'Jimbo' gumu kwa CCM

'Jimbo' gumu kwa CCM

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Kuanzia kuwepo kwa vituo vya luninga vinavyorusha midahalo kutoka mahali hapa,sikuwahi kuona CCM na Serikali yake ikishinda kwa hoja. Nimekuwa nje ya Chuo Kikuu hiki kabla,baadaye nikawa mwanafunzi wa Chuo husika na baadaye kuhitimu.




Lakini,sikuwahi kuona CCM wala Serikali yake ikishangiliwa hapa,hasa katika mijadala ya kihoja hasa. Hapa sizungumzii hotuba za viongozi wa CCM na Serikali yake wanapokuja kuwakaribisha viongozi wenzao wa nje wanaokuja na kuhutubu katika 'jimbo' hili.




Ni Ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Mara nyingi,hasa kwenye midahalo,CCM na Serikali yake wamekuwa wakizomewa,kunyooshewa vidole na hata 'kushambuliwa'. Nimesimuliwa juu yakutupiwa machungwa mabovu kwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi katika miaka ya 80.




Nikashuhudia,nikiwa tayari si mwanafunzi tena ,Rais Kikwete ‘akizomewa' na kuoneshwa mabango akiwa na Rais Yoweri Museveni waUganda hapo hapo Nkrumah. Kiukweli, mahali hapa hapavutii kwa CCM na Serikaliyake.




Kiongozi yeyote wa CCM na Serikali yake hujifikiria mara mbili mbili anapotakiwa kuhutubu Nkrumah. Wakati mwingine hulazimika kuunga mkono hoja zisizo za kiserikali ili abaki salama. Kama wanazuoni hawa wanaowanyima raha viongozi wa CCM na Serikali yake wangetawanyika na kufanya ya Nkrumah mahali pengine ,nchi hii ingekuwa mbali sana. Lakini, wanazuoni hawa sijui hupotelea wapi?!
 
hawa wangoa kucha utawashangiliaje mkuu. hao wasomi nawasifu sana
 
Mkuu, hivi hujajua kuwa kwenye midahalo hiyo CHADEMA huandaa vijana wa kuzomea ili ionekane kuwa hoja za viongozi wa ccm ni dhaifu? Binafsi siamini kuwa chadema ndo huja na hoja nzuri zaidi. Halafu tabia za kuzomea si miongoni mwa sifa za wasomi. Kwa kawaida mru aliyepevuka kiakili husikiliza kila hoja kwa umakini na kuifanyia uchambuzi. We fuatilia tu kwenye midahalo hiyo. Wanafunzi wanaozomea mara zote hawaombi hata nafasi ya kuchangia
 
Mimi nikiwaona CCM na minguo yao mwili unasisimka, naona kama tayari wanataka kuning'oa kucha...

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mkuu, hivi hujajua kuwa kwenye midahalo hiyo CHADEMA huandaa vijana wa kuzomea ili ionekane kuwa hoja za viongozi wa ccm ni dhaifu? Binafsi siamini kuwa chadema ndo huja na hoja nzuri zaidi. Halafu tabia za kuzomea si miongoni mwa sifa za wasomi. Kwa kawaida mru aliyepevuka kiakili husikiliza kila hoja kwa umakini na kuifanyia uchambuzi. We fuatilia tu kwenye midahalo hiyo. Wanafunzi wanaozomea mara zote hawaombi hata nafasi ya kuchangia
shida unapotetea hata visivyotetewa umeambiwa kuanzia miaka ya 1980 sasa Chadema kilikuwepo miaka hiyo. Tendea haki buku 7 ya Lumumba mkuu
 
hawa wangoa kucha utawashangiliaje mkuu. hao wasomi nawasifu sana
Mkuu, hakuna msomi mwenye tabia za kushangilia na kuzomea. Akili hizo ni za bavicha ambako kumejaa vilaza
 
shida unapotetea hata visivyotetewa umeambiwa kuanzia miaka ya 1980 sasa Chadema kilikuwepo miaka hiyo. Tendea haki buku 7 ya Lumumba mkuu

anatendea haki huku 7 ya wakwepa kodi na wauza unga
 
Mkuu, hakuna msomi mwenye tabia za kushangilia na kuzomea. Akili hizo ni za bavicha ambako kumejaa vilaza
Sisi ndo bavicha wenyewe na tupo wengi na nina uhakika asilimia bilioni kwamba tunaakili kushinda wengi wenu.....hamtuwezi kishule....na mambo mengine mengi....labda ufisadi na kuuza unga....
 
Popote penye ufahamu,Ccm hujitenga!! Mf miji yote yenye watu walioelimika ni maadui wa ccm,wilaya zote zilizobahatika kuelimika ni maadui wa ccm,vyuo vikuu vyote na taasisi za elimu yajuu kote huko ccm ni adui!!! Ccm ina uhusiano mkubwa na UJINGA,sehemu pekee ambazo ccm wamezishika ni zile zilizotopea kwenye ujinga,find your own equation.
 
Mkuu, hivi hujajua kuwa kwenye midahalo hiyo CHADEMA huandaa vijana wa kuzomea ili ionekane kuwa hoja za viongozi wa ccm ni dhaifu? Binafsi siamini kuwa chadema ndo huja na hoja nzuri zaidi. Halafu tabia za kuzomea si miongoni mwa sifa za wasomi. Kwa kawaida mru aliyepevuka kiakili husikiliza kila hoja kwa umakini na kuifanyia uchambuzi. We fuatilia tu kwenye midahalo hiyo. Wanafunzi wanaozomea mara zote hawaombi hata nafasi ya kuchangia

Sidhani kama kuna ukweli kwenye hili.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mkuu, hivi hujajua kuwa kwenye midahalo hiyo CHADEMA huandaa vijana wa kuzomea ili ionekane kuwa hoja za viongozi wa ccm ni dhaifu? Binafsi siamini kuwa chadema ndo huja na hoja nzuri zaidi. Halafu tabia za kuzomea si miongoni mwa sifa za wasomi. Kwa kawaida mru aliyepevuka kiakili husikiliza kila hoja kwa umakini na kuifanyia uchambuzi. We fuatilia tu kwenye midahalo hiyo. Wanafunzi wanaozomea mara zote hawaombi hata nafasi ya kuchangia

Kwa hiyo wale waliomzomea Mwinyi miaka ya 80 waliandaliwa na CHADEMA?
 
Ongeza hapo......
Mulugo walimtimu wakati akienda kusolve tatizo la mgomo wakati level yake haiendani kabisa na wasomi hao.
 
[Q
Hiyo miaka ya 80 chadema walikuwepo... Akili ya samaki..UOTE=Lizaboni;6969916]Mkuu, hivi hujajua kuwa kwenye midahalo hiyo CHADEMA huandaa vijana wa kuzomea ili ionekane kuwa hoja za viongozi wa ccm ni dhaifu? Binafsi siamini kuwa chadema ndo huja na hoja nzuri zaidi. Halafu tabia za kuzomea si miongoni mwa sifa za wasomi. Kwa kawaida mru aliyepevuka kiakili husikiliza kila hoja kwa umakini na kuifanyia uchambuzi. We fuatilia tu kwenye midahalo hiyo. Wanafunzi wanaozomea mara zote hawaombi hata nafasi ya kuchangia[/QUOTE]
 
Ni kweli mkuu.. Ccm wanawatumia wajinga..
Popote penye ufahamu,Ccm hujitenga!! Mf miji yote yenye watu walioelimika ni maadui wa ccm,wilaya zote zilizobahatika kuelimika ni maadui wa ccm,vyuo vikuu vyote na taasisi za elimu yajuu kote huko ccm ni adui!!! Ccm ina uhusiano mkubwa na UJINGA,sehemu pekee ambazo ccm wamezishika ni zile zilizotopea kwenye ujinga,find your own equation.
 
unajua maana ya mwanazuoni? wale ni wanafunzi siyo wanazuoni. kwa bahati mbaya viroba vimezagaa mlimani. hata hivyo sikubaliani na ww. nimesoma pale na nimehudhuria makombano mengi baada ya chuo. mfano mfupi ni jinsi nnchimbi alivyo funika juzi
 
Mkuu, hivi hujajua kuwa kwenye midahalo hiyo CHADEMA huandaa vijana wa kuzomea ili ionekane kuwa hoja za viongozi wa ccm ni dhaifu? Binafsi siamini kuwa chadema ndo huja na hoja nzuri zaidi. Halafu tabia za kuzomea si miongoni mwa sifa za wasomi. Kwa kawaida mru aliyepevuka kiakili husikiliza kila hoja kwa umakini na kuifanyia uchambuzi. We fuatilia tu kwenye midahalo hiyo. Wanafunzi wanaozomea mara zote hawaombi hata nafasi ya kuchangia

Unatia huruma....
 
Back
Top Bottom