Jinsi Joseph Kabila alivyopiga chenga ya mwili, akili za wapinzani na mataifa ya Nje!


Iko hivi, Ukishakalia kile kiti kinachoitwa Uraisi, Ukishapanga Safu zako vizuri kwenye vyombo vya usalama huwa hakuna cha fulani au fulani ndiye aliyekubeba kukaa hapo ulipo, Yaani wewe ni mtu level nyingine kabisa!, BWM na JKN ni mfano mmojawapo
 
Kabila alikuwa na Plan A ambayo ilikuwa ni kung'ang'ania madarakani ambayo ilifeli, akawa na Plan B kumpachika kibaraka wake Shadary nayo ikafeli, akaja na hii Plan C ya kum-shortchange Fayulu ambayo ndio kama imefaulu japo kwa muda.

Itabidi huyu Tshisekedi asome vizuri alama za nyakati akijua kwamba hakua chaguo sahihi la wacongomani na kama atajaribu kuwa rais wa cheo ila mamlaka akamuachia Kabila, basi hapo atakuwa amejitia kitanzi.

Itabidi watu, pamoja na taasisi yenye nguvu kama kanisa la Roman Catholic sambamba na wazungu wamvurugie "Party" tena mapema kabisa hatua ambayo yeye Tshisekedi hataweza kuivumilia na itampelekea nguanzisha Plan D ambayo haitamuacha salama Kabila na wapambe wake ambao wana tuhuma nyingi za ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Huyo Tshisekedi ili atawale inabidi atafute muafaka na kanisa pamoja na nchi za magharibi, hili hawezi kuliepuka hata afanyeje, because they call the shots.
 
Mimi nionavyo, kama kuna mkataba kati ya Kabila na Tshekedi utakuwa wa muda tu kwani kelele hizi nyingi zitamshtua Tshekedi na kumtosa Kabila. Ni suala la muda tu. Pia mahakama ya kikatiba washajua Kabila ni fungu la kukosa hivyo rufaa ya Fayulu inaweza ikaibua jambo litakalomuacha kabila mdomo wazi. Tusikilizie!
 
Kabla ya kuwasakama wazungu, tujiulize kwa dhati kabisa sisi waafrika, tunafanya nini kusaidia demokrasia ndani ya nchi zetu. Tukishindwa kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe tujiandae kusumbuliwa na hawa the so called mabeberu!
Demokrasia bila maendeleo ni ujinga mtupu na kelele Zinazoumiza masikio na vichwa vyetu.
 
Imeleta logic now.
 
nahitaji Muda Kukuelezea Uelewe,sina Kwa Sasa,ila Naahidi Kuweka Maelezo Marefu Hapa Baadae Naamini Utapata Ufafanuzi Mzuri Tu Mkuu.
Naomba unitumie PM huo mfafanuo au kiweka nitag mana inaonyesha ni stori nzuri sana. Kweli Jf raha
 

unajuaje kama atalinda maslahi ya nchi yake?
 
So deep

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Write your reply...kanisa katoliki acheni kuleta machafuko huko congo! Mmeanza kujipambanua kuwa, kweli nyinyi ni wawakilishi wa shetani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…