Unavyosema bado jiji la Mbeya bado, pia unatakiwa ufatilie na ujue sera ya nchi na vipaumbele vyake katika mikoa tofauti.
Hivi unajua kuwa hata airport ya songwe ni Mzee Mwandosya aliye pigania kipindi alikuwa waziri wa mawasiliano na uchukuzi mpaka ikajengwa Mbeya.
Na kipindi hicho sumaye waziri mkuu alikuwa anataka ijengwe arusha.
Mbeya imeendelea sana na pia imejitosheleza kwa mambo mengi ila kwa kuwa hauyaoni majengo makubwa kama ilivyo sehem kama DSM, Mwanza n.k ndio unasema hivyo.
Mbeya hamna majengo makubwa mengi sababu ni
1. Eneo kubwa la jiji la Mbeya limepitiwa na bonde la ufa hivyo kwa kipindi cha nyuma ilikuwa ngum kujenga ghorofa zaidi ya 5 kwa kuwa mara nyingi huwa kuna tetemeko la ardhi ila kwa sasa technolojia imekuwa ndio mana unaona ghorofa zilizojengwa kwa vyuma jijini Mbeya kama ya maranatha pale mwanjelwa
2. Mbeya hamna majengo makubwa kama DSM, Mwanza n.k kwa sababu ya mgogoro wa mpaka na nchi ya malawi kwa kuwa huo mgogoro ni wa mda mrefu na malawi inaamini kuwa sehemu kubwa ya Jiji la Mbeya ni sehem ya malawi kwa hiyo serikali ya tanzania inaogopa kuwekeza sana jijini Mbeya ikiwa na hofu kama hiyo.
3. Sera ya nchi nayo imechangia kufanya jiji la Mbeya kuwa nyuma sababu serikali ya tanzania imetenga mikoa mitano kama mikoa maalum kwa kuzalisha chakula ikaipa jina la big 5 mikoa hiyo ni iringa, ruvuma, rukwa, njombe na jiji la Mbeya. Kwa hiyo hata maendeleo ya yanayoonekana sasa jijini Mbeya ni juhudi binafsi za wana Mbeya.
4. Ijulikane pia kwamba majengo makubwa kwenye miji mikubwa tanzania kama DSM, Mwanza n.k yamejengwa na taasisi kama NSSF, LAPF, PPF, NHC, PSPF, GEPF n.k hivyo kuonekana kama hiyo mikoa imejengeka, kwa jiji la Mbeya ni tofauti kwani hiyo mifuko haijafanya uwekezaji wowote katika jiji la Mbeya kidogo NHIC ndio wanajenga jengo lao kubwa pale town karibu na kwa mkuu wa mkoa hivyo bado wana Mbeya wanatakiwa kupongezwa kwa juhudi binafsi za kujenga mkoa wao kidogo hizi taasisi ndio zinaanza kuwekeza majengo Mbeya
5. Barabara kubwa za jiji la Mbeya hazijajengwa na serikali mfano ni barabara ya kutoka uyole hadi kasumulu mpaka wa tanzania na malawi imejengwa na umoja wa afrika kwa sera ya umoja huo kuwa na barabara itakayoutambulisha umoja huo iliyoanzia Cairo nchini Misri hadi Cape town South Africa ikipita pia nchini tanzania jijini Mbeya, pia kuna barabara iliyojengwa kutoka jijini Mbeya kutokea eneo la isanga hadi wilayani chunya pia ilijengwa kwa msaada wa watu wamisri wenyeji wa mkoa wa mbeya wanajua tabu waliyoipata kwenda huko chunya. Pia kuna barabara inayoelekea airport ya zamani pale chuo cha T.I.A
6. Pia tunajua kuwa kwa nchi yetu ya tanzania sehem kubwa ya mambo ya maendeleo yanafanyika kisiasa kuliko kimkakati hivyo tunaona maeneo ambayo walikuwa wanatokea viongozi wakubwa wa nchi wenye ushawishi serikalini yalikuwa yanapewa kipaumbele mfano ma waziri wakuu awamu zote, na maraisi tunaona hata sasa JK alivyojaribu kuinua mkoa wa pwani kwa namna moja, pia tunaona mawaziri wakuu kama msuya, sumaye, lowasa, n.k kupeleka project kubwa maeneo wanayotokea kwa jiji la Mbeya halijawahu kutoa Raisi au waziri mkuu, katika miji iliyoendelea nafikiri mwanza haiko kisiasa sana labda JPM nae akiamua afanye yake.
Kwa jiji la Mbeya lilipofikia nafikiri ilitakiwa kupongezwa sio kubezwa na serikali kuweka sera za maendeleo sawa katika miji mikubwa yote kuliko kuipa kipaumbele mikoa michache mfano hai tunaona raisi JPM tangu amekuwa Raisi ni mara mbili anaenda arusha na wakati huo huo kuna mikoa hajawahi kukanyaga tangu awe raisi kwa hali kama hiyo tayari inawahamasisha hata wawekezaji sababu ya safar kama hizo za mkuu wa nchi mara nyingi eneo moja.
Note: watu wanaoongelea mambo ya uchawi jijini Mbeya nafikiri pia waangalie katika tanzania sehemu mikoa gani wakongwe wanakufa sababu ya hizo imani, pia ni mikoa gani albino wanaongoza kukatwa viungo nafikiri maeneo yenye hizo tamaduni hasa ni tanga, sumbawanga, shinyanga, DSM n.k mara, kigoma n.k tamaduni za ushirikina zipo jijini Mbeya ila sio kama wadau wanavyosema
Ni
Nitarudi badae.
Chuma Ulete ndo sana huko MBEYA