Jina la Sabaya lasimamisha kesi kwa muda

Pamoja na kuwa mkongwe chamani na Serikalini, lakini nami ni mjuzi na msomi wa sheria. Nilimaliza sheria miaka ya themanini na kuifanyia kazi hadi miaka ya mwishoni mwa tisini. Najua ninachokiandika hapa. Nina hakika na nikiandikacho hapa.

Amini nawaambia, Lengai Ole Sabaya 'ameshaachiwa' kisheria. Punde tu atakuwa mtu huru na atatamba na kubamba kuliko pamba. Hataachiwa kutokana na udhaifu wa ushahidi wa mashtaka. Hataachiwa kwakuwa utetezi wake una mashiko kama mwiko.

Sote tumeshuhudia jinsi kesi nzito na yenye mashiko ilivyojengwa na akina Kweka wa Jamhuri. Tumeshuhudia na kusikia jinsi utetezi wa Sabaya ulivyokuwa mwepesi kama karatasi. Lakini, Sabaya ataepuka kukutwa na hatia kama si Mahakama inayomsikiliza sasa basi ni ambayo watakata rufaa.

Sabaya ataachiwa kwa suala la kisheria. Baada ya kutokea mabishano ya kisheria kuhusu jina la Sabaya kukosewa, iliamriwa kuwa Sabaya asomewe maelezo yake upya. Akasomewa. Utetezi ukaendelea. Kuna kitu muhimu cha kisheria hakikufanyika. Mashahidi wa Jamhuri walipaswa kuitwa tena na kutoa ushahidi wao tena. Haikuwa hivyo.

Mashahidi walipaswa kuitwa upya kwakuwa Mshtakiwa 'amebadilishiwa' jina lake. Hawakuitwa na kesi inaendelea. Wao walitoa ushahidi dhidi ya Sayaba na si Sabaya. Kutoitwa tena kutatumika 'kumchomoa' Sabaya hapo au baada ya hapo. Ni suala la kisheria. Subirini mshuhudie jambo hili.

Askofu Gwajima hakamatiki?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kigoma Mjini)
 
Hata akiachiwa kwa muda aliokaa rumande atakuwa ameshajifunza kuwa hakuna aliye juu ya sheria, na kitumbua chake kimeshaingia mchanga anakuwa hana tofauti na raia mwingine wa kawaida. Na inawezekana ndio ukawa mwisho wa umaarufu wake labda aje Rais mwingine atakaye muelewa
Naunga mkono hoja maana miezi 4 inamtosha kabisa.
 
Ataishi maisha mabaya na kuwa na maadui wengi hatimae atakufa kifo kibaya mapema.
 
Typing error haibadilishi facts of the case. Waliofanya mistake ya jina hawakufanya mistake ya mtu. This is simply common sense.
Ukimrape mwanamke huponi kwasababu eti hakujui au katamka vibaya jina lako.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Hata akiachiwa kwa muda aliokaa rumande atakuwa ameshajifunza kuwa hakuna aliye juu ya sheria, na kitumbua chake kimeshaingia mchanga anakuwa hana tofauti na raia mwingine wa kawaida. Na inawezekana ndio ukawa mwisho wa umaarufu wake labda aje Rais mwingine atakaye muelewa
Usisahau pia kuwa raia na sisi tuna jambo letu tunamsubiri tu atoke
 
Back
Top Bottom