SoC02 Jinamizi: Rushwa ya ngono vyuoni

Stories of Change - 2022 Competition

Elisha Jilala

New Member
Jul 26, 2022
2
4
Swala la rushwa ya ngono vyuo vikuu na vyuo vya kati ni jinamizi linalozidi kuitafuna jamii yetu kila uchwao. Rushwa ya ngono si neno geni wala habari mpya kwa wafuatiliaji wengi wa mitandao ya kijamii.

Takwimu zinaonesha takribani wahadhiri zaidi ya ishirini (20) wa vyuo vikuu Tanzania kwa mwaka 2021/2022 walisimamishwa kazi kwasababu ya tuhuma za rushwa ya ngono huku wengine wakisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi.
Mfano. Kipande cha video kilichorushwa na mwanadada maarufu Mange kimambi, kupitia App yake maarufu "Mange Kimambi APP" ilimuonesha mhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) akiwa kitandani na mwanafunzi wake huku uchunguzi ukibaisha kuwa alifanya hivyo kwa kumuahidi matokeo mazuri mwanafunzi huyo. Zipo taarifa na habari kemkem zinazoshabihiana na tukio hilo. Je! Ni nini kinasababisha haya kutokea?

Sababu Zinazopelekea Rushwa ya Ngono Vyuoni
  • Mfumo wa uandaaji na ushahihishaji wa mitihani vyuoni, mhadhiri au mwalimu wa somo husika ana nafasi kubwa ya kuandaa mitihani na kutolea maamuzi juu ya matokeo ya mwanafuzi wake. Mwalimu hutunga mtihani na kusahihisha mtihani huku akipewa majukumu ya kutoa alama au marks za mwanafunzi kabla matokeo hayo hayajapitishwa na jopo la idara husika. Kwa mitihani ya chuo, ili ufanye mtihani wa mwisho ni lazima uwe na marks (course work) zinazokuruhusu kufanya mtihani wa mwisho wa mhula (semester) alama hizo hujumuisha, alama la majaribio na alama za semina na mahudhurio ya darasani. Ikitokea mwanafunzi kashindwa kufikisha alama hizo, mwalimu wa somo hufungua mlango wa malalamiko na wanafunzi hupata nafasi ya kwenda ofsini na kueleza shida zao. Wapo ambao huwekewa alama kimakosa, kupitia mlango wa malalamiko hutatuliwa shida zao. Lakini wapo wasichana ambao huitumia vyema nafasi hiyo kuwashawishi walimu ili wawape maksi na kuahidi kuwaridhisha kimwili. Hiyo ndiyo sababu kubwa inayotajwa huku sababu ndogo ndogo zikiambatanishwa ikiwemo. Tamaa za kimwili kwa wahashiri, uzembe wa wanafunzi na sababu nyinginezo.
Jinsi ya kuepuka Rushwa ya ngono Vyuoni
Soma kwa bidii ili kuepuka mazingira, kwa vyovyote au kwa namna yoyote kutegemea huruma ya mwalimu kuamua hatima ya ufaulu wako.

Vaa nguo za stala na zinazofunika vyema maungo ya mwili wako pale unapopeleka shida yako personal kwa mwalimu wako. Kwa kuwa hata walimu ni binadamu hujikuta katika wakati mgumu pale wanapotoa maamuzi katika mazingira ambayo mwanafunzi wake amevaa nguo fupi na zinazochora maumbo ya miili yao, hali inayowapa changamoto na kushindwa kujizuia.

Uendapo kwa .walimu wako kupeleka shida zako binafsi usiende peke yako. Ambatana na wenziyo japo hata mmoja. Hata kama mwenziyo atazuiwa kuingia basi mwambie akusubiri nje ya mlango. Hii itakuwa salama zaidi kwako.

Uonapo dalili za kuombwa rushwa ya ngono, toa taarifa kwenye uongozi wa chuo au uongozi wa serikali ya wanafunzi. Pia unaweza kuandika barua na kuipeleka sehemu husika.
 
Ushauri mzur sana kwa wanafunzi
 
Hakuna anaebakwa wanatoa wenyewe tena wanafurahia. Umeshasikia mtu kahukumiwa sababu hiyo. Acheni wivuuu.
 
Back
Top Bottom