Jimmy David Ngonya afariki dunia

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
jim.JPG



Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Simba na mfanyakazi wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Jimmy David Ngonya amefariki asubuhi hii. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN na pia awape nguvu na faraja mkewe, watoto na wajukuu wake, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu kwao. Tully, Ikupa na wengineo poleni sana kwa msiba mkubwa uliowafika.
 
RIP David
Poleni familia na ndugu wote mnaohusika na msiba huu
Mungu awajalie faraja kubwa wakati huu wa machungu ya moyoni
 
Amefariki alfajiri na nimepata habari asubuhi hii.Msiba uko kwa mwanawe Segerea.
RIP Jimmy David Ngoya
 
Kwa walio UK msiba uko kwa binti yake ambaye address yake ni hii: 38 Trelleck Road, Reading, RG1 6EN
 
RIP kamanda Jimmy David Ngonya tutakumbuka sna na kawasilimie wote waliotangulua
 
Rip Ngonya! Mcba upo segerea ukitoka town ukifika sanene unapita kushoto kwa mtoto wake.
 
RIP Jimmy David Ngonya, wakati akiwa simba aliitwa "Gorbachev" kutokana na msimamo wake...poleni sana wafiwa wote!
 
rip jimmy ila wakuu leo niaje aisee mbona misiba mingi hivi huu niwa sita mpaka sasa..
 
Katika uwanja wa michezo alipata kuwa Katibu wa Simba miaka ya 70 na akerejea katika nafasi hiyo katikati ya 80 moja ya mafanikio yanayokumbukwa wakati wa uongozi wake ni kuiongoza simba kama katibu mkuu kiufunga Al Ahly katikati ya miaka ya 80 huko Mwanza.
 
Back
Top Bottom