Jongwe
JF-Expert Member
- Apr 25, 2008
- 1,040
- 662
Bongo/Wabongo hivi neno hili limetokea wapi na maana yake ni nini? Neno hili lilipoanza nilikuwa nikiishi kigoma, kipindi hicho kulikuwa na watanzania wengi walikuwa wakienda Karemii -Zaire (DRC kwasasa) kufanya biashara. Wakiwa kwenye hizo biashara mTZ alikuwa akikamatwa kwa makosa fulani fulani na akipewa nafasi ya kujitetea ilikuwa lazima ashinde. Wazairwaa wakawa wanasema watanzania waongo sana, sasa kusema neno muongo wao wanaita bongo. . Watanzania boongo sana. Sasa ikawa sisi waTZ ni Bongo (Wabongo) waongo, nchi yetu ikawa bongo yaani nchi ya waongo. Hivyo ndivyo mimi nijuavyo. Wewe je unajua neno hilo limetokea wapi?