Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Jinsi Katiba inavyoiumbua CHADEMA

Yote na yote tunasema hakuna mshindi katika hili cha msingi pande zote zikutane waangalie wapi wameteleza waparekebishe, Taifa letu libaki kuwa moja, tunaopendana na kuheshimiana jukumu la kuliunganisha taifa ni letu wote bila kujali tofauti zetu, Mungu ibariki Tanzania NA HAYA NDIO MASLAHI YA TAIFA
 
Ibara ya 30 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inaongelea mipaka kwa Haki na Uhuru.
Chadema wanakuwa wanaongea sana huku Katiba ikiwaumbua wazi wazi.

Tuanze sasa:-

30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake
imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja
kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa
kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.
(2) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika Sehemu hii
ya Katiba hii, yanayofafanua misingi ya haki, uhuru na wajibu wa
binadamu, hayaharamishi sheria yoyote iliyotungwa wala kuzuia
sheria yoyote kutungwa au jambo lolote halali kufanywa kwa
mujibu wa sheria hiyo, kwa ajili ya -

(a) kuhakikisha kwamba haki na uhuru wa watu wengine
au maslahi ya umma haviathiriwi na matumizi
mabaya ya uhuru na haki za watu binafsi;
(b) kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika
jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya
maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya
madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi
mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya
umma;
(c) kuhakikisha utekelezaji wa hukumu au amri ya
mahakama iliyotolewa katika shauri lolote la madai
au la jinai;
(d) kulinda sifa, haki na uhuru wa watu wengine au
maisha binafsi ya watu wanaohusika katika mashauri
mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri; kutunza
heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama;
(e) kuweka vizuizi, kusimamia na kudhibiti uanzishaji,
uendeshaji na shughuli za vyama na mashirika ya
watu binafsi nchini; au

(f) kuwezesha jambo jingine lolote kufanyika ambalo
linastawisha au kuhifadhi maslahi ya taifa kwa jumla.

(3) Mtu yeyote anayedai kuwa sharti lolote katika Sehemu hii
ya Sura hii au katika sheria yoyote inayohusu haki yake au
wajibu kwake, limevunjwa, linavunjwa au inaelekea litavunjwa na
mtu yeyote popote katika Jamhuri ya Muungano, anaweza
kufungua shauri katika Mahakama Kuu.

Hii sheria inazungumuzia haki na wajibu wa mtu binafsi na vyama, lakini si vyama vya siasa. Ina maaana vyama vilivyotamkwa ni k.m. vya hiari nk. Vyama vya siasa zipo sehemu sura nyingine ya katika katiba na si hapo usichanganye watu.
 
Sasa si ndo uiseme hiyo sura unayoijua na sisi tujifunze?
 
Hii sheria inazungumuzia haki na wajibu wa mtu binafsi na vyama, lakini si vyama vya siasa. Ina maaana vyama vilivyotamkwa ni k.m. vya hiari nk. Vyama vya siasa zipo sehemu sura nyingine ya katika katiba na si hapo usichanganye watu.
Duh sura ipi sasa na ibara ya ngapi? Hakuna ibara yoyote kwenye katiba inaongelea uhuru wa vyama vya siasa.
 
Katazo la kufanya mikutano ama shughuli yeyote ya kisiasa kwa wapinzani hadi 2020 ipo kwa kifungu gani? Na kipemgele kipi cha katiba kanampa mtu mamlaka ya kuzuia shughuli za kisiasa nchini kwa muda anaotaka yeye?
 
((3) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii hayataidhinisha mtu kunyang'anywa haki yake ya kuwa hai isipokuwa tu kwa kifo kama matokeo ya vitendo vya kivita)

Jeshi la polisi linajifua kutoa uhai wa watakaoandamana na kufanya mikutano, je itakuwa ni kwa matokeo ya kivita kwa mujibu wa kifungu kidogo hiki?!
una uhakika kwamba wamejipanga kuua? ni virungu tu na maji ya kuwasha pamoja na mabomu ya machozi. ninyi mnataka tu mpate kick kwamba police wamemwaga damu. nao wameshashtuka. labda muuane wenyewe. hafi mtu ni virungu tu.
 
Katazo la kufanya mikutano ama shughuli yeyote ya kisiasa kwa wapinzani hadi 2020 ipo kwa kifungu gani? Na kipemgele kipi cha katiba kanampa mtu mamlaka ya kuzuia shughuli za kisiasa nchini kwa muda anaotaka yeye?
Na ni kifungu gani kwenye katiba kimesema vyama vya siasa kufanya mikutano?
 
Brother Warioba alikuwa na rasimu nzuri sana lkn ikachakachuliwa na mmoja kati ya watu wanaotajwa kutumika nguvu nyingi na ushaewishi ni Edward Lowassa akishirikiana na Change.Aliamini atakuwa Rais hivyo alitaka aongize kwa kutumika katiba hii hii.
Lkn Leo yupo CDM Leo na anaongoza mapambano dhidi ya katiba ambayo yeye mwenyewe aitumie kutawala. Ninachosema hata mambo wkt mwingine changanya na zako siyo kila anayepiga kelele ana nia ya kukusaidia mwanainchi wa kawaida, wengine ni matumbo mkuu!

Unamuongelea warioba yupi mkuu...jaji warioba au warioba aka Yuda iskariot aliyeamua kuacha kusimamia anachokiamini kulinda ulaji wa mtoto wake...

Lowasa Lowasa Lowasa...hv huko cmm hakukuwa na mtu mwenye akili za ushawishi zaidi ya Lowasa,,,au wabunge wote wa ccm ni vichwa maji vilivokuwa vinaendeshwa na Lowasa?? Na kama unaamini kuwa Lowasa alikuwa kila kitu ccm basi baaada ya kuhama nusu ya wanaccm wangemfuata...Mkuu umesema unashinda mahakamani kwa maana hyo we ni mwanasheria na mna ile society yenu inaitwa TLS sijui...kwani hii society yenu haiwezi kuishauri serikali ikamfungulia mashtaka mh Lowasa na ikatoa wanasheria wa kuisimamia hyo kesi hili huyu mh anayeiharibu nchi afikishwe sehemu inayomstahili...mbona zimekuwa ni ngonjera tu mara lowasa hivi mara vile...hyo society yenu haina vichwa viisaidie serikali kwa hilo...au mnavokutanaga sijui mara moja au.mbili.kwa mwaka huwa mnajadili nini kwa mslahi ya taifa,,,au huwa mnaekekezana sehemu mnaweza pata suti za mtumba tu...

Nimesoma comments zako kuna baadhi unasimamia ukweli acha kumpa kichwa hyo Lumumba annael sijui anayekuchukua kifungu cha katiba kama kilivo bila kujua tafsiri yake..

Katiba ndo sheria mama na hakuna sheria inaweza tungwa ambayo itakinzana na katiba...ikitokea hvo lazima kutakuwa na mgogoro.

Nyie wanasheria acheni kupaoasa sheria someni sheria muelewe sheria mlisaidie taifa...ndo maana kwenye mikataba tunaingizwa mkenge kila mara kwa wanasheria wetu kutokuelewa vizuri jinsi ya kutafsiri vifungu vya sheria..

Inasikitisha anayejiita mwanasheria na mwalimu wa sheria anachukua zaidi ya siku saba kuelewa kuwa bunge halina mamlaka ya kujadilia kutoa tamko kwa hukumu iliyotolewa na mahakama. Kama mwalimu wa sheria nashindwa jambo dogo kiasi hicho je mwanafunzi wake je??
 
Naona upo nje ya mada kabisa. Maana unalalama tu. Unajua umeandika maneno meeengi lakini ndani yake ni pumba tupu?
Hebu rudi kwenye mada na tuongelee kile wanachokidai chadema kama kweli kipo kikatiba au ni kutafuta kiki tu.
 
Mkuu Lissu anatumia advantage ya watu kama hawa ambao hawajawahi kuiona hata katiba inafananaje.

Lissu ni wa kawaida sana, kwa wale tunaoshinda mahakamani tunajua, Nchi hii kuna vichwa vingi tu Sema kinachompa kiki jamaa ni kwa vile ni mwanasiasa hivo kila anachofanya kinakuwa kwenye media, akiweka P.O watu wanajua, akishinda P.O watu wanajua, lkn kuna vichwa vipo na vinapiga hela kimya kimya!

Back on our Constitution, ni kwamba Lissu anawaeleza wanaukuta kuhusu haki zinazoelezwa on the bill of rights under part3, lkn hawawaelezi kuhusu limitations on the given rights ambazo the same constitution imeweka.

Kwa ufupi katiba hii inakupa haki upande mmoja na inakunyanganya kupitia upande wa pili.kwa mfano haki xote zilizoolozeshwa zinaweza kunyanganywa kwa sababu ya maslahi ya umma, ukifatilia vzr katiba hii haijadefine nini maana ya maslahi ya umma, yaani ni vitu vp vinakuwa counted as amounting into public interest. Hata mahakama hadi Leo hazijaweza kutoa msimamo wa nini hasa ni maslahi ya umma.

Kwa maana hiyo Rais anaweza kutumia kipengere hicho kuamua anavoona yeye na akasema ni kwa maslahi ya umma, mfano aliposema huu ni mda wa kutekelexa ahadi, anaweza akaidefine hiyo kama maslahi ya umma.

Lissu analijua hilo, na ukweli Rais anatumia katiba, hivyo kupambana na Rais badala ya kupambana na katiba inayompa na kutoa loopholes hizo wao wanapambana na matokeo yake! Wengi tulitegemea wangeenda mahakamani ili wapate nini msimamo wa mahakama, then tuone kama Rais ataenda kinyume na maamuz ya mahakama.
Katiba imetoa room ya mtu anayedhani haki hizo under part3 zimekiukwa aende mahakaman, cha ajabu nguli huyu wa sheria badala ya kuwaongoza wenzake kwenda mahakamani anahamisisha watu waandane.

Ikumbukwe utawala wa sheria si kwa upande wa serikali tu, hata ss raia inatuhusu.
Kwanini wasiende mahakamani kama katiba inavoelekeza badala yake wanaamua kuandaa maandamano, hapa ndipo unapoiona illmotives!

Ikumbukwe sheria ya vyama vya siasa haiwezi kuwa juu ya katiba, kama katiba imeweka limitations on the enjoyment of the provided rights under part 3, sheria nyingine haiwezi kutoa free enjoyment of the same rights!

Anyway haya mambo ni magumu ndo maana wengi wataishia kukutukana tu, na kutoa comment zisizo kuwa na vichwa wala miguu!

Mm sikuwa kuingia hata darasa la sheria ila common sense tu ilinipelekea kuelewa huwezi Rais wa nchi usiweze kuzuia mambo ambayo yanaingilia maslahi ya taifa...

Ni ajabu kweli watu kitumia raia wasiorlewa kufikoa malengo yao. Lakini nimbaya zaidi kam Rais wancho ataacha kulonda raia hao ili wasitapeliwe katika nafasi yake. Hicho kwangu mm ndicho kiapo alichoapa kuilonda katiba
 
U
Na ni kifungu gani kwenye katiba kimesema vyama vya siasa kufanya mikutano?

Unajua we ni mbunda na umbunda wako usikufanye ukachosha watu hapa...katiba haiwezi kueleza kika kitu ndo maana kuna sheria zinazotungwa kusimamia malengo fulani. Kama unataka katiba ieleze kila kitu basi tungekuwa na katiba yenye kurasa nyingi kushinda biblia na ingebidi kuwa na chombo maalumu cha kuibeba..

Katiba inasema uwepo wa vyama vingi vya siasa hyo mikutano na maandamano yamewekwa kwenye sheria iliyoanzisha vyama vingi vya siasa.

Tatizo lako ukasuku wa kijani ndo unakusumbua..
 
Sasa unayoyaongea hayo Je umsesoma katiba ya Tanzania Ibara 29,30 na 31? Hebu pitia hizo ibara ili uweze kujua kwamba haki na uhuru kuna limitations zake. Moja ya Limitation ya uhuru na haki ni maslahi ya umma. Na anayetafsiri maslahi ya umma ni mamlaka. Na tayari kwa kifungu hiki rais amesema hakuna kufanya mikutano mpaka 2020 ili watu waweze kufanya kazi kwa maslahi ya umma.

Sasa wewe hicho kisheria chako cha haki za vyama kufanya mikutano kitakuwa na nguvu gani kutokana na ibara hizo hapo tajwa za katiba?
Naomba usinikimbie.
 
Naona upo nje ya mada kabisa. Maana unalalama tu. Unajua umeandika maneno meeengi lakini ndani yake ni pumba tupu?
Hebu rudi kwenye mada na tuongelee kile wanachokidai chadema kama kweli kipo kikatiba au ni kutafuta kiki tu.

Nimemjibu jamaa yako alichouliza acha kurukia vitu visivokuhusu
 
Sasa unayoyaongea hayo Je umsesoma katiba ya Tanzania Ibara 29,30 na 31? Hebu pitia hizo ibara ili uweze kujua kwamba haki na uhuru kuna limitations zake. Moja ya Limitation ya uhuru na haki ni maslahi ya umma. Na anayetafsiri maslahi ya umma ni mamlaka. Na tayari kwa kifungu hiki rais amesema hakuna kufanya mikutano mpaka 2020 ili watu waweze kufanya kazi kwa maslahi ya umma.

Sasa wewe hicho kisheria chako cha haki za vyama kufanya mikutano kitakuwa na nguvu gani kutokana na ibara hizo hapo tajwa za katiba?
Naomba usinikimbie.

Hayo maslahi ya umma ni mtu mwenyewe anavotafsiri hayo maslahi ya umma...katiba haijaeleza hayo maslahi ya umma ni kitu gani..

Anaweza hata akasema ccm tu ndo wafanye mikutano kwa maslahi ya umma..rais wa nchi anatakiwa kutumia zaidi busara kuongoza na si ubabe wala hisia zake.

Na nimeshakuambia kama sheria ya kuanzisha vyama vingi ingeonekana inakinzana na sheria mama ingeshafanyia marekebisho zamani sana. Ishu hapa ni mkulu hataki kukubaliana na tafsiri ya katiba anang'ang'ania mstari kama ukivoandikwa kama ambavyo na wewe unang'ang'ania hapa..
 
una uhakika kwamba wamejipanga kuua? ni virungu tu na maji ya kuwasha pamoja na mabomu ya machozi. ninyi mnataka tu mpate kick kwamba police wamemwaga damu. nao wameshashtuka. labda muuane wenyewe. hafi mtu ni virungu tu.
Kwani hivo virungu na maji ya kuwasha ni panadol au ni cristerpen?!
Kwani haviwezi kuua?!
 
Hayo maslahi ya umma ni mtu mwenyewe anavotafsiri hayo maslahi ya umma...katiba haijaeleza hayo maslahi ya umma ni kitu gani..

Anaweza hata akasema ccm tu ndo wafanye mikutano kwa maslahi ya umma..rais wa nchi anatakiwa kutumia zaidi busara kuongoza na si ubabe wala hisia zake.

Na nimeshakuambia kama sheria ya kuanzisha vyama vingi ingeonekana inakinzana na sheria mama ingeshafanyia marekebisho zamani sana. Ishu hapa ni mkulu hataki kukubaliana na tafsiri ya katiba anang'ang'ania mstari kama ukivoandikwa kama ambavyo na wewe unang'ang'ania hapa..
Hapa una bwabwaja tu bila hata kusoma hiyo katiba. Vifungu vinajieleza wazi kwamba kama unaona katiba imevunjwa, inavunjwa au inaelekea kuvunja unatakiwa uende mahakamani.
Acha ufinyu wa mawazo soma hiyo katiba.
Sasa hao maboss zako wameenda mahakamani? Umewahi kujiuliza kwanini wasiende mahakamani? Wanajua watapigwa za uso.

Wewe hapa unakuja na kupayuka payuka bila hata kusoma katiba.
Vifungu nimekuwekea na katiba ipo online umekalia uzembe wa kushindwa kusoma.
 
Kwani hivo virungu na maji ya kuwasha ni panadol au ni cristerpen?!
Kwani haviwezi kuua?!
Hebu soma sheria ya jeshi la polisi kuhusu kuzuia mikusanyika na maandamano. Na kwamba polisi anaweza akatumia nguvu kwa yule anayeshindwa kutii amri halali ya polisi.

Vilevile polis anaweza akatumia silaha kuweza kumlinda mwingine ili asidhulike.

Vilevile anaweza akatumia shaba kwa yule anayetaka kutoroka akikamatwa.

Soma sheria za jeshi la polisi zipo online.
 
Screenshot_2016-08-27-15-56-08.png
 
Back
Top Bottom