Jinsi gani ya kuprint pasport?

VPN USED2020OCTOBER28

JF-Expert Member
Oct 27, 2011
1,505
674
habari wadau!!! samahani nimepiga pasport ambazo zinaitaji ukiprint ziwe kwenye karatasi moja pasport kama 40 hivi sasa inabidi kila moja iwe na namba yake jina, jinsia na sehemu ya kusaini mwenye pasport! please naomba mniambie unawezaje print halafu kionekane vitu hivyo husika vyote?

naomba niwasilishe!!!
 
unaweza hata ukatumia microsoft word, photoshop, illustrator etc

kwa urahisi hapo tumia karatasi ya A3 ambayo ni sawa na sentimita 29.7 kwa sentimita 42

a3-paper-size-in-centimetres.jpg


kwa mahesabu ya haraka haraka hakikisha picha ya maandishi inakuwa na urefu wa approx sentimita 6 kwa 5

sentimita 6 kwenye 29.7 vitaingia vipande 5 na sentimita 5 kwenye 42 vitaingia 8 jumla itakuwa 40 kama unavyotaka.

mfano kama unatumia microsoft word, itabidi kwanza uende page layout halafu page size halafu more size ueke ukubwa wa karatasi. kwa inch a3 inakuwa 11.69 x 16.53

nakushauri A3 sababu ni kubwa halafu bei rahisi kuprint around 1000 hadi 1500.
 
Back
Top Bottom