Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Naona hapa unajiumbua kweli. Hebu tumia kichwa kufikilia kidogo hapo peandikwaje!???

Sheria zitatungwa tu kutetea haki za watu.
Lakini yakija msuala ya public interest mamlaka inaondoa haki hiyo.

Huyu Bisimba anawadanganya na issue zake za haki za binadamu. Likija swala la public interest hakuna haki hizo.

Yanaondolewa kwa Sheria maalum, Ambayo ni Emergency Law, Kama Wanataka kususpend hizo Rights basi Watangaze hali ya hatari, tujue moja

Au wakatunge sheria nyingine ya kuwapa leeway ya kufanya wayatakayo, otherwise wanafanya kibabe tu na si kwa mujibu wa sheria.
 
Naona hapa unajiumbua kweli. Hebu tumia kichwa kufikilia kidogo hapo peandikwaje!???

Sheria zitatungwa tu kutetea haki za watu.
Lakini yakija msuala ya public interest mamlaka inaondoa haki hiyo.

Huyu Bisimba anawadanganya na issue zake za haki za binadamu. Likija swala la public interest hakuna haki hizo.
Kufikilia=Kufikiria, peandikwaje=pameandikwa je? Narudia tena kajifunze kiswahili na uandishi
 
Hapa ni elimu tu. Ili mkipata mkong'oto msisingizie katiba kuvunjwa.
Na bila polisi ninyi hamuwezi kitu
Ibara ya 30 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inaongelea mipaka kwa Haki na Uhuru.
Chadema wanakuwa wanaongea sana huku Katiba ikiwaumbua wazi wazi.

Tuanze sasa:-

30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake
imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja
kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa
kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii
ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa
binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa
mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -

(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine
au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi
mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;
(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika
jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya
maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya
madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi
mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya
umma;
(c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya
mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai
au la jinai;
(d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine au
maisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri
mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunza
heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;
(e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji,
uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika ya
watu binafsi nchini; au

(f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo
linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.

(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii
ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au
wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na
mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza
kufungua shauri katika Mahakama Kuu.

Hapo kwenye bold.
 
Mkuu Lissu anatumia advantage ya watu kama hawa ambao hawajawahi kuiona hata katiba inafananaje.

Lissu ni wa kawaida sana, kwa wale tunaoshinda mahakamani tunajua, Nchi hii kuna vichwa vingi tu Sema kinachompa kiki jamaa ni kwa vile ni mwanasiasa hivo kila anachofanya kinakuwa kwenye media, akiweka P.O watu wanajua, akishinda P.O watu wanajua, lkn kuna vichwa vipo na vinapiga hela kimya kimya!
Back on our Constitution, ni kwamba Lissu anawaeleza wanaukuta kuhusu haki zinazoelezwa on the bill of rights under part3, lkn hawawaelezi kuhusu limitations on the given rights ambazo the same constitution imeweka.
Kwa ufupi katiba hii inakupa haki upande mmoja na inakunyanganya kupitia upande wa pili.kwa mfano haki xote zilizoolozeshwa zinaweza kunyanganywa kwa sababu ya maslahi ya umma, ukifatilia vzr katiba hii haijadefine nini maana ya maslahi ya umma, yaani ni vitu vp vinakuwa counted as amounting into public interest.Hata mahakama hadi Leo hazijaweza kutoa msimamo wa nini hasa ni maslahi ya umma.

Kwa maana hiyo Rais anaweza kutumia kipengere hicho kuamua anavoona yeye na akasema ni kwa maslahi ya umma, mfano aliposema huu ni mda wa kutekelexa ahadi, anaweza akaidefine hiyo kama maslahi ya umma.
Lissu analijua hilo, na ukweli Rais anatumia katiba, hivyo kupambana na Rais badala ya kupambana na katiba inayompa na kutoa loopholes hizo wao wanapambana na matokeo yake! Wengi tulitegemea wangeenda mahakamani ili wapate nini msimamo wa mahakama, then tuone kama Rais ataenda kinyume na maamuz ya mahakama.
Katiba imetoa room ya mtu anayedhani haki hizo under part3 zimekiukwa aende mahakaman, cha ajabu nguli huyu wa sheria badala ya kuwaongoza wenzake kwenda mahakamani anahamisisha watu waandane.

Ikumbukwe utawala wa sheria si kwa upande wa serikali tu, hata ss raia inatuhusu.
Kwanini wasiende mahakamani kama katiba inavoelekeza badala yake wanaamua kuandaa maandamano, hapa ndipo unapoiona illmotives!
Ikumbukwe sheria ya vyama vya siasa haiwezi kuwa juu ya katiba, kama katiba imeweka limitations on the enjoyment of the provided rights under part 3, sheria nyingine haiwezi kutoa free enjoyment of the same rights!

Anyway haya mambo ni magumu ndo maana wengi wataishia kukutukana tu, na kutoa comment zisizo kuwa na vichwa wala miguu!
We mwenyewe una kili mambo haya magum kwa nini ujiingize kwenye mambo magum, waachie wenyewe, au na wewe unataka kuwa mwanasheria wa JF
 
Yanaondolewa kwa Sheria maalum, Ambayo ni Emergency Law, Kama Wanataka kususpend hizo Rights basi Watangaze hali ya hatari, tujue moja
Ujue rafiki hapa tunaongelea katiba sawa?
Ni kifungu kipi cha katiba kinaongelea hiyo emergency law? Hebu rudia vizuri ukiwa umetulia kisoma ibara ya 30(1).
Nakuomba usome kwa utulivu tu.

Halafu usiingize kitu ambacho ni nje ya katiba.
Uhuru na haki inaisha yakija maslahi ya umma.
 
Mleta mada nadhani huijui Constitution Law au umeisoma hiyo ibara lakini hujaielewa.

Soma ibara hiyo hiyo ya 30 lakini kipengele (2)

(30)
(2)
Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii
ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa
binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia"
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa
mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -
.....
....
...
"

Hiyo Ibara ya (2) Inaelezea kuwa Mambo yote ambayo yanalimit Freedom ambazo zimetolewa na Katiba HII ni LAZIMA YAPATE UHALALI KUTOKA KATIKA SHERIA FULANI ILIYOTUNGWA NA BUNGE . Siyo holela holela tu

Sasa kwa mujibu wa Sheria zetu, Ni Sheria ya Hali ya hatari tu inayoweza kususpend Hizo freedoms.

Kiufupi ni kwamba, Ukiachilia mbali energency law, Hakuna Kifungu cha Katiba kinachompa powers
Raisi Kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya siasa.

Version ya Kiingereza ya Katiba iko very clear, na hii ya Kiingereza ndo huwa inatumika mahakamani

Vitu kama huvielewi bora ukakaa kimya, Article 30(2) inaweka mkazo kwamba haki na wajibu zinazoainishwa on the bill of rights under part 3, hazitaathiri sheria zilizopo au zitakazotungwa kwa malengo kama yanavotajwa from sub paragraphy a to f,na hayo mambo mengi ukiyasoma yanaonyesha kuwa haki hizo zilizoolozeshwa hapo part3 siyo absolute bali, zinaapply subject to certain limitations! Mfano wa maxingira ambao limitations hizo zaweza wekwa ni kwa mambo yaliyotajwa kuanxia subparagraphy a to f!
 
Ujui sheria asee eti hapo palipoboldiwa rudi shule coz unakoelekea utakuwa katibu wa vilaza
 
Mkuu Lissu anatumia advantage ya watu kama hawa ambao hawajawahi kuiona hata katiba inafananaje.

Lissu ni wa kawaida sana, kwa wale tunaoshinda mahakamani tunajua, Nchi hii kuna vichwa vingi tu Sema kinachompa kiki jamaa ni kwa vile ni mwanasiasa hivo kila anachofanya kinakuwa kwenye media, akiweka P.O watu wanajua, akishinda P.O watu wanajua, lkn kuna vichwa vipo na vinapiga hela kimya kimya!
Back on our Constitution, ni kwamba Lissu anawaeleza wanaukuta kuhusu haki zinazoelezwa on the bill of rights under part3, lkn hawawaelezi kuhusu limitations on the given rights ambazo the same constitution imeweka.
Kwa ufupi katiba hii inakupa haki upande mmoja na inakunyanganya kupitia upande wa pili.kwa mfano haki xote zilizoolozeshwa zinaweza kunyanganywa kwa sababu ya maslahi ya umma, ukifatilia vzr katiba hii haijadefine nini maana ya maslahi ya umma, yaani ni vitu vp vinakuwa counted as amounting into public interest.Hata mahakama hadi Leo hazijaweza kutoa msimamo wa nini hasa ni maslahi ya umma.

Kwa maana hiyo Rais anaweza kutumia kipengere hicho kuamua anavoona yeye na akasema ni kwa maslahi ya umma, mfano aliposema huu ni mda wa kutekelexa ahadi, anaweza akaidefine hiyo kama maslahi ya umma.
Lissu analijua hilo, na ukweli Rais anatumia katiba, hivyo kupambana na Rais badala ya kupambana na katiba inayompa na kutoa loopholes hizo wao wanapambana na matokeo yake! Wengi tulitegemea wangeenda mahakamani ili wapate nini msimamo wa mahakama, then tuone kama Rais ataenda kinyume na maamuz ya mahakama.
Katiba imetoa room ya mtu anayedhani haki hizo under part3 zimekiukwa aende mahakaman, cha ajabu nguli huyu wa sheria badala ya kuwaongoza wenzake kwenda mahakamani anahamisisha watu waandane.

Ikumbukwe utawala wa sheria si kwa upande wa serikali tu, hata ss raia inatuhusu.
Kwanini wasiende mahakamani kama katiba inavoelekeza badala yake wanaamua kuandaa maandamano, hapa ndipo unapoiona illmotives!
Ikumbukwe sheria ya vyama vya siasa haiwezi kuwa juu ya katiba, kama katiba imeweka limitations on the enjoyment of the provided rights under part 3, sheria nyingine haiwezi kutoa free enjoyment of the same rights!

Anyway haya mambo ni magumu ndo maana wengi wataishia kukutukana tu, na kutoa comment zisizo kuwa na vichwa wala miguu!
Umenena vyema mkuu. Ila umesahau kuwa kuna njia nyingi za ku lodge case mahakamani ikiwemo ya kumfanya defendant wako kuwa complainant.
Kwa hiyo Ukuta una create case of public interest with curiosity, hii itazifanya mahakama zetu ku act promptly katika kutoa maamuzi yenye tafsiri ya vifungu vya katiba yetu
 
Ujui sheria asee eti hapo palipoboldiwa rudi shule coz unakoelekea utakuwa katibu wa ******
Kwani mimi nimekwambia najua sheria? Wewe unayejua tutoe tongotongo sisi ambao hatujui. Hebu fafanua basi ili tujue.
 
We mwenyewe una kili mambo haya magum kwa nini ujiingize kwenye mambo magum, waachie wenyewe, au na wewe unataka kuwa mwanasheria wa JF
Ni mambo magumu kwa watu kama nyie ndo mnaishia kutukana na kucomment ujinga.
Soma nilichokiandika hapo juu, Nina uhakika unaona maluwe luwe tu. Mtoa Mazda kaweka hapo vifungu vya katiba changia hapo kama nilivofanya au jibu nilichokiandika!
Ukweli umeshindwa ndo maana unajaribu kuni attack badala ya kujenga hoja based on the thread!
 
Ibara ya 30 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inaongelea mipaka kwa Haki na Uhuru.
Chadema wanakuwa wanaongea sana huku Katiba ikiwaumbua wazi wazi.

Tuanze sasa:-

30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake
imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja
kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa
kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii
ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa
binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa
mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -

(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine
au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi
mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;
(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika
jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya
maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya
madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi
mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya
umma;
(c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya
mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai
au la jinai;
(d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine au
maisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri
mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunza
heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;
(e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji,
uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika ya
watu binafsi nchini; au

(f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo
linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.

(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii
ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au
wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na
mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza
kufungua shauri katika Mahakama Kuu.

Hapo kwenye bold.
Ndugu yangu, vifungu ulivyoleta vinambana anaeingilia uhuru wa wengine kufanya siasa.Labda utuonyeshe CDM wanaumbukaje, kwani mpaka hapa vinawatetea dhidi ya huyo anaekwamisha haki na uhuru wao wa kufanya siasa.
 
Vitu kama huvielewi bora ukakaa kimya, Article 30(2) inaweka mkazo kwamba haki na wajibu zinazoainishwa on the bill of rights under part 3, hazitaathiri sheria zilizopo au zitakazotungwa kwa malengo kama yanavotajwa from sub paragraphy a to f,na hayo mambo mengi ukiyasoma yanaonyesha kuwa haki hizo zilizoolozeshwa hapo part3 siyo absolute bali, zinaapply subject to certain limitations! Mfano wa maxingira ambao limitations hizo zaweza wekwa ni kwa mambo yaliyotajwa kuanxia subparagraphy a to f!

Hebu tafuta mtu akufundishe sheria, naona unavamia vitu usivyovijua.

Hicho kifungu kinasema wazi kuwa vitu vyote " subsequent" ni lazima vifanyike katika context ya sheria kama kuna ulazima wa kuvifanya, either sheria hizo ziwe the existing ones or the ones to be made in the future.

Sasa kwa sasa only emergency Laws ndizo zinazoweza kususpend Hizo rights, Lakini siyo Kwa Matakwa ya Bwana Mkubwa anavyojisikia yeye!.

Someni sheria, msidandie vitu msivyovijua
 
Hapa ni elimu tu. Ili mkipata mkong'oto msisingizie katiba kuvunjwa.

Kama sifa ni mkong'oto umeleta vifungu vya katiba vya nini? Wewe sema tutatoa mkong'oto basi. Yaani katiba ya nchi wanaccm huwa mnaisoma nyuma ya migombo vya vyombo vya dola. Kama kweli mnasimamia katiba kwanini mjivunie jeshi la polisi na sio mahakama ili itafsiri sheria?
 
Kwani mimi nimekwambia najua sheria? Wewe unayejua tutoe tongotongo sisi ambao hatujui. Hebu fafanua basi ili tujue.
Kama ujui ungeomba ushauri na sio kuja na full concluded thread afu utegemee tuje kukutoa tongotongo ishi nazo siku ukitumbukia tutakuja wanasheria tukutoe afu utulipe kwa ukilaza wako haahhahahahaha ila usipaniki ndugu ntakutoa tongo tongo ukiwa serious kukiri umekosea
 
Serikali si ina wanasheria kwani hawajui hivi vifungu? Vingekua vinaweza kubeba mantiki isingetoka kauli ya kulazimisha wangekubal wakashindanie mahakamani ikiwa wapo kimya hii ina maana hv sio ishu
 
Back
Top Bottom