Jina 'BONGO' limetokana wapi?

Jongwe

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
1,039
659
Bongo/Wabongo hivi neno hili limetokea wapi na maana yake ni nini? Neno hili lilipoanza nilikuwa nikiishi kigoma, kipindi hicho kulikuwa na watanzania wengi walikuwa wakienda Karemii -Zaire (DRC kwasasa) kufanya biashara. Wakiwa kwenye hizo biashara mTZ alikuwa akikamatwa kwa makosa fulani fulani na akipewa nafasi ya kujitetea ilikuwa lazima ashinde. Wazairwaa wakawa wanasema watanzania waongo sana, sasa kusema neno muongo wao wanaita bongo. . Watanzania boongo sana. Sasa ikawa sisi waTZ ni Bongo (Wabongo) waongo, nchi yetu ikawa bongo yaani nchi ya waongo. Hivyo ndivyo mimi nijuavyo. Wewe je unajua neno hilo limetokea wapi?
 
Kuna theory nyingine niliisikia kuwa kuna mzungu alikua anafanya research yake ya economics. Alikuja Dar na kuishi kwa kima cha chini cha mshahara, alijibana sana sana, baada ya wiki mbili pesa ilikwisha kabisa. Aliuliza sasa watu wenye familia wanaishije kwa pesa hii, alijibiwa watu wanaishi kwa bongo yaani wanatumia ubongo. Ndio ikawa mwanzo wa jina hili.

Sifahamu ipi ni ya kweli kati ya hii na hiyo ya kwako.
 
Mi niliskia eti BONGO ni DSM, lakini nje huko wanajua BONGO ni Tanzania nzima. Wanasema eti chanzo ni maisha ya DSM kwamba yanahitaji akili nyingi sana kuyamudu, ndio wa mikoani wakaibatiza DSM -BONGO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom