Odhiambo cairo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,989
- 22,057
Wafuasi wa ma DICTATOR mnajitoa ufahamu, mpaka mnakera. Sisi hapa kwetu Tz katiba na tume yetu ni mbovu kupita kiasi . Lakini eti bado mna comment kuhusu chenga za Kabila kwa wa Zaire ?! . This is nonsense .Ukimwaga mboga tunamwaga ugali. Chenga uliyowapiga wakoloni mamboleo hakika ni ya kimataifa na imethibitisha wewe ni mwanaume ambaye hujakubali kuwa mnyonge mbele ya mabeberu.
Soma kwa makini
Iko hivi, rais aliyemaliza mda wake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila aliwekewa vikwazo vingi na mataifa ya ulaya kwa madai ya uminyaji wa demokrasia na kung'ang'ania madaraka ndipo Kabila aliamua kutangaza tarehe rasmi ya kufanyika uchaguzi na jambo lililowafurahisha wengi ni pale alipotangaza kuwa hatashiriki katika uchaguzi huo kama mgombea wa kiti cha urais kwakuwa muhula wake ushaisha kwa mujibu wa katiba ya Congo.
Uchaguzi uligubikwa na mashinikizo na maswali mengi yaliyokosa majibu. Kelele nyingi zilipigwa na kuwaaminisha wakongo kuwa chama tawala hakifai kuendelea kuwepo madarakani kwani hata asipogombea Kabila wananchi waliaminishwa kuwa mgombea yeyote wa chama tawala atakuwa kibaraka wa Kabila. Nyuma ya pazia mataifa ya ulaya kwa kushirikiana na vibaraka wao kama vile Kanisa Katoliki nchini Kongo walimuandaa mgombea wao ambaye akipita ataendesha Congo kwa maslahi yao binafsi.
Kabila kwa kutambua hilo akajua wananchi wana chuki dhidi ya chama tawala hivyo akifanya figisu kumpitisha mgombea wa chama tawala Shadary Ramadhan basi itazua machafuko nchini Kongo lakini pia akipita Martin Fayulu wa upinzani ndiye mgombea wa nchi za ulaya wanaempenda, kwa kuona hilo kwamba wakoloni wamemwaga ugali kwa kumchafulia chama chake na kumwekea vikwazo nae akaamua kumwaga mboga kwa kufanya figisu kumpitisha Felix Tshisekedi Tshilombo ambae sio papeti wa wakoloni mambo leo.
Ndio maana bado mataifa ya ulaya hadi leo wanatilia shaka matokeo ya urais nchini Kongo ila wanaogopa kuweka wazi kwakuwa wataulizwa shaka zenu mmezitolea wapi wakati nyie sio tume ya uchaguzi?
Mwaga ugali namwaga mboga! #Bado_somewhere
Tuzungumzie shida zetu zinatutosha. Angalau wao wamethubutu ,sisi na ujinga wetu tutajaribu vipi kwa tume hii inayomilikiwa na mtu.
Sent using Jamii Forums mobile app