Were acha ubishi, haki ya kufanya mikutano na maandamano inatokana na ibara ya 18 Isome vzr uielewe, sheria ya vyama vya siasa inafafanua pamoja na mambo mengine matakwa ya ibara ya 18.Wapi ktk katiba mamlaka hizo zimepata uwezo wa kuzuia shughuli za vyama vya siasa?
Ni mpaka itokee hali ya dharula ambayo ni vita,mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza kwa wakati mmoja na nk.Tena kwa idhini ya bunge ndipo rais wa jamuhuri ataweza kuzuia shughuli za kisiasa na ni kila baada ya miezi 3 ataomba Tena kibali cha bunge .Nakama bunge likiona hamna haja. Basi haruhusiwi kutangaza hali ya hatari.
Kwahiyo hivyo vipengele ulivyotoa havioneshi wapi mamlaka hizo zinapewa uwezo wa kuzuia shughuli za vyama vya siasa.
Mh hivyo vifungu ndio vinatoa uhalali wa mamlaka fulani kuzuia shughuli za kisiasa?
Mi naona hatutaelewana kwani mwenzangu unahasira mpaka unanitukana.
Ukweli unabaki palepale kuwa hujaonesha hicho kifungu .
Heri umekuwa mkweli kuliko kumshambulia mtu mwenye ufahamu wa sheria anapotaka kuwaeleza ukweli na mkang'ang'ania kwa kwaajili tu mpo upande wa CDM ama CCM. Lissu ni mwanasheria lakini pia ni mwanasiasa anatumia kipaji chake cha uanasiasa zaidi ya taaluma yake. Huyu ni sawa na wachungaji na ma sheikh wanaoendesha dini kwa maslahi yao kwa kutumia vipengele katika Biblia ama Korani ambavyo vitawashawishi waumini wao bila kutaja vipengele ambavyo vitaelezea zaidi madhara ya matendo watakayoyafanya.ni kweli unachosema, mungu ampe hekima na busara ili asitumie madaraka yake vibaya kwani anaweza kulitumbukiza taifa kwenye matatizo kwa chuki ambayo inaweza dumu kwa muda mrefu kwa wananchi wenye itikadi tofauti na asione matumizi ya vyombo vya dola kama polisi ni suluhisho bora sana kuzidi mazungumzo ya kupeana elimu. sio jambo zuri kuingia vitani na wananchi wako
Heri umekuwa mkweli kuliko kumshambulia mtu mwenye ufahamu wa sheria anapotaka kuwaeleza ukweli na mkang'ang'ania kwa kwaajili tu mpo upande wa CDM ama CCM. Lissu ni mwanasheria lakini pia ni mwanasiasa anatumia kipaji chake cha uanasiasa zaidi ya taaluma yake. Huyu ni sawa na wachungaji na ma sheikh wanaoendesha dini kwa maslahi yao kwa kutumia vipengele katika Biblia ama Korani ambavyo vitawashawishi waumini wao bila kutaja vipengele ambavyo vitaelezea zaidi madhara ya matendo watakayoyafanya.
Yeye anajiona anajuaaa kuliko woote..na kwa nini akazanie Ibara iyo ya 30(1)ambayo nayo inamfunga..Njaa mbaya sanaAcha kujidharirisha... Gusa sheria ya vyama vya siasa 4 na 5 alafu utuambie niwapi rais aamepewa mamlaka ya kukataza vyama vya siasa kufanya mikutano? Ilo ndo jambo la msingi
Mwalimu nyerere aliwahi kusema Àkiwa kwenye sherehe za mei mosi mjini Mbeya kuhusu hatari viongozi kuruhusiwa kuanza kunyofoa haki za kiraia, hivi tatizo liko wapi? Mbona haki ya vyama vya siasa zimekuwepo kwa zaidi ya miaka 20 sasa bila tatizo hivi tukipora haki za kiraia ndio tutapata maendeleo? haki zetu zitaondoka moja baada ya nyingine mwisho zitakuhusu pia wewe unaedhani uko mbali. Siungi Mkono maandamano lakini pia siungi Mkono upolaji wa haki za kilaia kwa kisingizio chochote kileMkuu Lissu anatumia advantage ya watu kama hawa ambao hawajawahi kuiona hata katiba inafananaje.
Lissu ni wa kawaida sana, kwa wale tunaoshinda mahakamani tunajua, Nchi hii kuna vichwa vingi tu Sema kinachompa kiki jamaa ni kwa vile ni mwanasiasa hivo kila anachofanya kinakuwa kwenye media, akiweka P.O watu wanajua, akishinda P.O watu wanajua, lkn kuna vichwa vipo na vinapiga hela kimya kimya!
Back on our Constitution, ni kwamba Lissu anawaeleza wanaukuta kuhusu haki zinazoelezwa on the bill of rights under part3, lkn hawawaelezi kuhusu limitations on the given rights ambazo the same constitution imeweka.
Kwa ufupi katiba hii inakupa haki upande mmoja na inakunyanganya kupitia upande wa pili.kwa mfano haki xote zilizoolozeshwa zinaweza kunyanganywa kwa sababu ya maslahi ya umma, ukifatilia vzr katiba hii haijadefine nini maana ya maslahi ya umma, yaani ni vitu vp vinakuwa counted as amounting into public interest. Hata mahakama hadi Leo hazijaweza kutoa msimamo wa nini hasa ni maslahi ya umma.
Kwa maana hiyo Rais anaweza kutumia kipengere hicho kuamua anavoona yeye na akasema ni kwa maslahi ya umma, mfano aliposema huu ni mda wa kutekelexa ahadi, anaweza akaidefine hiyo kama maslahi ya umma.
Lissu analijua hilo, na ukweli Rais anatumia katiba, hivyo kupambana na Rais badala ya kupambana na katiba inayompa na kutoa loopholes hizo wao wanapambana na matokeo yake! Wengi tulitegemea wangeenda mahakamani ili wapate nini msimamo wa mahakama, then tuone kama Rais ataenda kinyume na maamuz ya mahakama.
Katiba imetoa room ya mtu anayedhani haki hizo under part3 zimekiukwa aende mahakaman, cha ajabu nguli huyu wa sheria badala ya kuwaongoza wenzake kwenda mahakamani anahamisisha watu waandane.
Ikumbukwe utawala wa sheria si kwa upande wa serikali tu, hata ss raia inatuhusu.
Kwanini wasiende mahakamani kama katiba inavoelekeza badala yake wanaamua kuandaa maandamano, hapa ndipo unapoiona illmotives!
Ikumbukwe sheria ya vyama vya siasa haiwezi kuwa juu ya katiba, kama katiba imeweka limitations on the enjoyment of the provided rights under part 3, sheria nyingine haiwezi kutoa free enjoyment of the same rights!
Anyway haya mambo ni magumu ndo maana wengi wataishia kukutukana tu, na kutoa comment zisizo kuwa na vichwa wala miguu!
bado hujajua kutafsiri sheria kajifunze upyaIbara ya 30 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inaongelea mipaka kwa Haki na Uhuru.
Chadema wanakuwa wanaongea sana huku Katiba ikiwaumbua wazi wazi.
Tuanze sasa:-
30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake
imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja
kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa
kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii
ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa
binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa
mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -
(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine
au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi
mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;
(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika
jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya
maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya
madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi
mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya
umma;
(c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya
mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai
au la jinai;
(d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine au
maisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri
mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunza
heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;
(e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji,
uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika ya
watu binafsi nchini; au
(f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo
linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.
(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii
ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au
wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na
mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza
kufungua shauri katika Mahakama Kuu.
Mwalimu nyerere aliwahi kusema Àkiwa kwenye sherehe za mei mosi mjini Mbeya kuhusu hatari viongozi kuruhusiwa kuanza kunyofoa haki za kiraia, hivi tatizo liko wapi? Mbona haki ya vyama vya siasa zimekuwepo kwa zaidi ya miaka 20 sasa bila tatizo hivi tukipora haki za kiraia ndio tutapata maendeleo? haki zetu zitaondoka moja baada ya nyingine mwisho zitakuhusu pia wewe unaedhani uko mbali. Siungi Mkono maandamano lakini pia siungi Mkono upolaji wa haki za kilaia kwa kisingizio chochote kile
hakuna mahari katika katiba ambapo mhe, Rais anaruhusiwa kuvunja sheria za nchi,isipokuwa tu katika hali ya hatari inapotangazwa,na hii si kama Rais anaamka asubuhi anaamua kutangaza hali ya hatari, kuna utaratibu maarumu tena kwa muda maarumu, unapozungumzia vyama vya siasa na sheria ya vyama vya siasa ndio iliyomuweka mhe, Raisi madarakani kwa hiyo inakihusu chama chake pia hata CCM ipo kwa msingi wa sheria hiyo mnao shabikia hili mnionyeshe kwamba mhe rais yupo juu ya sheria za nchi hii? au wapi panatamka kuwa mhe,Rais anaruhusiwa kuvunja katiba,ambayo aliapa kuilinda. kwa taarifa yako kuwa urais na taasisi yake ni moja ya mihimili mitatu ya nchi kuna taasisi zingine kama bunge kuna mahakama,kambuka kuwa pia rais aweza kuondolewa madarakani na bunge moja ya sababu ni pale inapothibitika amevunja katiba.Bwana mkubwa, kwa taarifa yako basic rights unazozizungumzia wkt wa Nyerere hazikuwahi kuwekwa kwenye katiba, ziliwekwa mwaka 1984 au 1985 baada Nyerere kung'atuka.
Cha pili hawa kina Lissu wanawakalilisha kuwa mna haki, lkn wanajua ukweli hakuna haki bila wajibu.
Rights without limitations becomes chaos!
Katiba imetoa haki na imeweka miaka, lkn pia imeweka mazingira ambao haki hizo zinaweza kupokwa!
Someni katiba msisubiri wanaume wenzenu wafikirie kwa ajiri yenu!
You know nothinghakuna mahari katika katiba ambapo mhe, Rais anaruhusiwa kuvunja sheria za nchi,isipokuwa tu katika hali ya hatari inapotangazwa,na hii si kama Rais anaamka asubuhi anaamua kutangaza hali ya hatari, kuna utaratibu maarumu tena kwa muda maarumu, unapozungumzia vyama vya siasa na sheria ya vyama vya siasa ndio iliyomuweka mhe, Raisi madarakani kwa hiyo inakihusu chama chake pia hata CCM ipo kwa msingi wa sheria hiyo mnao shabikia hili mnionyeshe kwamba mhe rais yupo juu ya sheria za nchi hii? au wapi panatamka kuwa mhe,Rais anaruhusiwa kuvunja katiba,ambayo aliapa kuilinda. kwa taarifa yako kuwa urais na taasisi yake ni moja ya mihimili mitatu ya nchi kuna taasisi zingine kama bunge kuna mahakama,kambuka kuwa pia rais aweza kuondolewa madarakani na bunge moja ya sababu ni pale inapothibitika amevunja katiba.
Anyway tuwaache waendelee kushikiwa fikira zao na wanaume wenzao!Unajua hawa vijana wetu wanalazimisha mambo yaende wanavyotaka wakati katiba inawabana. Wanashangaa kuona Lisu anavyowaingiza king.
BROTHER usifikili kuwa wewe tu ndo unajua huu ndo msingi wa katiba ya Tanzania ni wapi inaruhusu hayo mnayosema? na hasa kwenye hoja yetu ya msingi, ishu sio kutukana na wewe njoo na evidence ya hayo unayoongea mwaga hapo tuone.You know nothing
Sawa kabisa umeanza vizuri hebu endelea zaidi mpaka ufike ibara ya 29, 30 ,31. Nitakupa hapaBROTHER usifikili kuwa wewe tu ndo unajua huu ndo msingi wa katiba ya Tanzania ni wapi inaruhusu hayo mnayosema? na hasa kwenye hoja yetu ya msingi, ishu sio kutukana na wewe njoo na evidence ya hayo unayoongea mwaga hapo tuone.
mimi naanza kama ifuatavyo:-
Sheria ya 1984 Na.15 ib.3
KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 UTANGULIZI MISINGI YA KATIBA KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani:
NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:
KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.
Tangazo la nchi yenye Mfumo wa vyama vingi Sheria ya 1992 Na.4 ib.5 3.(1)
Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. (2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge
RAIS NI TUNDA LA VYAMA VYA SIASA KWA HIYO YEYE NI MWANASIASA
KATIBA JMT IB 41.-(1) Baada ya Bunge kuvunjwa au kukitokea jambo jingine lolote lililotajwa katika ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 38 na inalazimu uchaguzi wa Rais kufanyika, kila chama cha siasa kinachopenda kushiriki katika uchaguzi wa Rais kitawasilisha kwa Tume ya Uchaguzi, kwa mujibu wa sheria, jina la mwanachama wake mmoja kinayetaka asimame kama mgombea katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na jina la mwananchama wake mwingine kinayempendekeza kwa nafasi
Bunge laweza kumshtaki Rais Sheria ya 1992 Na.20 ib.8 Sheria ya 1995 Na.12 ib.4 46A.-(1)
Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii. (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais..
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.
Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994
20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
MPAKA HAPO SIJAONA MAHALI AMBAPO KUNA MTU YEYOTE KATIKA JAMHURI MWENYE MADARAKA YA KUZUIA VYAMA VYA SIASA KUFANYA KAZI YA SIASA NAOMBA MSAADA NIONYESHE KIFUNGU KIMOJA TU MHESHIMIWA
We jamaa ni poyoyo!