Jiji la Mbeya kama kijiji

Mbeya ni kichekesho kwa kweli. Hii tanzania marndeleo yapo dar es salaam tu , tena hapo dar kwenyewe ni sehemu chache pia. Ila huku sehemu zingine sio siri zimesahaulika kabisa
 
Hivi mnaoponda Mbeya mmefika kweli? Mtu unaishia stendi tayari unahukumu mji mbovu?
 
Kama unaenda kikazi bora kwenda na mkeo vinginevyo unaweza kuanguka dhambini
 
Wee Mkuu hayo maeneo uliyoyataja, ni maeneo wanayofikia watu wa level ya kati huenda hata wewe ndo level yako, mimi siyo mtu wa Mbeya ila huwa nakwenda sana Mbeya kwa ishu zangu, Mbeya Hotel ni Hotel iliyokua inatamba miaka ya 1980, na Paradise na GR hotel hazipo hata katika top100 ya Hotel za Mbeya. Watu waliokua wanakupeleka huko walikukadiria kwamba wewe ni wa level za hotel hizo kiongozi, hata mimi kwasababu ni mtumishi wa Umma nikiomba nifanyiwe booking napelekwa huko maana sehemu zote ulizo taja hakuna chumba cha zaidi ya Tshs100,000, na walishawahi kunipeleka kahotel flan kapo juu zaidi ya hizo kanaitwa Hill View Hotel nilichemsha bei japo kana mazingira mazuri kuliko hata Kempisky.
 
Bukoba beibiiiii
Huko ndo majanga....tena bora hapo bukoba mjini....nilitembelea wilaya ya muleba na biharamulo yani hamna kitu alafu watu wa kule wanajifanya wajanja kumbe hamna lolote...huduma zenyewe pale muleba km hujui kihaya utasumbuka sana..
 

Mbona hali ya vumbi arusha na mbeya ni kama sawa tu! Mfano kwa mromboo vumbi linagonga mpaka jua unaacha kuliona, kama ni mjini kuna baadhi ya barabara za rami zime wekwa 2012/13.. Squatters sanawari upande wa pili wa barabara kwa juu kuna nyumba za fito,na ni mjini,, kijenge na maeneo mengi tu,, mvua ikinyesha tope sasa daa::: lakini bdo naipenda arusha na naimiss mbeya
 
Hivi mnabishana kuhusu jiji la mbeya, mmefika jiji la Tanga? Samahani wadigo wenzangu na wakwe zangu wasambaa
[emoji15] [emoji15] mji wa Tanga umedumaa wala hauendelei..
huko hivyo hivyo tokea 1990s mpaka sasa. mjini majengo ni yaleyale wanaokaa waarabu maghorofani
 
miji yote ina mapungufu ila mbeya itasubiri sana kwa arusha....na hilo lipo wazi kwa waliotembelea sehemu zote hizi mbili ukiacha ushabiki...
 
hivi mbeya mjini ni wapi? huku stand uhindini,,au huku maeneo ya TRA? au mwanjelwa? kiukweli IRINGA MJINI NI KUZURI KUPITA MBEYA
 
mpaka leo pale SONGWE AIRPORT, wenyeji hujaa kwa MAELFU ili kushuhudia ndege ya FASTJET ikitua na kupaa tena wengine hudamka mapema sana na kutembea kilomita kadhaa kuwahi uwanjani, jambo hili limenihuzunisha na kunisikitisha sana baada ya kuwaona ndugu zetu wanyakyusa ushamba hauwatoki pamoja na kwamba uwanja unafikisha miaka zaid ya miwili sasa!!! Wanyakyusa inabid mupunguze ushamba kidogo jamani maan mnatia aibu sana. Au ndo mlishazoea TAZARA?
 

Jiji gani lisilo hata na shopping mall hata moja. Magari yaliyojaa mbeya ni vitz, passo, raumu ipsym nk. nimekaa mbeya zaidi ya mwaka sasa na bado nipo mbeya sijawahi hata kuiona range rover avoque. Matajiri wakubwa wanatembelea passo. Kwa kifupi mbeya huwezi kulinganisha na mwanza wala Arusha. Uwanja wa ndege mwanza kwa siku zinatua ndege zaidi ya 6 kubwa Arusha the same. Mbeya ni fast jet tu siku nyingine route moja siku nyingine 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…