Jinsi Joseph Kabila alivyopiga chenga ya mwili, akili za wapinzani na mataifa ya Nje!

S

Shigganza

Member
Joined
May 24, 2018
Messages
50
Likes
108
Points
40
S

Shigganza

Member
Joined May 24, 2018
50 108 40
Jana tume ya uchaguzi Nchini nKongo (CENI) ilimtangaza FELIX TSHISEKEDI kutoka chama cha Upinzani cha UDSP kuwa mshindi wa kiti cha Urais baada ya kupata kura milioni 7, akifuatiwa na MARTIN FAYULU kura milioni 6.4 aliyekuwa akiwakilisha Muungano wa vyama vya Upinzani huku mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na Rais anayemaliza muda wake EMMANUEL SHANDRY akiambulia milioni 4.4.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, wafuasi wengi wa vyama vya Upinzani Nchini Kama ambavyo ilitarajiwa hawakusita kuonesha furaha zao kupitia mitandao mbalimbali kwa hoja kubwa kwamba chama tawala kimeondoka madarakani na wengine kwenda mbali zaidi na kusema 'Kabila habari yake imekwisha'

Kwa wafuatiliaji na wachambuzi waandamizi wa masuala ya kisiasa hasa za Kiafrika watakubaliana nami kwamba kilichofanyika ni Rais aliyeondoka madarakani KABILA kupiga chenga ya mwili akili za Wapinzani nchini Kongo na Afrika kwa ujumla sambamba na Mataifa ya nje ambayo kila kunapokucha hayapendi kuona taifa hilo likiwa katika hali ya amani na utulivu kwani kunaweza kuwa kikwazo kikubwa katika wizi wa madini yaliyojaa tele katika taifa hilo la Afrika ya kati.

kabila alipigaje hiyo chenga ya mwili?

Kutafuta mshindi ambaye atalinda maslahi yake binafsi na watu wa Kongo, ikumbukwe kanisa katoliki nchini Kongo na Ufaransa kwa nyakati tofauti yameeleza Mgombea aliyekuwa anawakilisha umoja wa Upinzani FAYULU ndiye aliyeshinda uchaguzi huo, Kama huo ndio ukweli ni wazi baada ya Kabila kubaini mgombea wake(SHANDRY) ameshindwa huku FAYULU akiwa na kura nyingi, akifuatiwa na TSHESEKEDI alichokifanya ni kuchagua shetani moja kati ya wawili( rejea theory of the lesser evil) na kwa mazingira yalivyokuwa akaamua kumtangaza TSHESEKEDI kuwa mshindi akiamini msimamo wake dhidi yake(kabila) ni AHUENI ikilinganishwa na FAYULU ikumbukwe kuwa TSHISEKEDI alikuwa tayri na uhasama na umoja wa vyama vya Upinzani ukiongozwa na FAYULU baada ya kumzuia kupeperusha bendera ya umoja huo licha ya kuwa maarufu na wafuasi wengi.

Ni nini kimetokea na kitatokea baada ya chenga hiyo ya mwili?

i) wananchi, vyama vya Upinzani na wakosoaji wakubwa wa kabila sambamba na mataifa ya nje yaliyokuwa yanampiga hayaongei lugha moja yanapingana yenyewe badala ya Kabila!!!!!!!

ii)Ni vigumu sasa kwa mataifa ya nje kutoa mashinikizo kwa tume ya uchaguzi kurudia uchaguzi zaidi ya kukosoa mwenendo wa uchaguzi haukuwa wa haki n.k kwanii bado aliyeshinda ni kutoka Upinzani Kama mataka ya awali ya Nchi hizo.

iii)TSHESEKEDI ataapishwa na kulinda maslahi mapana ya wakongomani pamoja na yale ya Kabila.

Kabila katoa funzo kubwa kwa Afrika kwamba tunaweza kulinda maslahi yetu mapana ya wananchi wetu pasipo kuleta kusababisha umwagaji damu, vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo hutoa fursa kwa mataifa ya nje kuvuruga amani na utulivu wa nchi zetu.
 
serio

serio

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2011
Messages
6,418
Likes
1,639
Points
280
serio

serio

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2011
6,418 1,639 280
Nelson nely

Nelson nely

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Messages
4,027
Likes
2,289
Points
280
Nelson nely

Nelson nely

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2014
4,027 2,289 280
...kama ni kweli basi huyo Kabila sr.alikuwa mshenzi

Sent using Jamii Forums mobile app
ni Kweli Mkuu,baba Yake Joseph Alikuwa Ni Mtusi Wa Rwanda Na Alikuwa Akiongoza Kikosi Chake Cha Waasi Kilichokuwa Kikipambana Dhidi Ya Serikali Ya Bwn Ndadaye Wa Burundi.Makubaliano Yakafikiwa Kati Ya Kikundi Cha Kabila Sr Na Kile Cha Babake Jose Kwamba Waungane Wamng'oe Mobutu Then Kabila Amsaidie Babake Jose(kanembe) Kumng'oa Ndadaye Burundi.Kabla Hawajafanikisha Ndipo Kanembe Akakutwa Na Madhira Hayo.Kabila Sr Akawaahidi Vyeo Mbalimbali Askari Waliobaki Wa Babake Jose Ili Waendelee Kuwa Wamoja Lakini Aliotwaa Madaraka Aliwasahau Kabisa Kabisa.Ukienda Drc Kuna Kamsemo Maarufu"afadhali Angekuwepo Kanembe"..Huu Msemo Ulianza Jeshin Kipindi Kabila Yu Hai,wakamuonya Hakuonyeka,akavimba Kichwa,wakampasua,maana Jeshi Lilishaingia Utusi Na Uzawa!Hili La Utusi Likapewa Kampan Na PK,Likamtwaa Jose Habari Ikaishia Hapo.
 
IGWE

IGWE

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2011
Messages
8,685
Likes
2,799
Points
280
IGWE

IGWE

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2011
8,685 2,799 280

...unaonekana unajua mengi sana mkuu
....anyway_itoshe tu kusema asante sana kwa elimu hii ya historia uliyotupa bure...Jah bless the dead

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nelson nely

Nelson nely

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Messages
4,027
Likes
2,289
Points
280
Nelson nely

Nelson nely

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2014
4,027 2,289 280
Kabila alichomfanya Shandry, ni sawa na JK alichomfanya mtoto wa mkulima... Alimuomba achukue form akijua haupati urais hata kwa dawa...

Sent using Jamii Forums mobile app
ndiyo Ukweli Na Hata Kabila Alishafanya Makubaliano Kitambo Tu Na Tshisekedi Na Si Majuzi Kama Watu Wanavyodai,huwezi Amini Makubaliano Hayo Yaliyoambatana Na Mkataba Maalum Yalifanyika Kabla Ya Kabila Kumtangaza Shadary!Na Kitu Cha Kuchekesha Zaidi Ni Kuwa Hata Shadary Mwenyewe Anaufahamu Mkataba Huo Na Ni Mmoja Wa Mashuhuda Wa Utiwaji Saini!Ilikuwa Kwamba Kama Akishinda Shadary Na Felix Ameula Pia,na Kama Akishinda Felix Basi Kabila Na Shadary Wangeula Ila Kupitia Mlango Wa Nyuma Kwamba Bado Kabila Angedhibiti Jeshi Na Usalama Wa Taifa.
 
myoyambendi

myoyambendi

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2013
Messages
67,334
Likes
325,836
Points
280
myoyambendi

myoyambendi

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2013
67,334 325,836 280
Masikini Joseph Kabila...Nakumbuka Baba Yake Jose Alizamishwa Ziwa Tanganyika Akiwa Mahututi Kwa Amri Ya Laurent Desire Kabila,Baada Ya Jaribio La Kumtoa Madarakani Bwana Mobutu Kufeli Vibaya Na Askari Takriban 200 Wa Kabila Sr Wakiongozwa Na Marehemu Baba Yake Mzazi Wa Jose Kuuwawa,ndipo Babake Jose Akarudishwa Kambini Msituni Kuripoti Kwa Kabila Akiwa Amevunjika Miguu Yote!Ndipo Laurent Kabila Akawaagiza Askari Wake Wampakie Kwenye Boti Wamkimbize Ujiji Kigoma Apate Matibabu(ila Akawaamuru Wakifika Katikati Ya Ziwa Wamtupe Humo Halafu Warudi)Ndipo Mzee Kabila Akamtwaa Mke Wa Marehemu,marceline,Joseph Pamoja Na Dada Yake Akaja Kuwabwaga Msasani Daresalaam Kama Wanawe Kisha Akarudi Uwanja Wa Mapambano.Baadaye Joseph Alikuja Kuelewa Mazingira Ya Kifo Cha Babake Na Matatizo Yakaanzia Hapo! Rip Laurent.."mwanao" Alipendwa Zaidi Na Wanajeshi Wako Vile Hukuwatekelezea Ulichowaahidi Mlipokuwa Mngali Msituni,ukawajibu Nyodo Nao Wakasanua Kwa "mwanao" Ukweli Kwamba Wewe Si Baba Yake Na Baba Yake Ulimzamisha Ziwani!!
duh! hii habari kubwa sana..
 
myoyambendi

myoyambendi

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2013
Messages
67,334
Likes
325,836
Points
280
myoyambendi

myoyambendi

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2013
67,334 325,836 280
ndiyo Ukweli Na Hata Kabila Alishafanya Makubaliano Kitambo Tu Na Tshisekedi Na Si Majuzi Kama Watu Wanavyodai,huwezi Amini Makubaliano Hayo Yaliyoambatana Na Mkataba Maalum Yalifanyika Kabla Ya Kabila Kumtangaza Shadary!Na Kitu Cha Kuchekesha Zaidi Ni Kuwa Hata Shadary Mwenyewe Anaufahamu Mkataba Huo Na Ni Mmoja Wa Mashuhuda Wa Utiwaji Saini!Ilikuwa Kwamba Kama Akishinda Shadary Na Felix Ameula Pia,na Kama Akishinda Felix Basi Kabila Na Shadary Wangeula Ila Kupitia Mlango Wa Nyuma Kwamba Bado Kabila Angedhibiti Jeshi Na Usalama Wa Taifa.
Siasa za kusini mwa jangwa la sahara...
 
F

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Messages
2,245
Likes
1,731
Points
280
F

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined Jun 27, 2017
2,245 1,731 280
ni Kweli Mkuu,baba Yake Joseph Alikuwa Ni Mtusi Wa Rwanda Na Alikuwa Akiongoza Kikosi Chake Cha Waasi Kilichokuwa Kikipambana Dhidi Ya Serikali Ya Bwn Ndadaye Wa Burundi.Makubaliano Yakafikiwa Kati Ya Kikundi Cha Kabila Sr Na Kile Cha Babake Jose Kwamba Waungane Wamng'oe Mobutu Then Kabila Amsaidie Babake Jose(kanembe) Kumng'oa Ndadaye Burundi.Kabla Hawajafanikisha Ndipo Kanembe Akakutwa Na Madhira Hayo.Kabila Sr Akawaahidi Vyeo Mbalimbali Askari Waliobaki Wa Babake Jose Ili Waendelee Kuwa Wamoja Lakini Aliotwaa Madaraka Aliwasahau Kabisa Kabisa.Ukienda Drc Kuna Kamsemo Maarufu"afadhali Angekuwepo Kanembe"..Huu Msemo Ulianza Jeshin Kipindi Kabila Yu Hai,wakamuonya Hakuonyeka,akavimba Kichwa,wakampasua,maana Jeshi Lilishaingia Utusi Na Uzawa!Hili La Utusi Likapewa Kampan Na PK,Likamtwaa Jose Habari Ikaishia Hapo.
Huweleweki, unasema babake ni kutoka Rwanda huku akipambana Ndadai wa Burundi. Kwanini autake urais wa Burundi na sio Rwanda? Ndadai alionngoza Burundi mwaka 1993 na kuuwawa mwaka huohuo. Tayari Kabila na familia yake wapo Dar siku nyingi miaka ya 70. Sijakuelewa ujue!! Jipange ulete habari kamili.
 
Nelson nely

Nelson nely

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Messages
4,027
Likes
2,289
Points
280
Nelson nely

Nelson nely

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2014
4,027 2,289 280
Huweleweki, unasema babake ni kutoka Rwanda huku akipambana Ndadai wa Burundi. Kwanini autake urais wa Burundi na sio Rwanda? Ndadai alionngoza Burundi mwaka 1993 na kuuwawa mwaka huohuo. Tayari Kabila na familia yake wapo Dar siku nyingi miaka ya 70. Sijakuelewa ujue!! Jipange ulete habari kamili.
nahitaji Muda Kukuelezea Uelewe,sina Kwa Sasa,ila Naahidi Kuweka Maelezo Marefu Hapa Baadae Naamini Utapata Ufafanuzi Mzuri Tu Mkuu.
 
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
1,508
Likes
5,075
Points
280
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
1,508 5,075 280
ndiyo Ukweli Na Hata Kabila Alishafanya Makubaliano Kitambo Tu Na Tshisekedi Na Si Majuzi Kama Watu Wanavyodai,huwezi Amini Makubaliano Hayo Yaliyoambatana Na Mkataba Maalum Yalifanyika Kabla Ya Kabila Kumtangaza Shadary!Na Kitu Cha Kuchekesha Zaidi Ni Kuwa Hata Shadary Mwenyewe Anaufahamu Mkataba Huo Na Ni Mmoja Wa Mashuhuda Wa Utiwaji Saini!Ilikuwa Kwamba Kama Akishinda Shadary Na Felix Ameula Pia,na Kama Akishinda Felix Basi Kabila Na Shadary Wangeula Ila Kupitia Mlango Wa Nyuma Kwamba Bado Kabila Angedhibiti Jeshi Na Usalama Wa Taifa.
Iko hivi, Ukishakalia kile kiti kinachoitwa Uraisi, Ukishapanga Safu zako vizuri kwenye vyombo vya usalama huwa hakuna cha fulani au fulani ndiye aliyekubeba kukaa hapo ulipo, Yaani wewe ni mtu level nyingine kabisa!, BWM na JKN ni mfano mmojawapo
 
F

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Messages
2,245
Likes
1,731
Points
280
F

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined Jun 27, 2017
2,245 1,731 280
nahitaji Muda Kukuelezea Uelewe,sina Kwa Sasa,ila Naahidi Kuweka Maelezo Marefu Hapa Baadae Naamini Utapata Ufafanuzi Mzuri Tu Mkuu.
Sawa, ondoa utata na mkanganyiko. Upo sahihi kiasi fulani ila pia umetuchanganya.
 
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Messages
2,670
Likes
2,136
Points
280
Age
55
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2013
2,670 2,136 280
Kabila alikuwa na Plan A ambayo ilikuwa ni kung'ang'ania madarakani ambayo ilifeli, akawa na Plan B kumpachika kibaraka wake Shadary nayo ikafeli, akaja na hii Plan C ya kum-shortchange Fayulu ambayo ndio kama imefaulu japo kwa muda.

Itabidi huyu Tshisekedi asome vizuri alama za nyakati akijua kwamba hakua chaguo sahihi la wacongomani na kama atajaribu kuwa rais wa cheo ila mamlaka akamuachia Kabila, basi hapo atakuwa amejitia kitanzi.

Itabidi watu, pamoja na taasisi yenye nguvu kama kanisa la Roman Catholic sambamba na wazungu wamvurugie "Party" tena mapema kabisa hatua ambayo yeye Tshisekedi hataweza kuivumilia na itampelekea nguanzisha Plan D ambayo haitamuacha salama Kabila na wapambe wake ambao wana tuhuma nyingi za ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Huyo Tshisekedi ili atawale inabidi atafute muafaka na kanisa pamoja na nchi za magharibi, hili hawezi kuliepuka hata afanyeje, because they call the shots.
 
F

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Messages
2,245
Likes
1,731
Points
280
F

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined Jun 27, 2017
2,245 1,731 280
Mimi nionavyo, kama kuna mkataba kati ya Kabila na Tshekedi utakuwa wa muda tu kwani kelele hizi nyingi zitamshtua Tshekedi na kumtosa Kabila. Ni suala la muda tu. Pia mahakama ya kikatiba washajua Kabila ni fungu la kukosa hivyo rufaa ya Fayulu inaweza ikaibua jambo litakalomuacha kabila mdomo wazi. Tusikilizie!
 
Forum statistics

Threads 1,250,884
Members 481,523
Posts 29,749,538