Jinsi Joseph Kabila alivyopiga chenga ya mwili, akili za wapinzani na mataifa ya Nje!

ndiyo Ukweli Na Hata Kabila Alishafanya Makubaliano Kitambo Tu Na Tshisekedi Na Si Majuzi Kama Watu Wanavyodai,huwezi Amini Makubaliano Hayo Yaliyoambatana Na Mkataba Maalum Yalifanyika Kabla Ya Kabila Kumtangaza Shadary!Na Kitu Cha Kuchekesha Zaidi Ni Kuwa Hata Shadary Mwenyewe Anaufahamu Mkataba Huo Na Ni Mmoja Wa Mashuhuda Wa Utiwaji Saini!Ilikuwa Kwamba Kama Akishinda Shadary Na Felix Ameula Pia,na Kama Akishinda Felix Basi Kabila Na Shadary Wangeula Ila Kupitia Mlango Wa Nyuma Kwamba Bado Kabila Angedhibiti Jeshi Na Usalama Wa Taifa.

Iko hivi, Ukishakalia kile kiti kinachoitwa Uraisi, Ukishapanga Safu zako vizuri kwenye vyombo vya usalama huwa hakuna cha fulani au fulani ndiye aliyekubeba kukaa hapo ulipo, Yaani wewe ni mtu level nyingine kabisa!, BWM na JKN ni mfano mmojawapo
 
Kabila alikuwa na Plan A ambayo ilikuwa ni kung'ang'ania madarakani ambayo ilifeli, akawa na Plan B kumpachika kibaraka wake Shadary nayo ikafeli, akaja na hii Plan C ya kum-shortchange Fayulu ambayo ndio kama imefaulu japo kwa muda.

Itabidi huyu Tshisekedi asome vizuri alama za nyakati akijua kwamba hakua chaguo sahihi la wacongomani na kama atajaribu kuwa rais wa cheo ila mamlaka akamuachia Kabila, basi hapo atakuwa amejitia kitanzi.

Itabidi watu, pamoja na taasisi yenye nguvu kama kanisa la Roman Catholic sambamba na wazungu wamvurugie "Party" tena mapema kabisa hatua ambayo yeye Tshisekedi hataweza kuivumilia na itampelekea nguanzisha Plan D ambayo haitamuacha salama Kabila na wapambe wake ambao wana tuhuma nyingi za ufisadi na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Huyo Tshisekedi ili atawale inabidi atafute muafaka na kanisa pamoja na nchi za magharibi, hili hawezi kuliepuka hata afanyeje, because they call the shots.
 
Mimi nionavyo, kama kuna mkataba kati ya Kabila na Tshekedi utakuwa wa muda tu kwani kelele hizi nyingi zitamshtua Tshekedi na kumtosa Kabila. Ni suala la muda tu. Pia mahakama ya kikatiba washajua Kabila ni fungu la kukosa hivyo rufaa ya Fayulu inaweza ikaibua jambo litakalomuacha kabila mdomo wazi. Tusikilizie!
 
Kabla ya kuwasakama wazungu, tujiulize kwa dhati kabisa sisi waafrika, tunafanya nini kusaidia demokrasia ndani ya nchi zetu. Tukishindwa kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe tujiandae kusumbuliwa na hawa the so called mabeberu!
Demokrasia bila maendeleo ni ujinga mtupu na kelele Zinazoumiza masikio na vichwa vyetu.
 
ndiyo Ukweli Na Hata Kabila Alishafanya Makubaliano Kitambo Tu Na Tshisekedi Na Si Majuzi Kama Watu Wanavyodai,huwezi Amini Makubaliano Hayo Yaliyoambatana Na Mkataba Maalum Yalifanyika Kabla Ya Kabila Kumtangaza Shadary!Na Kitu Cha Kuchekesha Zaidi Ni Kuwa Hata Shadary Mwenyewe Anaufahamu Mkataba Huo Na Ni Mmoja Wa Mashuhuda Wa Utiwaji Saini!Ilikuwa Kwamba Kama Akishinda Shadary Na Felix Ameula Pia,na Kama Akishinda Felix Basi Kabila Na Shadary Wangeula Ila Kupitia Mlango Wa Nyuma Kwamba Bado Kabila Angedhibiti Jeshi Na Usalama Wa Taifa.
Imeleta logic now.
 
nahitaji Muda Kukuelezea Uelewe,sina Kwa Sasa,ila Naahidi Kuweka Maelezo Marefu Hapa Baadae Naamini Utapata Ufafanuzi Mzuri Tu Mkuu.
Naomba unitumie PM huo mfafanuo au kiweka nitag mana inaonyesha ni stori nzuri sana. Kweli Jf raha
 
Jana tume ya uchaguzi Nchini nKongo (CENI) ilimtangaza FELIX TSHISEKEDI kutoka chama cha Upinzani cha UDSP kuwa mshindi wa kiti cha Urais baada ya kupata kura milioni 7, akifuatiwa na MARTIN FAYULU kura milioni 6.4 aliyekuwa akiwakilisha Muungano wa vyama vya Upinzani huku mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na Rais anayemaliza muda wake EMMANUEL SHANDRY akiambulia milioni 4.4.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, wafuasi wengi wa vyama vya Upinzani Nchini Kama ambavyo ilitarajiwa hawakusita kuonesha furaha zao kupitia mitandao mbalimbali kwa hoja kubwa kwamba chama tawala kimeondoka madarakani na wengine kwenda mbali zaidi na kusema 'Kabila habari yake imekwisha'

Kwa wafuatiliaji na wachambuzi waandamizi wa masuala ya kisiasa hasa za Kiafrika watakubaliana nami kwamba kilichofanyika ni Rais aliyeondoka madarakani KABILA kupiga chenga ya mwili akili za Wapinzani nchini Kongo na Afrika kwa ujumla sambamba na Mataifa ya nje ambayo kila kunapokucha hayapendi kuona taifa hilo likiwa katika hali ya amani na utulivu kwani kunaweza kuwa kikwazo kikubwa katika wizi wa madini yaliyojaa tele katika taifa hilo la Afrika ya kati.

kabila alipigaje hiyo chenga ya mwili?

Kutafuta mshindi ambaye atalinda maslahi yake binafsi na watu wa Kongo, ikumbukwe kanisa katoliki nchini Kongo na Ufaransa kwa nyakati tofauti yameeleza Mgombea aliyekuwa anawakilisha umoja wa Upinzani FAYULU ndiye aliyeshinda uchaguzi huo, Kama huo ndio ukweli ni wazi baada ya Kabila kubaini mgombea wake(SHANDRY) ameshindwa huku FAYULU akiwa na kura nyingi, akifuatiwa na TSHESEKEDI alichokifanya ni kuchagua shetani moja kati ya wawili( rejea theory of the lesser evil) na kwa mazingira yalivyokuwa akaamua kumtangaza TSHESEKEDI kuwa mshindi akiamini msimamo wake dhidi yake(kabila) ni AHUENI ikilinganishwa na FAYULU ikumbukwe kuwa TSHISEKEDI alikuwa tayri na uhasama na umoja wa vyama vya Upinzani ukiongozwa na FAYULU baada ya kumzuia kupeperusha bendera ya umoja huo licha ya kuwa maarufu na wafuasi wengi.

Ni nini kimetokea na kitatokea baada ya chenga hiyo ya mwili?

i) wananchi, vyama vya Upinzani na wakosoaji wakubwa wa kabila sambamba na mataifa ya nje yaliyokuwa yanampiga hayaongei lugha moja yanapingana yenyewe badala ya Kabila!!!!!!!

ii)Ni vigumu sasa kwa mataifa ya nje kutoa mashinikizo kwa tume ya uchaguzi kurudia uchaguzi zaidi ya kukosoa mwenendo wa uchaguzi haukuwa wa haki n.k kwanii bado aliyeshinda ni kutoka Upinzani Kama mataka ya awali ya Nchi hizo.

iii)TSHESEKEDI ataapishwa na kulinda maslahi mapana ya wakongomani pamoja na yale ya Kabila.

Kabila katoa funzo kubwa kwa Afrika kwamba tunaweza kulinda maslahi yetu mapana ya wananchi wetu pasipo kuleta kusababisha umwagaji damu, vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo hutoa fursa kwa mataifa ya nje kuvuruga amani na utulivu wa nchi zetu.

unajuaje kama atalinda maslahi ya nchi yake?
 
Huweleweki, unasema babake ni kutoka Rwanda huku akipambana Ndadai wa Burundi. Kwanini autake urais wa Burundi na sio Rwanda? Ndadai alionngoza Burundi mwaka 1993 na kuuwawa mwaka huohuo. Tayari Kabila na familia yake wapo Dar siku nyingi miaka ya 70. Sijakuelewa ujue!! Jipange ulete habari kamili.
So deep

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Write your reply...kanisa katoliki acheni kuleta machafuko huko congo! Mmeanza kujipambanua kuwa, kweli nyinyi ni wawakilishi wa shetani.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom