Jinsi Joseph Kabila alivyopiga chenga ya mwili, akili za wapinzani na mataifa ya Nje!

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,220
12,937
Naam Wapendwa Habari za Ijumaa..!
Tuangazie kile kinachoendelea pale Nchini Congo mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa na kumpa ushindi Tshisekedi. Mh Joseph Kabila karata alizozichanga inaonekana zinawavuruga mabeberu pamoja na mawakala wao!

Mabeberu inaonekana walileta michango yao mikubwa na kuwekeza kwa nguvu zote kwa chama kikuu cha Upinzani nchini Congo kupitia mgombea wake Martin Fayulu, Marekani alileta mpaka wanajeshi eti machafuko yakitokea waliende wananchi wake wanaoishi Congo..! Je! Marekani alikuwa na agenda yake ya siri kuleta wanajeshi wake pale Gabon?

Marekani sasa imetoa tamko rasmi ikiitaka CENI iwathibitishie kama kweli felix Tshikedi alishinda wakati huo huo Ufaransa nayo imesema mshindi hakuwa Felix Tshesekedi bali alikuwa Martin Fayulu! huku kanisa la RC nalo likitzungumza hayo hayo sawa na wakoloni wao!

Je, kabila alikuwa anajua mipango ya Mabeberu dhidi ya taifa lao la Congo kuwa wqnaushirika mkubwa na Martin Fayulu..?

Kwangu mimi uenda Kabila aliona hali ya hewa isichafuke bora Taifa libaki salama heri Felix Tshisekedi kuliko Martini Fayulu huku akijua kuwa endapo angetangazwa mshindi kupitia chama Tawala Emmanuel Ramazani Shadary Congo ingechafuka sana kwa vurugu na hiki uenda ata Marekani walikitarajia sasa mambo yamegeuka ghafla bila yeyote kutarajia na mshindi ni Felix Tshisekedi.
1547185921499.png
 
Kabla ya kuwasakama wazungu, tujiulize kwa dhati kabisa sisi waafrika, tunafanya nini kusaidia demokrasia ndani ya nchi zetu. Tukishindwa kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe tujiandae kusumbuliwa na hawa the so called mabeberu!
 
Kabila hana mapenzi na Kongo. Alichofanya ni kuingia makubaliano ya kulindwa na huyo Tshisekedi na kushirikiana naye kwenye serikali. Wakongo bado hawajapata fursa kamilifu ya kuamua hatma yao kama taifa. Kama ilivyo kwa mataifa mengi ya Africa, Tanzania ikiwemo.
 
Jana tume ya uchaguzi Nchini nKongo (CENI) ilimtangaza FELIX TSHISEKEDI kutoka chama cha Upinzani cha UDSP kuwa mshindi wa kiti cha Urais baada ya kupata kura milioni 7, akifuatiwa na MARTIN FAYULU kura milioni 6.4 aliyekuwa akiwakilisha Muungano wa vyama vya Upinzani huku mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na Rais anayemaliza muda wake EMMANUEL SHANDRY akiambulia milioni 4.4.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, wafuasi wengi wa vyama vya Upinzani Nchini Kama ambavyo ilitarajiwa hawakusita kuonesha furaha zao kupitia mitandao mbalimbali kwa hoja kubwa kwamba chama tawala kimeondoka madarakani na wengine kwenda mbali zaidi na kusema 'Kabila habari yake imekwisha'

Kwa wafuatiliaji na wachambuzi waandamizi wa masuala ya kisiasa hasa za Kiafrika watakubaliana nami kwamba kilichofanyika ni Rais aliyeondoka madarakani KABILA kupiga chenga ya mwili akili za Wapinzani nchini Kongo na Afrika kwa ujumla sambamba na Mataifa ya nje ambayo kila kunapokucha hayapendi kuona taifa hilo likiwa katika hali ya amani na utulivu kwani kunaweza kuwa kikwazo kikubwa katika wizi wa madini yaliyojaa tele katika taifa hilo la Afrika ya kati.

kabila alipigaje hiyo chenga ya mwili?

Kutafuta mshindi ambaye atalinda maslahi yake binafsi na watu wa Kongo, ikumbukwe kanisa katoliki nchini Kongo na Ufaransa kwa nyakati tofauti yameeleza Mgombea aliyekuwa anawakilisha umoja wa Upinzani FAYULU ndiye aliyeshinda uchaguzi huo, Kama huo ndio ukweli ni wazi baada ya Kabila kubaini mgombea wake(SHANDRY) ameshindwa huku FAYULU akiwa na kura nyingi, akifuatiwa na TSHESEKEDI alichokifanya ni kuchagua shetani moja kati ya wawili( rejea theory of the lesser evil) na kwa mazingira yalivyokuwa akaamua kumtangaza TSHESEKEDI kuwa mshindi akiamini msimamo wake dhidi yake(kabila) ni AHUENI ikilinganishwa na FAYULU ikumbukwe kuwa TSHISEKEDI alikuwa tayri na uhasama na umoja wa vyama vya Upinzani ukiongozwa na FAYULU baada ya kumzuia kupeperusha bendera ya umoja huo licha ya kuwa maarufu na wafuasi wengi.

Ni nini kimetokea na kitatokea baada ya chenga hiyo ya mwili?

i) wananchi, vyama vya Upinzani na wakosoaji wakubwa wa kabila sambamba na mataifa ya nje yaliyokuwa yanampiga hayaongei lugha moja yanapingana yenyewe badala ya Kabila!!!!!!!

ii)Ni vigumu sasa kwa mataifa ya nje kutoa mashinikizo kwa tume ya uchaguzi kurudia uchaguzi zaidi ya kukosoa mwenendo wa uchaguzi haukuwa wa haki n.k kwanii bado aliyeshinda ni kutoka Upinzani Kama mataka ya awali ya Nchi hizo.

iii)TSHESEKEDI ataapishwa na kulinda maslahi mapana ya wakongomani pamoja na yale ya Kabila.

Kabila katoa funzo kubwa kwa Afrika kwamba tunaweza kulinda maslahi yetu mapana ya wananchi wetu pasipo kuleta kusababisha umwagaji damu, vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo hutoa fursa kwa mataifa ya nje kuvuruga amani na utulivu wa nchi zetu.
 
Ambacho hakifahamiki pia ni kuwa Tshisekedi ni shemeji yake kabila kwa maana ameoa mwanamke wa kitusi. Hata wakati kabla kampeni hazijaanza, wawili hao walifanya vikao mara kadhaa kubwa ikiwa kumuandaa kuwa chaguo lake la kimkakati ili kuiunganisha DRC huku maslahi yake na chama tawala yakilindwa.

Wachambuzi na wanamkakati wa kisiasa wanasema Tshisekedi anatakiwa kuunda serikali ili kwa kuzingatia matakwa ya Rais Kabila maana ni ukweli kuwa hakuwa na nafasi ya kushinda ila Kabila aliitaka Tume ya uchaguzi na idara ya usalama kuhakikisha anaibuka mshindi.

Wanasema ikiwa kabila ataona Tshisekedi anaweza kumsaliti anaweza kummaliza kwa kutumia mwanya wa mgogoro baina yake na wanaoupinga ushindi wake ili ionekane ndio wamempoteza. Ifahamike katiba ya DRC inasema Rais akiuwawa aliyekuwepo ndiye ataendelea kuongoza nchi.....

Joseph Kabila ni master mind

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kabila aliona soo chama kimfie ndio maana kwanza alistaafu, akamwachia shadari kimfie na hayo unayoyasema yanawezekana maana kabila alikua huru hata kuchagua rafiki kimya kimya baada ya kuona chama chake kinaenda kufa, ila kumbuka hilo halifanyi au kumpa kinga hata ya kutokwenda the hague.!
 
unajua kabila alikuwa hapatani kabisa na kanisa la katoliki,na kanisa kwa sauti moja lilimuunga mkono fayulu hadharani,hivyo kabila alipna ni heri ampe tchisekedi na wakaongea nae masaa 4 kabla ya matokeo kutolewa na yalipotolewa tshisekedi alimsifu sana kabila na kumuita ndugu
sasa kanisa halitokubali na bahati mbaya fayulu alisema hana imani na mahakama za congo kwa madai ni vibaraka wa kabila,sasa hata akikata rufaa haotasaidia kitu
ngoma iliyopo ni hii je kanisa la katoliki litakaa kimya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaelekea mwandishi alikuwa na haraka na ana upeo mdogo sana kwenye masuala ya kimataifa .Kabila alipigaje chenga , Chagua la Kabila amepata nafasi ya pili ,na Kama angechaguliwa moja kwa moja angelinda maslahi ya Kabila,! Pressure toka jumuia ya kimataifa zilikuwa kubwa sana kwa Kabila ambaye alikea madarakani kwa zaidi ya muda unaotakiwa ilihali katiba haimruhuru
 
True....!
Nimesoma sehemu Tshisekedi akikiri kuwa ni kweli baada ya kula kupigwa na kabla ya Matokeo kutangazwa alikua na Mazungumzo na Serikali ya Kabila, mwenyewe akitetea kuwa ni kawaida, ilitokea kwa Mandela South Africa.....kwa nini iwe Nongwa kwa Congo..!?
 
Back
Top Bottom