Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

soma sehemu "h" ya sheria hii ili ujitafakari upya sio matusi njoo na hoja na vielelezo.

Sheria ya Vyama vya Siasa, Tanzania

TANGAZO LA SERIKALI NA. 215 la tarehe 12/10/2007
SHERIA YA VYAMA VYA SIASA
(SURA YA 258)

-------------

KANUNI
(Zimetungwa chini ya fungu la 22(b))

KANUNI ZA MAADILI YA VYAMA VYA SIASA ZA MWAKA 2007

3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa pale muktadha utaelekeza vinginevyo- “chama cha siasa” maana yake ni chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kwa mujibu wa Sheria.
“Msajili” maana yake ni Msajili wa Vyama vya Siasa aliyeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria pia itajumuisha Naibu Msajili na Msajili Msaidizi;
“Sheria” maana yake ni Sheria ya Vyama vya Siasa.

SEHEMU YA PILI
HAKI YA CHAMA

4.–(1) Kila chama cha siasa kitakuwa na haki zifuatazo-

(a) Kutoa elimu ya uraia na elimu ya uchaguzi kwa wananchi kwa kufuata sheria na kanuni za nchi;
(b) Kutoa maoni ya kisiasa kadri itakavyoona inafaa ili kutekeleza sera zake, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar;
(c) Kujadili na kushindanisha sera zake na zile za chama cha siasa kingine kwa lengo la kutaka kukubalika na wananchi;
(d) Kuwa na uhuru wa kutafuta kuungwa mkono na wapiga kura; na
(e) Kila Chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na maandamano kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa;
(2) Wakati wa uchaguzi wowote utakaoendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, kila chama cha siasa kitakuwa na haki na uhuru wa kushiriki na kushirikishwa na Tume ya Uchaguzi na au chombo chochote chenye mamlaka katika kufanya uchunguzi na kupata matokeo katika jambo au suala lolote linalohusu uchaguzi.

SEHEMU YA TATU
WAJIBU WA CHAMA

5.-(1) Kila Chama cha Siasa kitakuwa na wajibu wa kutunza maadili chini ya kanuni hizi kwa: -
(a) kukieleza kwa wanachama wake ili kuongeza uadilifu wa kisiasa ndani na nje ya chama cha siasa;
(b) kulaani, kuepukana kuchukua hatua zitakazofaa ili kuzuia au kuepusha vitendo vya vurugu, uvunjaji wa Amani au ukandamizaji wa aina yeyote ile;
(c) kutotumia vyombo vya dola kukandamiza na kutoa vitisho kwa chama cha siasa kingine kwa manufaa yake;
(d) kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni ya uongo na kuhusu mtu yeyote au chama cha siasa chochote;
(e) kufanya mkutano wa kisiasa na maandamano bila kufanya vurugu kwa mujibu wa sheria za nchi;
(f) kulaani na kupinga-
(i) vitendo vyenye kuashiria ukandamizaji;
(ii) matumizi ya lugha ya matusi
(iii) vitendo vya kibabe na vurugu
(iv) matumizi ya nguvu ili kujipatia umaarufu wa chama au sababu yeyote ile;
(f) Kuepuka kuteremsha bendera iliyowekwa kwa mujibu wa Sheria, kuharibu kwa namna yeyote ile kitu chochote ambacho ni ishara au nembo inayotumiwa na chama kingine kama sehemu ya utambulisho wa chama hicho;
(g) Kuepuka kushawishi kwa kutoa rushwa kama kichocheo ili kupata upendeleo au heshima kwa nia ya kufanikisha malengo;

(h) Kuepuka kutumia mamlaka. Rsilimali za serikali, vyombo vya dola, au wadhifa wa kiserikali, kisiasa au ufadhili wa nje ama wa ndani kwa namna yeyote ile ili kukandamiza chama kingine.

(i) Kuepuka vitendo vya ubaguzi wa rika, kabila, jinsia, dini na mahali alipozaliwa mtu yeyote ikiwa ni jamii au asili Fulani kwa kufanikisha malengo ya siasa; na
(j) Kuheshimu maamuzi halali yaliyofanywa kwa pamoja na vyama vyote.
(2) Kwa kuzingatia Sheria, kila chama cha siasa kitakuwa na uhuru wa kushirikiana na chama cha siasa kingine kwa nia njema kwa ajili ya kupanga vikao, mikutano ya hadhara kwa pamoja au maandamano kwa wakati mmoja kama kwamba mambo hayo yamefanywa na chama cha siasa kimoja au bila kuvunja sheria za nchi.
Wewe naona upo nje kabisa na huu mjadala. Hiyo ni sheria ya vyama vya siasa haiwezi kuwa juu ya katiba. Katiba ndio sheria mama. Kuna kipengere kwenye katiba ibara ya 30. Inaongelea maslahi ya umma. Elewa Sheria na katiba ipi iliyojuu
 
vyama vya upinzani vilipata kura harali zaidi ya m6 na ccm zaidi ya m8 ni nani anasimamia maslahi ya umma katika hili
umefanya utafiti ukajua kuna watu kiasi gani nyuma ya wanaodai haki zao za kikatiba, ambazo wewe unadhani sio maslahi ya umma kesi iliyo mbele yetu ni maslahi ya umma dhidi ya maslahi ya umma sio maslahi binafsi dhidi ya maslahi ya umma, ibara unayotaja inahusu maslahi binafsi dhidi ya maslahi ya umma. check upya maana ya kifungu hicho pls
 
Wewe naona upo nje kabisa na huu mjadala. Hiyo ni sheria ya vyama vya siasa haiwezi kuwa juu ya katiba. Katiba ndio sheria mama. Kuna kipengere kwenye katiba ibara ya 30. Inaongelea maslahi ya umma. Elewa Sheria na katiba ipi iliyojuu

Tangazo la nchi yenye Mfumo wa vyama vingi Sheria ya 1992 Na.4

ib.5 3.
(1)Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
(2) Mambo yote yahusuyo uandikishaji na uendeshaji wa vyama vya siasa nchini yatasimamiwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na ya sheria iliyotungwa na Bunge.

nimekupa katiba ya TZ ibara ya 5 ibara ndogo ya 3 , 2
maana yake ni kwamba sheria ya vyama vya siasa huwezi kuitenganisha na katiba kwani imezaliwa na katiba maana yake sheria hiyo ipo kwa mujibu wa matakwa ya katiba

zaidi ya yote huna unalolijua zaidi ya kukaririshwa.

Ndugu usilazimishe tamko la kusema nchi ya vyama vingi ndio halali ya kufanya mikutano. Ni sehemu gani katiba imesema vyama vya siasa kufanya mikutano?
 
Mkuu Lissu anatumia advantage ya watu kama hawa ambao hawajawahi kuiona hata katiba inafananaje.

Lissu ni wa kawaida sana, kwa wale tunaoshinda mahakamani tunajua, Nchi hii kuna vichwa vingi tu Sema kinachompa kiki jamaa ni kwa vile ni mwanasiasa hivo kila anachofanya kinakuwa kwenye media, akiweka P.O watu wanajua, akishinda P.O watu wanajua, lkn kuna vichwa vipo na vinapiga hela kimya kimya!

Back on our Constitution, ni kwamba Lissu anawaeleza wanaukuta kuhusu haki zinazoelezwa on the bill of rights under part3, lkn hawawaelezi kuhusu limitations on the given rights ambazo the same constitution imeweka.

Kwa ufupi katiba hii inakupa haki upande mmoja na inakunyanganya kupitia upande wa pili.kwa mfano haki xote zilizoolozeshwa zinaweza kunyanganywa kwa sababu ya maslahi ya umma, ukifatilia vzr katiba hii haijadefine nini maana ya maslahi ya umma, yaani ni vitu vp vinakuwa counted as amounting into public interest. Hata mahakama hadi Leo hazijaweza kutoa msimamo wa nini hasa ni maslahi ya umma.

Kwa maana hiyo Rais anaweza kutumia kipengere hicho kuamua anavoona yeye na akasema ni kwa maslahi ya umma, mfano aliposema huu ni mda wa kutekelexa ahadi, anaweza akaidefine hiyo kama maslahi ya umma.

Lissu analijua hilo, na ukweli Rais anatumia katiba, hivyo kupambana na Rais badala ya kupambana na katiba inayompa na kutoa loopholes hizo wao wanapambana na matokeo yake! Wengi tulitegemea wangeenda mahakamani ili wapate nini msimamo wa mahakama, then tuone kama Rais ataenda kinyume na maamuz ya mahakama.
Katiba imetoa room ya mtu anayedhani haki hizo under part3 zimekiukwa aende mahakaman, cha ajabu nguli huyu wa sheria badala ya kuwaongoza wenzake kwenda mahakamani anahamisisha watu waandane.

Ikumbukwe utawala wa sheria si kwa upande wa serikali tu, hata ss raia inatuhusu.
Kwanini wasiende mahakamani kama katiba inavoelekeza badala yake wanaamua kuandaa maandamano, hapa ndipo unapoiona illmotives!

Ikumbukwe sheria ya vyama vya siasa haiwezi kuwa juu ya katiba, kama katiba imeweka limitations on the enjoyment of the provided rights under part 3, sheria nyingine haiwezi kutoa free enjoyment of the same rights!

Anyway haya mambo ni magumu ndo maana wengi wataishia kukutukana tu, na kutoa comment zisizo kuwa na vichwa wala miguu!
Back on our constitution,...hakika hautakuwa miongoni mwa hvo vichwa.

Hivo vichwa vingesaidia jamii kujua haki zao kikatiba au kuitaka/kuishauri serikali tuwe na katiba ambayo haimpi raia/jamii haki kwa mkono mmoja na kunyan'ganya kwa mkono wa pili.

Elimu uliyopata kwa kodi za wananchi maskini...hata kama unalipa mkopo sio kwa ajili ya kupiga hela ndefu tu,,,bali ni kwa ajili ya kusaidia jamii pia,,
 
Ndio maana katiba huwa inatengeneza sheria zinazotungwa kwa matakwa ya katiba kama sheria ya vyama vya siasa inatambua mikutano na maandamano ndio maana ili uelewe vizuri kwenye katiba unakuta maneno bila kuathili,itatungwa sheria, hizi zote huitwa sheria ambata sheria zinazoteleza matakwa ya katiba ukitaka kuondoa hizo razima ufanye marekebisho ya katiba
 
Hii ni sheria ya Jeshi la Polisi:_

44. Afisa polisi msimamizi anaweza kusitisha au kuzuia kufanyika au kuendelea kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano yoyote katika sehemu yoyote ile kama, kwa mawazo ya afisa huyo anaona kufanyika au kuendelea kufanyika, kama inavyoweza kuwa, kwa mkusanyiko au maandamano hayo yanavunja amani au kuvuruga usalama wa umma au kulinda amani na amri, na anaweza, kwa manufaa ya umma, ikiwa ni pamoja na amri ya kutawanya kwa mkusanyiko huo au maandamano kama ilivyosemwa.

45. Mkusanyiko au maandamano yoyote ambayo watu watatu au zaidi wanaohudhuria au kuchukua nafasi wanazembea au kukataa kufuata amri yoyote ya kutawanywa iliyotolewa chini ya masharti yaliyopo katika kifungu kidogo cha (4) cha kifungu cha 43 au kifungu cha 44, itahesabika kuwa mkusanyiko kinyume na sheria katika maana iliyopo katika kifungu cha 74 cha Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai*
 
Back on our constitution,...hakika hautakuwa miongoni mwa hvo vichwa.

Hivo vichwa vingesaidia jamii kujua haki zao kikatiba au kuitaka/kuishauri serikali tuwe na katiba ambayo haimpi raia/jamii haki kwa mkono mmoja na kunyan'ganya kwa mkono wa pili.

Elimu uliyopata kwa kodi za wananchi maskini...hata kama unalipa mkopo sio kwa ajili ya kupiga hela ndefu tu,,,bali ni kwa ajili ya kusaidia jamii pia,,

Brother Warioba alikuwa na rasimu nzuri sana lkn ikachakachuliwa na mmoja kati ya watu wanaotajwa kutumika nguvu nyingi na ushaewishi ni Edward Lowassa akishirikiana na Change.Aliamini atakuwa Rais hivyo alitaka aongize kwa kutumika katiba hii hii.
Lkn Leo yupo CDM Leo na anaongoza mapambano dhidi ya katiba ambayo yeye mwenyewe aitumie kutawala. Ninachosema hata mambo wkt mwingine changanya na zako siyo kila anayepiga kelele ana nia ya kukusaidia mwanainchi wa kawaida, wengine ni matumbo mkuu!
 
Mamlaka ya Rais

148.-(1) Bila ya kuathiri masharti yatakayowekwa na sheria
yoyote iliyotungwa na Bunge, miongoni mwa madaraka ya Rais
akiwa kama Amiri Jeshi Mkuu ni kuyaamuru majeshi ya nchi
yatende mambo yanayohusika na vita vya ulinzi wa Jamhuri ya
Muungano, mambo ya kuokoa maisha na mali ya watu katika
hali ya hatari na mambo mengineyo ambayo Amiri Jeshi Mkuu
ataona yahitajika, na kwa ajili hiyo Amiri Jeshi Mkuu aweza
kuyaamuru hayo majeshi yatende mambo hayo ama ndani au
nje ya Tanzania.
Bila shaka wewe ni mbumbumu wa sheria hio ibara inazungumzia hali ya hatari je? hali ya hatari imetangawza..watu wamekaa miaka kibao chuoni wanasoma sheria wewe uje ukurupuke tu na kuanza kuichambua katiba tuu ennh...kama hali ya hatari haija tangazwa hicho kifungu hakitumiki...
 
Hii ni sheria ya Jeshi la Polisi:_

44. Afisa polisi msimamizi anaweza kusitisha au kuzuia kufanyika au kuendelea kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano yoyote katika sehemu yoyote ile kama, kwa mawazo ya afisa huyo anaona kufanyika au kuendelea kufanyika, kama inavyoweza kuwa, kwa mkusanyiko au maandamano hayo yanavunja amani au kuvuruga usalama wa umma au kulinda amani na amri, na anaweza, kwa manufaa ya umma, ikiwa ni pamoja na amri ya kutawanya kwa mkusanyiko huo au maandamano kama ilivyosemwa.

45. Mkusanyiko au maandamano yoyote ambayo watu watatu au zaidi wanaohudhuria au kuchukua nafasi wanazembea au kukataa kufuata amri yoyote ya kutawanywa iliyotolewa chini ya masharti yaliyopo katika kifungu kidogo cha (4) cha kifungu cha 43 au kifungu cha 44, itahesabika kuwa mkusanyiko kinyume na sheria katika maana iliyopo katika kifungu cha 74 cha Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai*
Kwaio mkulu ni afisa wa polisi sio?
 
Kinachosisitizwa na mleta mada, pamoja na nukuu za Katiba ya JMT, ni kusisitiza kuwa n
 
Safi sana
CDM wana tumia umbumbumbu wa wanachama wao
Kuwa danganya.
Nakuambia hawa hawana nafasi tena
Wana tapatapa,
Hoja ya Ufisadi imewapoteza hawana
Muelekeo tena
Soma uelewe usichangie KWA jazba, hii SHERIA si ya upande mmoja, kuna chanzo na sababu.
 
Bila shaka wewe ni mbumbumu wa sheria hio ibara inazungumzia hali ya hatari je? hali ya hatari imetangawza..watu wamekaa miaka kibao chuoni wanasoma sheria wewe uje ukurupuke tu na kuanza kuichambua katiba tuu ennh...kama hali ya hatari haija tangazwa hicho kifungu hakitumiki...
Acha kukurupuka kama umetoka shimoni. Hujui hata tumeanzia wapi. Hebu isome kwanza ibara ya 30 na kisha uende kwenye hiyo. Acha ukurupukaji.
 
Kusisitiza kwamba CHADEMA wana wanasheria nguri, km Lissu, ambao wanajua Katiba iliyonukuliwa ina vifungu vinavyotoa nafasi kufikisha mahakamani suala la kuvunjwa Katiba. Kwa nini hawa wanasheria nguri wanakimbilia njia ya mkato, na isiyo halali (tayari polisi imeyazuia) ya maandamano. Hatuhitaji tafsiri ya Katiba mitandaoni, au kwenye mikutano ya hadhara au maandamano, ambako ni kuvunja Katiba hiyo hiyo.
 
Acha kukurupuka kama umetoka shimoni. Hujui hata tumeanzia wapi. Hebu isome kwanza ibara ya 30 na kisha uende kwenye hiyo. Acha ukurupukaji.
Huko kote nishasoma mkuu...na katiba kwangu sio issue...unachotakiwa kutaja pa ni sehemu zinazozungumzia uhuru wa watu kuandamana...maana kabla haujafika huko ibara ya 30 unaanza na uhuru wa watu kwanza...
 
Wewe ndiye unatakiwa ueleze wapi katiba imetoa uhuru wa mtu kuandamana. Kuanzia ibara ya kwanza mpaka ya mwisho kwenyekatiba hakuna sehemu katiba imempa raia haki ya kuandamana.
Soma katiba wewe acha kulishwa maneno hewa na akina Lisu
 
Kusisitiza kwamba CHADEMA wana wanasheria nguri, km Lissu, ambao wanajua Katiba iliyonukuliwa ina vifungu vinavyotoa nafasi kufikisha mahakamani suala la kuvunjwa Katiba. Kwa nini hawa wanasheria nguri wanakimbilia njia ya mkato, na isiyo halali (tayari polisi imeyazuia) ya maandamano. Hatuhitaji tafsiri ya Katiba mitandaoni, au kwenye mikutano ya hadhara au maandamano, ambako ni kuvunja Katiba hiyo hiyo.
Maandamano yakishakua na kauli mbiu ya uchochezi hata mimi siyafurahii,kweni tukiandaa maandamano yenye kauli amani tutazuiwa na nani?unaelewa tafsili ya UKUTA?
 
Umetumia nguvu kubwa kuandika ujumbe wako,

Sasa hapo Chadema wameumbuka Wapi?

Anayeisigina Katiba anafahamika, lakini kwa bahati mbaya watu wengi wanamgwaya ......

Inaelekea hizi post za mfululizo za kuishambulia Chadema bila hoja zenye mashiko ni kuonyesha kuweweseka kwa watawala kutokana na vuguvugu la operesheni Ukuta.
chadema wameumbuka wapi? nikuulize; cdm wameenda mahakamani kutaka agizo la mkuu wa jeshi la polisi kusitisha maandamano namikutano ya hadhara lisitishwe. je walifanikiwa? sasa kwa nini wsnajidai lazima waandamane.
 
Back
Top Bottom