Jinsi counter wa baa alivyoibiwa pesa

Jinsi counter wa baa alivyoibiwa pesa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,713
Reaction score
57,233
Alienda mtu kunywa pombe ikumbukwe sio mteja wa pale hafahamiki. Akiendelea kunywa akaanza kumuomba counter amuazime simu ili mpigie mtu amletee hela aendelee kunywa mdada wa counter katika utetezi wake anadai Mara ya kwanza alimnyima kwa madai simu haina salio jamaa akaendelea kusihi apewe tu amtumie meseji.

Haifahamiki Kama ni uchawi ulitumika au sayansi ya kumnyenga mtu kwa kumpa offer za bia ila dakika ya mwisho dada alimpatia simu na jamaa bila kupoteza muda akabadilisha namba ya simu iliyoandika the boss yeye akaeidit ikawa namba yake za boss. Tena zilikuwa kama tatu akazibadilisha zote akamrudishia simu. Wakaendelea kumwagilia moyo.

Asubuhi kufika meseji inaingia ikimtaka amwambie mauzo ya jana kapata shingapi dada akastaajabu kwanini leo iwe hivi wakati bosi hanaga kawaida ya kuulizia mahesabu huwa anakuja mwenyewe kuyafuatilia. Basi kwa kuwa bosi ni bosi akaambiwa ipo kiasi fulani laki tano.

Jamaa (boss) akamuamrisha aende kwa wakali atume fasta pesa kwenye namba fulani nyingine 07***** jina litakuja fulani fulani ili anunue vinywaji kwa bei rahisi kwani Kuna mtu anataka afunge bar yake pesa ikatumwa maelezo baadae yanakuja kuwa mengi Ila ndo tayari kesi ya utapeli imeshatokea.

Wale wenye biashara waambieni wanaowauzia wawe makini kuzoeana na mtu haraka maisha ya Sasa sio ya kumsaidia mtu simu yako usimuazime kabisa usije kupata shida ya matukio ya kihalifu.
 
Pole dada wa watu atakatwa mpaka basi
Mdada anamwambia boss amkate 200000 kila mwezi ambakishie 50000 Sasa sijajua itaishiaje hi kesi maana kesho wote na wahudumu wengine wanaitwa polisi wakatoe maelezo...ndo hapo nikapata nafasi pia ya kujua mshahara wa counter kumbe NI laki mbili na nusu
..me Nilikuwa najuaga labda laki moja tu
 
Back
Top Bottom