Jinsi DC Sabaya alivyomnasa Afisa Ugani na mtandao wa kitapeli wa Q NET alivyochota mamilioni ya watu

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797


HAI, KILIMANJARO

Mkuu wa wilaya ya HAI, Mkoani Kilimanjaro Lengai ole Sabaya amemsweka ndani mtumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Dominica Mwapombe kwa tuhuma za kuendesha mtandao wa kitapeli na kufanikiwa kujipatia mamilioni ya fedha kutoka kwa walimu kwa njia ya udanganyifu.

Aidha ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru wilayani humo, kufanya uchunguzi wa kina juu tukio hilo na kuchukua hatua za kisheria.

Sabaya amefikia uamuzi huo Mara baada ya kupokea malalamiko ya watu mbalimbali wakiweno walimu waliofika ofisini kwake wakidai kutapeliwa na Mwapombe

Kupitia taasisi ya biashara ya Qnet Marketing ambapo yeye ni mwakilishi wake.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, Mwapombe ambaye ni afisa ugavi wa halmashauri hiyo amefanikiwa kuchota mamilioni ya fedha kutoka kwa walimu na wafanyabiashara (majina yamehifadhiwa) waliopo katika wilaya hiyo baada ya kuwashawishi na kufanikiwa kuwaunganisha na mtandao wa kibiashara wa Qnet.

Walimu wanne na mfanyabiashara mmoja waliohojiwa na mkuu huyo wa wilaya katika mkutano wa walimu uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, walidai kumpatia mtuhumiwa mamilioni ya fedha kwa makubaliano kwamba watapokea kiasi cha dola 200 kila mwezi na kwamba ili upate kiasi hicho lazima ulete mwanachama wawili ama watatu wa kujiunga na mtandao huo.

"Kuna walimu na wafanyabiashara wamefika ofisini kwangu kulalamika kutapeliwa na taasisi ya Qnet kupitia Mwampombe na wenzake kuna mwalimu amelipa kiingilio cha Sh. milioni 4.2, kuna aliyetoa Sh. milioni 4.3, mwingine amelipa Sh. million 3.5 na mwingine ametoa Sh. milion 1.6 "

"Hawa wote waliahidiwa kupokea sh, laki NNE kwa mwezi lakini tangu wametoa fedha hizo kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu hawajawali kupokea chochote kwa sababu hawajaleta wanachama, sasa huu ni utapeli kama matapeli wengine" alisema Sabaya.

Aliongeza kuwa mtandao huo wa Qnet haujasajiriwa kupitia wakala wa usajiri wa makampuni (BRELA), hii ni baada ya kupiga simu kwa mkurugenzi wa Brela, David Nyaisa ambaye kupitia simu ya mkuu huyo wa wilaya iliyokuwa imewekwa sauti alithibitisha kuwa kampuni hiyo haina usajiri.

Mmoja ya walimu hao(Jina limehifadhiwa) akiongea katika mkutano huo,alisema alishawishiwa na rafiki yake kujiunga na mtandao huo na kutoa kiasi cha sh milioni 4.3 kwa mtuhumiwa ,akiahidiwa kupokea dola 200 kila mwezi baada ya kuwa ameleta wanachama wengine huku akipewa zawadi ya saa na cheni.

"Tangu nimetoa hii hela tarehe 5mwezi wa kwanza mwaka huu sijaona hela yoyote nimeingiziwa kwenye akaunti yangu na kila nikiwafuata kuwaomba hata lisiti wanadai nitaingiziwa kwenye mtandao ,nakuomba mheshimiwa unisaidie maana ndoa yangu ipo mashakani" Alisema mmoja ya wahanga wa tukio hilo.

Kwa upande wa mtuhumiwa ambaye ni mwakilishi wa Qnet alisema kuwa kampuni hiyo ni ya kibiashara na imesajiriwa kwa ajili ya kufanya biashara kwenye mtandao.

"Kwanza Mimi sio mwajiriwa wa Qnet ni mwakilishi huru na hii biashara niyakwenye mtandao hata kwenye ilani ya 61 ya ccm inaeleza mkakati wa kuimarisha biashara ya kwenye mtandao" alisema Mwapombe.

Ends...

Picha 1 ,DC Sabaya
Picha 2,Mtuhumiwa wa utapeli wakati akihojiwa.
Picha 3,Mhanga wa utapeli akielezea jinsi alivyotapeliwa.

IMG_20201210_143925_3.jpg
IMG_20201210_151625_4.jpg
IMG_20201210_151633_4.jpg
 
Sawa mkuu umenena, ila tusiwatukane walimu hawa maana mazingira ya kufanya biashara Tanzania ni magumu kiasi mtu anaogopa anaweza kuiingiza hiyo 4.3M kwenye biashara na isirudi hivyo wanapotokea watu wa kusema watamuwezesha kuvuna faida toka kwayo ni rahisi kushawishika!
Mbona Qnet imejadiliwa humu sana na sarakasi zake hao waalimu walishindwa hata kutafuta wasifu wa iyo kampuni mitandaoni.

Eti upate dola 200 kwa mwezi ukiwa umekaa tu pumbavu zao.
 
Kwahiyo ameona aimarishe biashara ya mtandao kama ilani ya ccm inavosema kweli huyo mwapombe kiboko
Sabaya mbona anamuadhibu kijana Safi hivi anayetekeleza ilani ya CCM? Ipo kwenye ilani ya CCM.

Yaani walimu hawa nao ni tatizo pia. Ningekuwa mkuu wa wilaya ningewaweka ndani wao kwanza. Una mil 4.5 halafu unashindwa kuzifanyia jambo zikupe faida badala yake unapeleka kwa MwanaCCM?
 
Walimu wasihukumiwe kwa kujumishwa. Sio watu wote wana access na Jamiiforums. Mwaka 2017 na mimi nilipelekwa kwa hao Qnet kule kwa Warioba na jamaa yangu mmoja alikuwa mtumishi tena mkubwa tu halmashauri.

Ofisi zilikuwa kwa Warioba. Tulipofika pale kanisa siyo kabisa afu wanaongea lugha za ajabu. Nikawasikiliza mpaka mwisho nikajiondokea zangu.
 
Watu wanaotapeliwa hivi sio wa kuwaonea huruma, ni kuwaacha tu wawe masikini. Wajinga wakubwa, mnakuwa walimu alafu mnashindwa kujiongeza tu kidogo kujua uongo na ukweli.
 
Back
Top Bottom