Kipyenga cha kampeni za Uchaguzi wa DRC chapulizwa rasmi. Ungependa nani ashinde Urais kati ya Felix, Martin Fayulu na Moise Katumbi?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,811
Kama heading inavyojieleza.Kuna Wagombea takribani 25.

Hata hivyo Wagombea Wakuu ni wafuatao;

-Felix Tshisekedi (Rais anaegombea awamu ya 2)
-Moise Katumbi(Tajiri wa Madini)
-Martin Fayulu(Mgombea wa RC)

Binafsi napendelea Rais Felix Tshisekedi Ashinde na aendelee na awamu ya pili Kwa sababu amejitahidi kuunganisha Nchi licha ya Changamoto kubwa za kiusalama na mizozo ya Kisiasa kwenye Ndoa yake na Kabila.

Anaonekana anaipenda Nchi yake na sio kibaraka wa Wazungu na amejitahidi kupambana na Kibaraka wa Wazungu Rwanda.

Moise Katumbi ni mfanyabiashara mbinafsi na ambae hajui maisha ya shida na ataangalia maslahi yake binafsi zaidi.

Pia huyu Tajiri ana malengo ya kuigawa Congo Ili Jimbo lake la Katanga lijitenge so hafai.

Martin Fayulu huyu sio tuu ni kwamba ni mgombea wa Kanisa la RC huko DRC Bali ni kibaraka mtiifu wa Beberu USA maana amewahi kuwa boss wa kampuni ya mafuta ya Kimarekani ya Exxon Mobil.

Huyu bwana atauza Nchi Kwa USA na atakuwa anatumikia Vatican.

View: https://twitter.com/Jambotv_/status/1727313013185855979?t=UOgZ_lSVoFjrs1ukyGD0Xw&s=19

My Take
Bado Muungano wa kabila wanatakiwa kuamua wamuunge mkono nani kati Yao au wasimamishe mgombea wao.

Bora zimwi likujualo (Felix) halikuli likakwisha kuliko hao wengine lazima watamshughulokia Kabila na genge lake.
 
Back
Top Bottom