria ya kawaida( principle regislation) ambayo inapata uhalali wake kutoka kwenye katiba( mother law).

Hivyo chochote kilichomo humo lazima kiathiriwe na kile kilichomo ndani ya katiba. Hivyo kama Article 30 inaweza Ku limit basic rights zilizopo kwenye katiba hasa part3, inashindwa Ku limit hii sheria uliyiweka hapa!

Kumbuka sheria huwez kuisoma kirahisi kama ulivofanya ww, sheria husomwa subject to constitution and other laws. Huwez kuchukua sheria moja ukasema imesema hv basi tayari, huo ndo upotoshaji tunaousema!
 
Hapa ni elimu tu. Ili mkipata mkong'oto msisingizie katiba kuvunjwa.
Acha kujaza servers za JF kwa kupaste katiba humu bila hata kutetea uamuzi wa serikali yako kuipinga hiyo katiba
 
Toa maelezo kikatiba katiba imepingwa kivipi?
 
"Miongoni mwa mamlaka ya rais akiwa amiri jeshi mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa jamhuri ya muungano"

Ndugu una ugomvi na tafsiri ya maandiko! Kwa mfano anapopiga marufuku mikutano ya kisiasa je ni moja ya mamlaka yake kwa mujibu wa kifungu hiki?!
 
Bro, claw back clause ndo kama hizo alizokutajia mleta Mada, mfano Article 30, hiyo ni claw back clause, ambayo imeweka limitations on the enjoyment of the rights provided under part 3, mbona Lissu hawambii hili, anawaambia tu mna haki, hawaambii kama mnawajibu pia!
Unachopigania Wewe ni nn?
 
A
"Miongoni mwa mamlaka ya rais akiwa amiri jeshi mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa jamhuri ya muungano"

Ndugu una ugomvi na tafsiri ya maandiko! Kwa mfano anapopiga marufuku mikutano ya kisiasa je ni moja ya mamlaka yake kwa mujibu wa kifungu hiki?!
cha kusoma kamstari kamoja tu kwa ajiri ya kujifurahisha. Soma kipengere chote hapa:-

148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.
 
Soma katiba wewe hakuna sehemu katiba imesema kama hakuna haki uandamane.
ndugu umekosea kusema hakuna sehemu kwenye katiba inayosema kuandamana, hiyo sehemu ipo we nenda kwenye sura ya pili vyama siasa utaona wamezungumzia hadi mikutano ya hadhara
 
A

cha kusoma kamstari kamoja tu kwa ajiri ya kujifurahisha. Soma kipengere chote hapa:-

148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.

Bila kuathiri.....
hiyo phrase ni ya msingi sana.
 
Mimi naona mtoa post ndo mara yake ya kwanza kuisoma katiba kwa hy alipoona hapo tena bila kujua tafsiri ya kisheria akakimbilia Jf. Soma tena alafu urudi humu
Leta Kifungu chako ambacho si mara ya kwanza kukisoma
 
ndugu umekosea kusema hakuna sehemu kwenye katiba inayosema kuandamana, hiyo sehemu ipo we nenda kwenye sura ya pili vyama siasa utaona wamezungumzia hadi mikutano ya hadhara
Huyu Annael ni UVCCM mwenye kiwango cha chini cha uelewa lakini ila mwenye kiwango cha juu cha ushabiki na aliyejaa propaganda mfu. Usihangaike naye, atakupotezea malengo yako buree
 
ndugu umekosea kusema hakuna sehemu kwenye katiba inayosema kuandamana, hiyo sehemu ipo we nenda kwenye sura ya pili vyama siasa utaona wamezungumzia hadi mikutano ya hadhara
Hapa tunaongelea katiba wewe unasema Sheria ya vyama vya siasa. Katiba ndio sheria mama. Sheria mama inasema kama hujaridhika nenda mahakama kuu.

Na tayari mahakama kuu imetolewa ufafanuzi kupitia sheria za police. Kwamba:-
Kwenye sheria ya police kifungu 43 kuhusu maandamano

(6) Mtu yeyote ambaye hajaridhika na masharti ya amri ya
kusimamisha iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (3) au, amri yoyote iliyotolewa na afisa polisi chini ya kifungu kidogo cha (4), anaweza kukata rufaa kwa Waziri ambaye maamuzi yake yatakuwa ya mwisho.

Kwamba mnatakiwa kwenda kuwashitaki police kwa waziri wa Mambo ya Ndani(Mwigulu Nchemba) huenda akawaruhusu muandamane
 
Kuandamana haki yao lkn wataingilia haki za watu wengine wanaotumia huduma za jamii kama barabara
 
Hapa tunaongelea katiba wewe unasema Sheria ya vyama vya siasa. Katiba ndio sheria mama. Sheria mama inasema kama hujaridhika nenda mahakama kuu.

Na tayari mahakama kuu imetolewa ufafanuzi kupitia sheria za police. Kwamba:-
Kwenye sheria ya police kifungu 43 kuhusu maandamano

(6) Mtu yeyote ambaye hajaridhika na masharti ya amri ya
kusimamisha iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (3) au, amri yoyote iliyotolewa na afisa polisi chini ya kifungu kidogo cha (4), anaweza kukata rufaa kwa Waziri ambaye maamuzi yake yatakuwa ya mwisho.

Kwamba mnatakiwa kwenda kuwashitaki police kwa waziri wa Mambo ya Ndani(Mwigulu Nchemba) huenda akawaruhusu muandamane
kessi ya tumbili unampelekea ngedele, unadhani nini matokeo yake? hata hivyo tusome kipengele cha vyama vya siasa tu ambavyo ndo vimetufikisha kwenye mivutano
 
Back
Top Bottom